Saturday, October 31, 2009
MATOKEO YA LIGI KUU UINGEREZA
Soma Zaidi ...
Friday, October 30, 2009
AMUUWAA MKEWE KWA KUMPIGA MAPANGA USONI
Wednesday, October 28, 2009
MAISHA YA SKULI ZAMANI
Na Abdulla Al-Harthy
Kuna kitu kimoja au viwili mimi siwezi kusahau juu ya maisha yaliokuwepo Visiwani wakati ule wa neema, utulivu na sharaf zilizokuwepo.
Kimoja ni wakati wa masomo na walimu wetu tuliokuwa nao wa kila aina na kila mchaganyiko, pamoja na jitihada zao za kutusomesha.
Ninachokikumbuka mimi ni juu ya walimu wetu mbali mbali, akiwemo Maalim Ibrahim Kassim ambaye alikuwa mwalimu wa hesabu huko Mnazi Mmoja. Alikuwa akitaka kukupiga huwa anatafuna ulimi na ukikinga anakwambia upo tyari kupigana? Wakati huo huwa huku anakunja koti lake na kukutandika magumi.
Maalim Aboud Jumbe alikuwa katika walimu waliosifika kwa Kiingereza huko Mnazi Mmoja Secondary School. Alikuwa na baiskeli yake aina ya Humber. Akitoka kazini na kurudi nyumbani, wakati mwengine alikuwa akinipakia. Hayo yalikuwa mapenzi ya kweli kati ya walimu na wanafunzi wa zama zetu.
Kina Maalim Hija Saleh na Malim Uledi Jabu walikuwa ni katika walimu mahodari kabisa kwa hesabu katika skuli za msingi (Primary School).
Maalim Uledi Jabu alikuwa sifa zake ni kupenda kuwasaidia wanafunzi wake. Yeye alikuwa akisomesha Historia na Kiswahili.
Alikuwa anavaa koti na kanzu na kunako koti lake, kwa kawaida , kulikuwa hakukosi kichwa cha samaki au cha kuku.
Tulipohamia Shimoni School (hivi sasa kuna Uwanja wa Mao Dze Dung) kulikuwa na kina Maalim Hilal, Ahmed Zahran, Seyyid Ahmed Mansab, Hassan Mshangama na Mohammed Aley.
Tulikuwa tumegawiwa siku za uhamisho magurupu mawili. Kundi moja likenda Kupaz (Coopers – sasa Uwanja wa Maisara) na sisi tukaenda Mashimoni. Mimi nilikwenda na wenzangu kunako mabanda ya makuti – juu kwenye paa na ukutani pia.
Pamoja na kuwa na mabanda mengine ya makuti juu na ukuta wa mawe chini, Sh. Abdulla Saleh Farsy alikuwa akitusomesha Kiarabu na Dini.
Saa nne tulikuwa tukimfukuzia Said Njugu kununua njugu, na kina mama walikuwa wakiuza mbaazi, na mbatata za urojo. Wakati huo kiwanja cha mpira kilichopo Shimoni ndio kilikuwa kinafukiwa, kwani kwanza kulikuwa na jaa la taka la mji.
Gari iliokuwa ikija skuli ni moja tu ambayo, ilikuwa tunaiita gari la mabati kutoka Nyumba ya Moto (nyumba ambayo wakiishi watoto waliolelewa na Mfalme). Kulikuwa hakuna hata apandae baiskeli, na hiyogari ilikuwa ikipandisha wanafunzi hata tulikuwa tukiionea huruma.
Mimi sijawahi kuipanda, lakini ilichukua mtoto yeyote yule wa Kisiwani aliokuwa akisoma skulini hapo.
Kulikuwa wakati huo hakuna Mzanzibari anayesoma skuli za nje wala za mapesa. Skuli za nje zilikuwa ni za Comorian na ya misheni iliopo nje ya Kupaz.
Sijui huo ubepari unaozungumzwa leo ulionekana vipi wakati kulikuwa hakuna anayeweza kumiliki hata kumpeleka mtoto wake skuli kwa gari, wakati ambapo kulikuwa hakuna wamiliki wa magari na ikiwa walikuwepo walikuwa hawajai mkononi.
