Wednesday, April 7, 2010

KARUME AKABIDHI NYUMBA MPYA ZA MICHENZANI KWA WAHUSIKA
Rais wa Zanzibar Mh, Amani Karume jana alizindua rasmin jumba namba 10 lenye nyumba 92 na kuwakabidhi funguo watu 5 ambao walivunjiwa nyumba zao wakati ujenzi wa majumba hayo ulipoanza mnamo mwaka 1970.

Katika uzinduzi huo Rais Karume alisema kua umaliziaji wa majummba hayo mawili kati ya majumba 10 ambayo ni jumba namba 9 na 10 na yanajumuisha idadi ya nyumba 182 ndani yake uligharimu kiasi cha shilingi bilioni 2.1, na katika ugawaji wa nyumba hizo wale ambao nyumba zao zilivunjwa katika ujenzi wa majumba hayo ndio waliopewa kipaumbele na nyumba zilizosalia zimekodisha kwa watumishi wa vikosi vya usalama ambao walishiriki katika ujenzi wa majumba hayo.

No comments:

Post a Comment