Tuesday, February 9, 2010

TIMU YA TAIFA YA BENIN YAVUNJWA


Shirikisho la mchezo wa soka nchini Benin, limevunja kikosi kizima cha timu ya taifa ya nchi hiyo kufuatia matokeo mabaya katika michuano ya kuwania kombe la mataifa bingwa barani Afrika.

Kocha wa timu hiyo raia wa Ufaransa Michel Dussuyer na maafisa wote wa kiufundi pia wamefutwa kazi. Kwa mujibu maafisa wakuu wa shirikisho hilo, kikosi hicho kimevunjwa kutokana na utovu wa nidhamu na kutowajibika kama wazalendo.

Timu hiyo inayojulikana kama The Squirrels, iliyaaga mashindano hayo nchini Angola, baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu katika kundi lake na alama moja pekee.

No comments:

Post a Comment