Raia wa jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo wanaanza siku mbili ya maombolezi ya kitaifa, kufuatia vifo vya watu mia mbili thelathini kwenye mlipuko wa lori ya mafuta mashariki mwa nchi hiyo.
Kuna hofu kuwa idadi hiyo ya maafa ikaongezeka.
Madaktari mkoani Kivu wanaendelea kuwahudumia mamia ya majeruhi wa ajali hiyo huku hospitali nyingi zikikumbwa na wakati mgumu kutoa huduma bora kutokana na uhaba wa vifaa vya matibabu.
Hapo Jumamosi waathiriwa 200 walizikwa kwenye kaburi la pamoja. Bendera za nchi hiyo zinapeperushwa nusu mlingoti.
Katika hotuba kwa taifa hilo, rais wa nchi hiyo Joseph Kabila amesema wamepokonywa ndugu na dada kwa njia ya kikatili.
Lori hilo la mafuta lilianguka katika kijiji cha Sange wilaya ya Kivu ya kusini siku ya Ijumaa wiki iliyopita.
Wakati watu walipokuwa wakijaribu kuteka mafuta yaliyokuwa yakivuja, lori hilo lililipuka na kusababisha moto mkubwa ulioteketeza nyumba kadhaa na kusababisha vifo hivyo.
No comments:
Post a Comment