Saturday, December 5, 2009

WACONGO WATUPWA JELA NA WENGINE WAPEWA MASAA KUONDOKA BONGO


Watu wanaosadikiwa kua ni raia wa Congo wamekamatwa huko Sumbawanga na kufikishwa mahakamani ambapo walishtakiwa kwa kosa la kuishi nchini kinyume cha sheria,hakimu mkaazi wa mahakama ya Sumbawanga aliwataka watu hao kulipa fidia ya sh. 30,000/ kila mmoja ambapo wawili tu kati ya watu 10 ndio waliokua na uwezo wa kulipa fidia hio hivo kusababisha kupewa masaa 72 kuondoka nchini na wanane waliobaki walishindwa kulipa pesa hizo na kupelekea kutupwa jela kwa muda wa mwaka mmoja kila mmoja.

No comments:

Post a Comment