Wednesday, February 3, 2010

AL-BASHIR HUENDA AKASHTAKIWA

Majaji rufaa wameiambia mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC kuangalia upya iwapo Rais wa Sudan, Omar al-Bashir ashitakiwe kwa mauaji ya kimbari mjini Darfur.

Majaji walibatilisha uamuzi wa awali kwa madai kuwa waendesha mashitaka hawakutoa ushahidi wa kutosha.

Mwendesha mashitaka mkuu ameiambia BBC uamuzi wa Bw Bashir wa kuyafukuza mashirika ya kutoa misaada mwaka jana baada ya ICC kutoa kibali cha kukamatwa kwake ni ushahidi mpya wa nia yake ya mauaji hayo.

Sudan imesema uamuzi uliotolewa na jopo hilo ni sababu za kisiasa.

Rais al-Bashir amekataa kuitambua mahakama ya kimataifa ya ICC.

Umoja wa Mataifa unaamini takriban watu laki tatu wamefariki dunia kutokana na mapigano mjini Darfur.

No comments:

Post a Comment