Inasikitisha kuona kuwa Uzanzibari ule sasa haupo na umemezwa na hali ya sasa kutokana na mambo yalivyobadilika.
Mimi nashukuru kuwa ni miongoni mwa tuliojifaidia kuona yaliopita ambayo ni ya kutafakhari nayo, pia tunaomba Mungu ayarudishe kama yalivyokuwa.
Tulikuwa tunapewa mabuku, wino, nibu, dawa za homa tuliokuwa tukila kila wiki. Daktari wa meno, Dk. Soud alikuwa akitupitia kila skuli mwaka mara mbili na pia wakati huo kulikuwa hakuna sare za skuli.
Sare zimeanza Skuli ya Darajani ambako mimi sijasoma. Aghlabu wanafunzi tulikuwa
tukivaa kanzu au suruali ndefu au fupi (kipande).
Lakini kulikuwa na feshini ya kuvaa kaki na shati jeupe au fulana ya navy blue kutoka dukani kwa Maalim Abdulrauf lililokuwepo hapo Kinu cha Taa, Malindi.
Ukivaa hivyo ndio unaonekana umesha-staff kimji wakati ule.
Kulikuwa hakuna makuu. Pamoja na viatu vya mpira vyeupe miguuni basi mambo hapo yamejishia. Ndugu zetu wa kike wote walikuwa Skuli ya Rahaleo na ya Forodhani.
Wanafunzi wote wa kike walikuwa kunako skuli hizo mbili za mjini na walikuwa wanatoka watokako kwa miguu hadi skuli. Awe atavyokuwa lazima autwange kwa miguu (Ubepari huo!).
Mchana utaona wasichana mikoba yao ya ukili begani . Wakubwa na mabuibui yao na wadogo na magauni yao au na ushungi wao (mmeziona skuli ziliopo leo mjini?).
Kabla ya Skuli ya Rahaleo kujengwa mwisho wa miaka ya 40 wanafunzi wa kike walikuwa wakisoma Forodhani, nyuma ya Msikiti wa Ijumaa wa Forodhani, uliopo nyuma ya Palace (Kasri ya Mfalme).
Walimu, pamoja na wasomi wote wa kike wametokea hapo au kuanzia hapo.
Mungu aibariki Zanzibar na awaoneshe watoto wetu yale tuliyoyaona sisi wazee wao. Soma Zaidi ...
Monday, October 26, 2009
ELIZABETH ANUSURIKA KUTOKA KATIKA JUMBA LA BIG BROTHER KWA MARA NYENGINE TENA
Kwa mara nyengine tena mtanzania Elizabeth na mshirika wake mnigeria Kevin wamebakia kwenye jumba la Big Brother huku Kristal na Mwenziwe Quinn wakiaga mashindano hayo.hii ni mara ya pili kwa Elizabeth kunusurika kutolewa kwenye jumba hilo.
Soma Zaidi ...WACHAPWA BAKORA 25 KWA KUANGALIA VIDIO ZA NGONO KWENYE SIMU
Maafisa wa ulinzi wa kundi la Al shabab waliwafumania vijana hao wakiangalia video za ngono kwa kutumia simu zao siku ya ijumaa na walicharazwa bakora hizo siku ya jumamosi katika mji wa kusini mwa Somalia wa Kismayo unaotawaliwa na Al shabab.
"Vijana hawa wawili walikamatwa wakiangalia video za ngono kwa kutumia simu zao na baada ya kukiri makosa yao wameadhibiwa kwa mujibu wa sharia za kiislamu", alisema Sheikh Omar Mohamed, afisa wa mambo ya dini wa Al shabab alipokuwa akiongea na shirika la habari la AFP.
"Kila mmoja wao alichapwa bakora 25 na watatumikia siku 15 jela kwa vitendo vyao viovu walivyovifanya", aliongeza Sheikh Mohamed.
Wakazi wa eneo hilo walithibitisha kucharazwa bakora kwa vijana hao.Kundi la Al shabab linatumia sharia za kiislamu katika maeneo wanayoyatawala. Wezi hukatwa mikono au miguu kulingana na kosa lenyewe na wazinzi hucharazwa bakora. Soma Zaidi ...
