Tuesday, November 24, 2009

ATUPWA JELA MAISHA BAADA YA KUMSABABISHIA KIFO BIBI KIZEE KWA WOGA

CHARLOTTE, N.C. Kijana mmoja nchini Marekani atamalizia maisha yake yaliobaki gerezani baada ya kugundulika kua mkosa kwa lile lililoelezwa kua ni kumtia woga bibi mmoja mwenye umri wa miaka 75 anaeishi North Carolina na kumsababishia kifo.

Vyombo vya habari vilieleza kua mahakama haikumtia haitiani kijana huyo mwenye umri wa miaka 21 Larry Whitfield kwa kosa la kumuua bibi Marry Parnells mwaka jana.Lakini waligundua kua ni mkosa kwa kumsababishia kifo bibi huyo baada ya kumteka na hii kupelekea moja kwa moja kufungwa kifungo cha maisha.

Waendesha mashtaka walieleza kua kijana huyo alikua akitafuta sehemu ya kujificha baada ya jaribio lake la kuteka benki huko Gastonia Septemba 2008 kutofanikiwa na ndipo alipovunja na kuingia ndani ya nyumba ya bibi Parnells.Wahusika walisema kua whitfield hakumgusa bibi huyo lakini alipata mshtuko wa moyo na kufa, na wala whitfield hakuomba msaada.

No comments:

Post a Comment