Friday, January 1, 2010

ABDULMUTALLAB ALIANZA SAFARI YAKE GHANA NA WALA SI NIGERIA

Serikali ya Nigeria imesema raia wa nchi hiyo aliyejaribu kulipua ndege ya Marekani mnamo tarehe 25 mwezi desemba, alikuwa ameanzia safari yake nchini Ghana na si Nigeria kama inavyodhaniwa.

Waziri wa habari Dora Akunyili ameiambia BBC kuwa mtu huyo Umar Farouk Abdulmutallab alikuwa amesafiri kutoka Accra Ghana na kuwasili nchini Nigeria ambapo alikaa kwa muda wa nusu pekee kabla ya kupanda tena ndege kuelekea Amsterdam.

Maafisa wa Nigeria na Udachi wamesisitiza raia huyo alipitia ukaguzi wote wa usalama kwenye viwanja vya ndege.

No comments:

Post a Comment