MAMBO KANGAJA HUENDA YAKAJA
Nyaraka za wasafiri wa kale walioitembelea Zanzibar zinatueleza kuwa Wasafiri kutoka Misri na Ugiriki walifika Zanzibar mnamo mwanzoni mwa Karne ya Tano baada ya kuzaliwa Nabii Issa. Wasafiri wengine kama Ibn Batuta na Ibn Mas-ud pia waliitembelea Zanzibar na kuandika khabari zake kama walivyoiona katika dahari hizo.
Wengine wengi walifika katika Visiwa hivi wakitumia Pepo za Musim (Monsoon Winds) kutoka sehemu za Ghuba ya Uajemi na Ghuba ya Waarabu na nchi za Kusini ya Arabuni, Bara Hindi, Mashariki ya Mbali khasa Uchina na Visiwa vya Java na Sumatra (ambavyo sasa ni Indonesia ) na wote hao walivutiwa na Zanzibar .
Katika yaliyowavutia ni kuiona Zanzibar kuwa ni nchi yenye ardhi nzuri yenye miti mingi na maji safi ya kunywa ya kutosha pamoja na bandari nzuri na salama ya kuegesha vyombo vyao na kupata mahitajio yao mengine.
Baadaye wengi katika wasafiri hawa waliovutiwa sana na mandhari nzuri na bashasha ya watu wake walifanya maskani yao hapa Zanzibar . Na hapo ndipo yalipoanza maingiliano makubwa kati ya wageni na wenyeji.
Hayo tuliyoyaeleza hapo juu ni historia. Wanaoishi sasa katika Karne hii hawayajui. Yamesalia katika kumbukumbu za taarikh ya kale. Lakini sisi wazee tumediriki kuyaona baadhi ya mambo haya ambayo wengi katika vijana wa leo hawayajui.
Kwa hivyo, si vibaya kuwazungumzia vijana ijapokuwa kwa uchache tu. Kwa hakika, sifa za Zanzibar ni zile zile walizotuhadithia wasafiri wa kale. Na katika kusifu wamesema waliyosema kwamba: Visiwa vya Zanzibar hewa yake ni safi , ardhi yake ina rutba nyingi yenye miti mingi ya namna kwa namna na yenye maji safi ya kunywa. Wenyeji wake ni watu wazuri, wachangamfu, wenye hishma na wanaopenda wageni.
Hizo ni sifa iliyopewa Zanzibar na watu wake. Tuliyoyaona sisi ni namna ya watu wa Zanzibar wa mjini na mashamba walivyokuwa wakipendana, wakihishimiana na wakisaidiana hata ikawa la mmoja wao ni la wote, likiwa la msiba au la furaha.
Kutokana na hayo, neema ikazagaa katika kila pembe ya Visiwa hivi. Hapakuwa na chuki, bughudha wala utengano wa aina yoyote baina yao kama ilivyo sasa, mambo ambayo sasa yamezipeperusha neema zote tulizozishuhudia wakati huo.
Katika zama zetu, watoto nao pia walikuwa wa watu wote, wakitunzwa vilivyo na wazee wote wa mtaa bila ya kuwabagua. Watoto wote wa umri mdogo walihudhuria katika vyuo vya Qur-ani mitaani pamoja na baadaye kwenda skuli pamoja.
Haya yalisaidia sana katika kuwafanya watoto hao wajuane kama walivyo wazee wao na kuwahishimu wazee.
Watoto wadogo walihifadhiwa vizuri ili wakulie katika malezi mazuri. Watoto wote iliwabidi warejee majumbani likichwa jua. Baada ya hapo, watoto wakubwa ama wakenda miskitini kujifunza dini au wakibaki majumbani mwao kudurusu masomo yao . Ilikuwa hapana ruhusa watoto kuzurura ovyo majiani mpaka saa za usiku kama ilivyo hivi leo na matokeo yake tunawapoteza vijana wetu wanaotumbukia katika kila aina ya balaa lisilokuwa na tija wala kheri kwao.
