Saturday, December 12, 2009

TIGER WOODS ATAPUMZIKA NA GOLF ILI KUOKOA NDOA YAKE

Tiger Woods alisema jana Ijumaa kuwa atachukua mapumziko katika mchezo wa golf ili kuokoa ndoa yake.
Woods aisema kwa sasa anataka kuangalia zaidi katika kuijenga familia yake kusudi kuwa mume bora,na baba bora,ingawa hakusema kua mapumziko hayo yatamaliza lini.

Uamuzi huo Woods ameutangaza ikiwa ni wiki mbili tangu alipopata ajali ya gari huko Florida, lakini vyombo vingi vya habari vilielezea juu ya utata wa ajali hio, na kusema kua hii haikua ni ajali bali ilikua ni ugomvi kati yake na mkewe.

Mwanamke mmoja alijitokeza hadharani na kuanika kua alikua na uhusiano wa kimapenzi na Tiger Woods uhusiano ambao ulidumu kwa miezi 13 na waliachana siku mbili kabla ya ajali, pia mwanamke huyo aliitangaza voice Woods iliokuwa kwenye simu yake.

Woods kupiti katika website yake alisema kwamba anajua kua amechukiza nyoyo za watu wengi hususan mkewe na watoto wake "nataka kuwaambia tena watu wote kuwa nawataka radhi kwa mambo yaliyotokea na nawaomba msamaha , najua kama siwezi kurekebisha athari nilizozifanya, lakini nitajitahidi kujaribu.

No comments:

Post a Comment