Thursday, February 11, 2010

KIKAO MAALUM CHA UMOJA WA ULAYA KUJADILI MZOZO WA UGIRIKI

Umoja wa Ulaya unazingatia kuisaidia Ugiriki inayokabiliwa na tatizo kubwa la madeni. Hayo alitamka Kansela wa Austria Werner Faymann siku moja kabla ya kufanywa mkutano maalum wa viongozi wa umoja huo leo hii mjini Brussels.

Hapo awali,Waziri Mkuu wa Uhispania José Luis Rodríguez Zapatero alie pia Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya, alihakikisha kuwa Ugiriki itasaidiwa na umoja huo.

Wakati huo huo nchini Ugiriki wafanyakazi kutoka sekta za kuhudumia umma,wameandamana kwa maelfu kupinga mipango ya serikali ya kupunguza matumizi yake. Kuambatana na mipango hiyo, wafanyakazi serikalini hawatopata nyongeza ya mishahara na hakuna wafanyakazi wapya watakaoajiriwa katika sekta za kuhudumia umma.

Kwa kuchukua hatua hizo,serikali ya Ugiriki inajaribu kupunguza nakisi iliyovunja rekodi ikiwa ni asilimia 13 ya bajeti yake. Lengo ni kuwa ifikapo mwaka 2014 nakisi hiyo itafikia asilimia 3 ya bajeti, ambacho ni kiwango kinachoruhusiwa na Umoja wa Ulaya.

No comments:

Post a Comment