Wakati huo, watu wote wakiweza kulala majumbani mwao kwa usalama pasina khofu ya kuingiliwa na majambazi wa kupora mali yao , kuua au hata kuwanajisi watoto vigori kama ilivyo hivi leo. Huo ulikuwa wakati ambao wafanya biashara na wenye maduka walikuwa na usalama wa mali zao na hawakuwa wakilazimika kujifungia ndani kwa milango ya chuma kama wanyama waliomo katika “zoo”.
Uko wakati ule? Wakati akinamama walivyoweza kujifaragua na mapambo yao ya dhahabu kwenda katika mashughuli ya arusi bila ya wasiwasi wa kushambuliwa na wahuni wa kuwavunjia hishima zao na kuwapora mapambo yao .
Wakati wenye mashamba, wakulima na wafugaji, walipokuwa na uhakika wa usalama wa mazao yao na wanyama wao.
Wakati majenzi ya nyumba yalipokuwa yakifuata rasim na ramani zilizowekwa na sheria. Magari makubwa na madogo yakifuata sheria za barabarani ili kuepusha ajali za kila siku na wapitao njia kusalimikana maisha yao .
Wakati maji ya mifereji yakihifadhiwa ili kuepusha maradhi mabaya yasiwapate watu.
Wakati lugha yetu ya Kiswahili iliyojaa ufasaha wa tungo na tenzi za wataalamu na mabingwa wa fani ya lugha yetu ilipohifadhiwa na kuhifadhika bila ya kuingiliwa na maneno na misemo isiyo na asli yoyote ya lugha ya Kiswahili.
Basi haya tuliyoyaeleza hapa na mengi mengineyo ndiyo yanayotufanya wazee tuliyoijua Zanzibar ya zama zile kulalamika na kusononeka. Tumebaki kujiuliza ziko wapi kheri, tijara na neema tulizoziona? Iko wapi salama na amani na adabu zetu za asli pamoja na ustaarabu wa Waswahili? Yote yameondoka. Zanzibar imebaki inaning’inia.
Kutokana na hayo basi, ni wajibu wa kila mwananchi mwenye ghera na uchungu wa Visiwa hivi “wanasiasa, wasomi, walimu, masheikh na wazee mitaani “kushirikiana pamoja na kusimama kidete kuyahuisha yale yote yaliyonasibishwa na mema na mazuri ya nchi hii. Ni wajibu wetu kuwarithisha watoto wetu nchi yao ikiwa na utukufu wake ule ule wa asli uliyoifanya Zanzibar isifike na kutajika katika kila pembe ya Ulimwengu huu.
Na haya si ndoto za Alinacha! Yanawezekana kabisa ikiwa tutakuwa na nia ya dhati ya kuyasimamisha.
Najua kuwa tunaposimulia haya, vijana husema kutujibu masikitiko yetu kuwa “Ya Kale Hayapo”. Lakini na sisi wazee tuliyoiona Zanzibar wakati wa hadhi na utukufu wake tunawaambia: “Mambo Kangaja Huenda Yakaja”. Soma Zaidi ...
Sunday, October 25, 2009
BARCALONA WAICHAKAZA ZARAGOZA 6-1
Saturday, October 24, 2009
CHELSEA WAIBAMIZA BLACKBURN STAMFORD BRIDGE
MWANAMKE APATWA NA UGONJWA BAADA YA KUDUNGWA SHINDANO YA KINGA YA MAFUA YA NGURUWE
Desiree Jennings, 25, alipatwa na ugonjwa unaompata mtu mmoja kati ya watu milioni moja baada ya kuchomwa sindano ya kinga ya mafua ya nguruwe ambayo ilisababisha awe kama amepooza.
Jennings hupatwa na maumivu makali sana anapotembea kwenda mbele na hulazimika kujinyonga nyonga na kuzungusha miguu yake ili kupunguza maumivu hayo lakini hata hivyo hawezi kutembea umbali mrefu.
Lakini hali hiyo hutoweka kabisa na hutembea vizuri kabisa anapotembea kinyume kinyume.
Cha ajabu zaidi huweza kukimbia kwenda mbele bila ya matatizo yoyote lakini anaposimama hali hubadilika na huhitaji mtu kumsaidia asianguke.
