Thursday, November 5, 2009

MWANASHERIA MKUU NCHINI KENYA AKIRI MARUFUKU


Mkuu wa Sheria nchini Kenya Amos Wako Amethibitisha kuwa yeye ndiye afisa wa ngazi ya juu aliyepigwa marufuku kuzuru Marekani.
Amos Wako amesema kuwa amepokea barua kutoka kwa ubalozi wa marekani na ni miongoni mwa maafisa wengine kumi na watano wa ngazi ya juu serikalini walioandikiwa barua ya kufuta hati zao za usafiri kuzuru nchi hiyo.

Jumatatu wiki iliyopita, naibu wa waziri wa kigeni wa Marekani wa masuala ya Afrika Johnie Carson alitangaza kuwa Marekani imewapiga marufuku maafisa kumi na watano wa ngazi za juu katika serikali ya Kenya kwa kuwa kizuizi kikubwa katika mabadiliko ya sheria nchini humo.

Akihutubia kwenye televisheni ya Kitaifa muda mfupi uliopita, Wako alikanusha madai kuwa amehusika kuvuruga marekebisho nchini , akisema kuwa amekuwa mstari wa mbele kupigania marekebisho hayo.

No comments:

Post a Comment