Monday, March 1, 2010

WATU 51 WAFA KWA KIMBUNGA ULAYA YA MAGHARIBI

Kiasi watu 54 wamekufa kutokana na kimbunga na mvua kubwa zilizonyesha magharibi mwa Ulaya mwishoni mwa wiki. Kati ya vifo hivyo, 45 vimetokea nchini Ufaransa ambako kumeathiriwa zaidi na kimbunga hicho kilichopewa jina la Xynthia.

Katika maeneo mengi magharibi mwa Ujerumani, barabara kadhaa hazipitiki na huduma zote za usafiri wa treni zimesimamishwa kutokana na kuanguka kwa miti. Aidha, safari za ndege zimefutwa nchini humo na katika nchi nyingine. Kimbunga hicho kilipiga kwanza pwani za Uhispania na Ureno kabla ya kupiga Ufaransa na Ujerumani.

Upepo mkali uliokuwa ukisambaa kilometa 160 kwa saa umeathiri huduma za umeme kwa zaidi ya nyumba milioni moja nchini Ufaransa. Mawimbi yenye urefu wa mita nane yalipiga maeneo ya pwani na kusababisha mafuriko katika maeneo ya nyanda za chini.

No comments:

Post a Comment