Sunday, December 13, 2009

KILI STARS, ZANZIBAR HEROES USO KWA USO LEO HII KUWANIA NAFASI YA TATU

Mashindano ya Chalenji yanatarajiwa kufikia ukingoni leo hii huko Nchini Kenya.leo hii kutakua na mechi ya fainali itakayozishirikisha timu za Uganda na Rwanda ambazo zitachezwa katika uwanja wa Nyayo mjini Nairobi.

Kocha wa timu inayopewa nafasi kubwa ya kutwaa kombe hilo Uganda, Robert Williamson amesema kuwa "Rwanda sio timu nyepesi na wamekua wakionesha upinzani mkubwa kila wanapocheza dhidi ya Uganda lakini tutawafunga tu".

Mshindi wa mschi hio atanyakua kitita cha dola za kimarekani 30,000.

Kabla ya mechi hio ya fainali kutakua na mechi ya kutafuta nafasi ya mshindi wa tatu kati ya Kilimanjaro Stars watakapokipiga na ndugu zao Zanzibar Heroes, kabla mechi hio ya mshindi wa tatu ilipangwa kufanyika jana lakini kutokana na sababu zisizoweza kuepukika mechi hio ilibidi isogezwe leo.

Kocha mkuu wa Zanzibar Heroes amesema hawatarajii kupoteza mechi yao ya leo baada ya kushindwa kuingia fainali baada ya kutolewa na Uganda.

Na kwa upande wake Kocha mkuu wa Kili Stars Maximo amesema baada ya kushindwa kuingia fainali atahakikisha kikosi chake kinatwaa nafasi ya tatu kama ilivyokua kwa mashindano ya chalenji yaliyopita.

Mshindi wa mechi hio atapata kitita cha dola za kimarekani 10,000

No comments:

Post a Comment