Sunday, April 11, 2010

UCHAGUZI WA KIHISTORIA WAFANYWA SUDAN

Chaguzi za rais,bunge na serikali za mitaa zinafanywa kuanzia leo tarehe 11 hadi 13 Aprili, licha ya kususiwa na vyama vingi vikuu vya upinzani.

Rais wa Sudan, Omar Hassan al-Bashir anatazamiwa kushinda, baada ya wagombea wawili wakuu kujitoa katika kinyanganyiro hicho.

Yasser Arman wa chama cha SPLM kutoka Sudan ya Kusini na Sadiq al Mahdi wa chama cha Umma kutoka kaskazini ya nchi, walitazamiwa kutoa changamoto kali katika uchaguzi wa kugombea wadhifa wa rais.

Lakini vyama vingi vya upinzani vimekataa kushiriki katika uchaguzi huo kwa madai kuwa kulikuwepo ila katika utaratibu wa maandalizi ya uchaguzi.

Baadhi ya waangalizi wana wasiwasi kuwa uchaguzi huo na hasa matokeo ya kwanza ya uchaguzi huenda yakazusha machafuko katika nchi iliyoteketezwa kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Kwenye hatari kubwa zaidi kwa machafuko kuibuka ni jimbo la Darfur ambako Umoja wa Mataifa unatathmini kuwa kama watu 300,000 wameuawa tangu mapigano yalipoanza katika jimbo hilo la magharibi hapo mwaka 2003.


.

No comments:

Post a Comment