Monday, January 4, 2010

JACOB ZUMA KUONGEZA MKE WA TANO

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma anafanya ndoa yake ya tano baadaye leo.
Harusi ya leo itafanyika kuambatana na mila na utamaduni wa jamii ya Zulu ambapo Thobeka Stacey Mabhija atakuwa mke wa tatu wa Zuma.

Wake wengine wawili wa Zuma Sizakele Khumalo-Zuma na Nompumelelo Ntuli-Zuma sharti washiriki sherehe ya leo ili kumkubali mke mwenza wao.

Rais Zuma pia amesha mposa mwanamke mwingine na tayari amelipa mahari.

Waandishi habari wamesema imani ya Zuma kuwa na wake wengi imeigawanya jamii Afrika Kusini.

Baadhi wanamuunga mkono huku vijana wengi wakisema desturi hiyo imepitwa na wakati.

Mmoja wa wake wa Zuma Kate Mantsho-Zuma alifariki dunia na rais huyo alitengana na waziri wa mambo ya ndani wa Nkosazana Dlamini Zuma.

No comments:

Post a Comment