Friday, October 16, 2009

MTOTO WA MAAJABU AWASHANGAZA WANASAYANSI DUNIANI

Wanasayansi na madaktari nchini Urusi wamestaajabishwa na mtoto mwenye umri wa miezi tisa ambaye mwili wake umekuwa ukitoa maandishi katika lugha ya kiarabu yakinukuu vipande vya maneno katika Quran.

Wanasayansi nchini Urusi wameshindwa kujua ni nini kinapelekea mtoto anayeitwa Ali mwenye umri wa miezi tisa, mwili wake uwe unatoa maandishi tofauti tofauti ya kiarabu mara kwa mara.

Televisheni ya Vesti news ya nchini Urusi ilionyesha video ya mtoto huyo na picha ambazo wazazi wake wamekuwa wakimpiga kila maandishi mapya yanapotokea.

Kwa mujibu wa wazazi wake wanaoishi kwenye mji wa Dagestan, siku mbili baada ya Ali kuzaliwa herufi za kiarabu zilianza kujitokeza kwenye miguu yake na baada ya siku kadhaa zilianza kutengeneza maneno kamili.

Maandishi tofauti tofauti ya kiarabu hutokea zaidi kila siku ya jumatatu na ijumaa kwenye sehemu mbalimbali za mwili wake.

Awali kulikuwa na alama za maandishi yaliyofifia kwenye kidevu chake na baadae maandishi hayo yalijitokeza wazi yakisomeka "Allah", alisema mama wa mtoto huyo Madina Yakubova.

Miongoni mwa maneno ambayo yamesomeka wazi ni yale yanayosema "Waonyesheni watu dalili za kuwepo kwangu".Kwa kushangaza zaidi kwenye mguu mmoja wa Ali yalijitokeza maandishi yaliyosemeka "Allah (Mungu) ndiye muumba wa vitu vyote".

Ali alipozaliwa aligundulika kuwa na matatizo makubwa ya moyo wake na ugonjwa unaoathiri zaidi ubongo unaoitwa "cerebral paralysis" lakini alipopimwa tena baada ya maandishi hayo ya kiarabu yalipoanza kujitokeza aligundulika hana matatizo yoyote na afya njema.

Madaktari nchini Urusi hawajui ni nini kinaendelea kwenye mwili wa mtoto huyo na wamekiri hawajawahi kwamba hawana jibu la kutoa kwa taaluma za kisayansi.

3 comments:

  1. MTOTO HUYU MPAKASASA ANA UMRI WA MIAKA MINGAPI?
    BY
    "miki.m.mustafa@live.com"

    ReplyDelete
  2. hilitukio linamda gani tangu litokee?

    ReplyDelete
  3. Huyu mtoto kwa sasa atakua na mwaka mmoja na miezi miwili kama utaangalia wakati hizi habari zilipotoka.

    ReplyDelete