Tuesday, February 2, 2010

MTAFARUKU BENKI YA WATU WA ZANZIBAR TAWI LA PEMBA

Baadhi ya wateja wa Benki ya Watu wa Zanzibar Tawi la Chake Chake Pemba wakiwa katika taharuki ya kukimbizana baada ya “Fire Extinguisher” kupasuka ndani ya Benki hiyo na kudhania kuna mlipuko ama moto.

Baadhi ya wateja walikanyagana na kupata majeraha madogo madogo. Hata hivyo hali ilirejea na huduma zikaendelea kama.

Kawaida. Benki ya watu wa Zanzibar Chake imekuwa na wateja wingi sana hata wengine kushindwa kuwahudumia kwa wakati na ipasavyo kutokana na nafasi ya benki hiyo kuwa ni ndogo sana

” Kwa hakika tunahitaji jengo la benki lifanyiwe ukarabati kwa vile halitoshelezi isitoshe huduma ya ATM hakuna, Tupigieni kelele ndugu waandishi jambo hili lisikike kwa serikali hali ni mbaya sana” Alizungumza mmoja wa wateja wa Benki hiyo.

Mazingira ya Benki hiyo sio mazuri kwa majengo na kama inatokezea hatari kama ya moto inaweza kuleta hasara kubwa kwa binaadamu na mali zao ipo haja serikali kulitazama upya jengo hili na sio kulibadilisha rangi kila mwaka.

No comments:

Post a Comment