Friday, October 9, 2009


Mmiliki wa klabau ya Soka ya Chelsea ya Uengereza Roman Abramovic, ameahidi kuipa msaada timu ya Soka ya Miembeni ya Zanzibar katika mashindano mbali mbali inayotarajiwa kushiriki.
Ahadi nono ya Bosi huyo ameitoa mbele ya viongozi wa timu hiyo wakati akiwa ziarani nchini humu hivi karibuni,akisimulia kuhusu hadi hiyo huko Rahaleo Mjini Unguja,
Meneja wa klabu hiyo Abubakar Wakili , alisema kuwa Bosi huyo tayari ameshafanya mazungumza ya awali na uongozi wa timu hiyo juu ya dhamira yake ya kukisaidia kikosi cha Miembeni.
“Tayari mazunguzo ya awali baina ya uongozi wa Miembenia na Bosi huyo wa Chelsea tayari yameshafanyika ya kutaka kukisaidia kikosi chetu” alisema
Wakili alifahamisha kuwa mazungumzo hayo ya awali kwa uongozi wa Miembeni na Bosi Abramovic, yalimefanyika huko Mkoani Arusha Tanzania Bara, lakini bosi huyo hakuweza kumaanisha ni msaada gain atakaoutoa kwa klabu hiyo.
Mazungumzo ambayo yalianza kuzaa matunda mazuri ya mafanikio kwa uongozi juu ya kuwa na uhakika wa kupatiwa ufadhili pamoja na ushirikiano baina ya timu ya Miembenia na Chelsea.
“Tulipata matumaini makubwa katika mazungumzo yetu na Bosi huyo ambapo alieka bayana kuwa atatusaidia kwa shida na raha”
Hata hivyo Kaimu katibu huyo alisema kuwa hivi sasa kilichobakia ni umalizaji wa mazungumzo yao na Bosi huyo, ambapo wanataraji hivi karibuni watakamilisha.
“Kilichobakia sasa tunamsubiri kwa hamu kubwa Bosi Abramovic kuja nchini humu kwa ajili ya mazungumzo ya mwisho na baadaye kufuata hiyo ahadi yake aliyoitoa kwetu” alisema Wakili.
Hatua ya Miembeni ya kusaka mfadhili kwa klabu yao imekujaa baada ya aliyekuwa mfadhili wa mwanzo Amani Makungu kuiwachia mkono timu hiyo na hivi sasa klabu hiyo inaendeshwa na Wazee wa dhama zilizoipita wa timu hiyo.

No comments:

Post a Comment