Wednesday, December 16, 2009

ZANZIBAR IKO HATARINI KUTOKANA NA ONGEZEKO LA KINA CHA MAJI BAHARINI

Imeelezwa kua wakaazi wa sehemu za pwani nchini Tanznaia wamekua wakaiishi kwa wasi wasi kufuatia hali ya kuongezeka kwa kina cha maji ya bahari.

Bibi Rose Mpuya ambae ni afisa mwandamizi msimamizi wa mzingira ya pwani Tanzania (NEMKI) katika mazungumzo aliyofanya na BBC alisema hali hio inasababishwa na kuyayuka kwa barafu ilioko katika baadhi ya nchi duniani (polar countries)na kupelekea kuongezeka kwa kina cha bahari.

Afisa huyo alizitaja sehemu ambazo ziko hatarini kukumbwa na janga hilo ni kunuchi beach, kisiwa cha maziwe kilichopo maeneo ya kaskazini ya pangani Tanga, ambapo alikitaja kisiwa hicho kua kimeshafunikwa kabisa na maji.
Aliongeza kua Zanzibar na maeneo yake yote pia yamo hatarini kukumbwa na janga hili, pia sehemu katikan sehemu za bagamoyo baadhi visima ambavyo vilikua vikitumika kwa kuchotwa maji ya kunywa visima hivyo kwa sasa vinatoa maji ya chumvi

Bibi Rose alielezea mambo ambayo yanaweza kuchukuliwa kama ni tahadhari ili kujikinga na athari hizo,ikiwemo kuepuka ukataji wa mikoko, kulinda matumbawe, kuacha uvuvi wa kutumiabaruti, kutokata nyasi bahariabazo zinakua kwenye fukwe za bahari, mambo hayo yote kama yatalindwa basi yatazuia ukali wa mawimbi ya bahari kuharibu fukwe na kusababisha maji kupanda juu.

No comments:

Post a Comment