Monday, May 3, 2010

WATOTO WA KARNE YA 21

Njiani akiwa anatembeya Mr X hafla anakumbana na
watoto wawili wa kiume wakiwa mbele yake
wanaanza kuzungumza;

Mtoto 1: Leo nimesikiya tangazo mshahara umetoka
wa walimu, itabidi nimwambiye mama anigaiye pesa.

Mtoto 2: Mimi hata sijui mama yangu anapokeya lini
lakini naona siku zote ana pesa mkononi.

Mtoto 1: Mama yako anafanya kazi gani?
Mtoto 2: Mbunge wa Jimbo letu...

Mtoto 1: Anapokeya kiasi gani?
Mtoto 2: Wanasema mshahara ni siri

Mtoto 1: Mbona nimesoma gazeti wanapokeya
milioni 15?

Mtoto 2: Inaweza kuwa, kwasababu hata mimi
tayari keshanijengeya nyumba yangu, nikimaliza
form six tu naoa.

Mtoto 1: Mimi naona mama yangu hanenepi,
kila siku tunakula dagaa kauzu, na akirudi skuli
kajaa vumbi usoni...

Mtoto 2: Anapokeya mshahara kiasi gani?

Mtoto 1: Yule baby Powder katangazia kawarudishiya
elfu kumi zao...

Mtoto 2: Kwahiyo mshahara wote ni kiasi gani?

Mtoto 1: nafikiri itakuwa laki moja na nusu

Mtoto 2: heee mi mama yangu ananipa laki mbili
kwa ajili ya shopping kila mwisho wa mwenzi...

Mtoto 1: Mume jaaliwa... lakini naona unyonge nchi
hii hawishi maisha, watakula haohao wanasiasa tu...
Sisi siku nyengine nyumbani tunakula mlo mmoja tu
na mama keshawahi kuanguka kazini kutokana na
njaa...

Mtoto 2: Duh... basi bora mama yako na yeye awe
mwana siasa, mutanenepa nyumba nzima...

Mtoto 1: Kunenepa sisi nyumba nzima hakutosababisha
kuleta maendeleo ya nchi hii... itakuwa tunajinenepesha
sisi tu...

Mtoto 2: Sasa una hiari mfe na unyonge wenu, basi fanyeni
mgomo kama watu wa bara...

Mtoto 1: si mpaka wawe na ari hiyo...

***SALLY UKUMBINI

.

No comments:

Post a Comment