Saturday, March 20, 2010

USWISS KUCHUNGUZA KIFO CHA MKIMBIZI WA KINIGERIA


Uswiss imeizua ndege maalum ya kuwarudisha wakimbizi makwao kufuatia kifo cha Mnigeria baada ya kugoma kula.

Polisi wa Uswiss wamesema kua walimfunga pingu mtu huyo mwenye umri wa miaka 29 ambae walikua wakimrudisha kwa nguvu yeye pamoja na Wanigeria wengine 15 ambao maombi yao ya ukimbizi yalikataliwa.

Mamlaka inayohusika imeanzisha upelelezi kuhusiana na tukio hilo, nao polisi walisema walilazimika kumfunga pingu mtu huyo baada ya kukataa kurudishwa kwao.

Wakimbizi wawili wa Kinigeria ambao walishuhudia tukio hilo walisema, polisii hawawafanyii ubinaadamu.

"Wanatufanya kama wanyama" alisema jamaa mmoja aliyejuilikana kwa jina la Emmanuel.

"Wanatufunga miguuni, magotini, mikononi, kiunoni, na mwilini na pia wanatuvalisha makofia kama wanayovaa wapiganaji boxing, ilikua si rahisi hata kujitikisha" alizidi kulalamika Emmanuel.

Hata hivyo, imeelzwa kua mtu huyo aliyekufa alikua akijishughulisha na madawa ya kulenya, ambae aligoma kula kwa siku kadhaa, na kifo kama hichi ni cha tatu kuwahi kutokea nchini Uswiss tangu mwaka 1999.

Imeripotiwa kua mwaka jana peke yake ndege zipatazo 43 ziliwarudisha makwao watu takriban 360, wengi wao wakiwa ni kutoka Balkan na Afrika..

No comments:

Post a Comment