Saturday, March 6, 2010

TANZANIA NA UJERUMANI YAZINDUA TAASISI YA MELI YA MV LIEMBA

Tanzania na Ujerumani zimezindua taasisi ya marafiki wa kweli ya meli ya MV Liemba ambayo inakusudia kutumika kwa kulinda na kuendeleza mahusiano mema ambayo yamekua yakidumu kwa nchi zote mbili.
Uzinduzi wa taasisi hio uliofanywa katika meli ya MV Liemba iliyoko katika ziwa Tanganyika umeshuhudiwa na balozi wa Ujerumani nchini Tanzania pamoja na maafisa wengine kutoka Serikalini
Pamoja na azma yake kubwa ni kutaka kudumisha mahusiano mema yaliyopo kwa nchi hizo mbili, taasisi hio pia inakusudia kujikita katika maeneo ya utoaji wa elimu inayohusu mazingira, utawala bora pamoja na teknolojia ya uvuvi kwa wananchi wa Tanzania hususan wale wa maziwa makuu.
Meli hio ya MV Liemba ambayo imekua ikifanya shughuli zake katika maeneo ya maziwa makuu kwa muda wa miaka mia moja, imekua ndio shabaha ya kuanzishwa kwa taasisi hii ya marafiki wa kweli.
Katika miaka ya hivi karibuni, Ujerumani imekua ikiongeza misaada yake kwa Tanzania na kufadhiliwa miradi mbali mbali ya kimaendeleo, kwa mfano mwishoni mwa mwaka jana Ujerumani ilitangaza kufadhili miradi myengine ya afya, maji elimu pamoja na eneo la utawala bora ukiweka kando miradi myengine ambayo imekua ikifadhiliwa mara kwa mara.
Akizungumza katika uzinduzi huo, balozi wa Ujerumani nchini Tanzania ambae alifuatana na maafisa mbali mbali kutoka Ujerumani aliahidi kuiongezea vipuri zaidi meli hio ili iweze kudu zaidi kwa kipindi chengine cha miaka mia moja.
Taasisi hio inatizamwa kama kituo cha utoaji mafunzo kwa wananchi wa maeneo ya maziwa makuu na inatajwa kuja katika kipindi muafaka wakati nchi za eneo la Afrika Mashariki zikijiandaa kupasisha soko la pamoja na kuruhusu maingiliano huru ya watu wa eneo hilo.

No comments:

Post a Comment