Hali hiyo ilimtokea siku 10 baada ya kuchomwa sindano hiyo ya kinga ya ugonjwa wa mafua ya nguruwe H1N1.
Ndoto ya Jennings kuwa mcheza shoo ya ushangiliaji wa timu ya soka ya Marekani ya Washington Redskins imetoweka baada ya kukumbwa na hali hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na madaktari Jennings anasumbuliwa na ugonjwa unaowapata watu wachache sana duniani unaoitwa dystonia.Ugonjwa huo huifanya misuli isinyae na kupelekea hali hiyo aliyo nayo.
Chini ni video yake inayomuonyesha jinsi anavyotembea kwa tabu kwenda mbele huku akitembea kinyume nyume bila matatizo yoyote.
Soma Zaidi ...Thursday, October 22, 2009
HONGERA TZ KWA MAENDELEO KATIKA ELIMU
JAMBAZI ASALI PAMOJA NA MTU ALIYETAKA KUMUIBIA
Jamaa mmmoja nchini Marekani alivamia duka la fedha akiwa na bunduki na kumwekea bunduki kichwani mfanyakazi wa duka hilo kwa nia ya kupora fedha lakini aliwashangaza watu alipobadili uamuzi wake ghafla na kupiga magoti chini na kuanza kumuomba msamaha.
Soma Zaidi ...Monday, October 19, 2009
Sunday, October 18, 2009
Saturday, October 17, 2009
BAADHI YA MATOKEO YA MECHI ZA LEO
Friday, October 16, 2009
GHANA MABINGWA WA DUNIA U20
MTOTO WA MAAJABU AWASHANGAZA WANASAYANSI DUNIANI
Wanasayansi nchini Urusi wameshindwa kujua ni nini kinapelekea mtoto anayeitwa Ali mwenye umri wa miezi tisa, mwili wake uwe unatoa maandishi tofauti tofauti ya kiarabu mara kwa mara.
Televisheni ya Vesti news ya nchini Urusi ilionyesha video ya mtoto huyo na picha ambazo wazazi wake wamekuwa wakimpiga kila maandishi mapya yanapotokea.
Kwa mujibu wa wazazi wake wanaoishi kwenye mji wa Dagestan, siku mbili baada ya Ali kuzaliwa herufi za kiarabu zilianza kujitokeza kwenye miguu yake na baada ya siku kadhaa zilianza kutengeneza maneno kamili.
Maandishi tofauti tofauti ya kiarabu hutokea zaidi kila siku ya jumatatu na ijumaa kwenye sehemu mbalimbali za mwili wake.
Awali kulikuwa na alama za maandishi yaliyofifia kwenye kidevu chake na baadae maandishi hayo yalijitokeza wazi yakisomeka "Allah", alisema mama wa mtoto huyo Madina Yakubova.
Miongoni mwa maneno ambayo yamesomeka wazi ni yale yanayosema "Waonyesheni watu dalili za kuwepo kwangu".Kwa kushangaza zaidi kwenye mguu mmoja wa Ali yalijitokeza maandishi yaliyosemeka "Allah (Mungu) ndiye muumba wa vitu vyote".
Ali alipozaliwa aligundulika kuwa na matatizo makubwa ya moyo wake na ugonjwa unaoathiri zaidi ubongo unaoitwa "cerebral paralysis" lakini alipopimwa tena baada ya maandishi hayo ya kiarabu yalipoanza kujitokeza aligundulika hana matatizo yoyote na afya njema.
Madaktari nchini Urusi hawajui ni nini kinaendelea kwenye mwili wa mtoto huyo na wamekiri hawajawahi kwamba hawana jibu la kutoa kwa taaluma za kisayansi. Soma Zaidi ...
Thursday, October 15, 2009
USIDHANI KAMA NI VITA!!!
Soma Zaidi ...
MATOKE YA MECHI ZA JANA KOMBE LA DUNIA
England 3 - 0 Belarus
Sweden 4 - 1 Albania
Denmark 0 - 1 Hungary
Portugal 4 - 0 Malta
Estonia 2 - 0 Belgium
Czech Republic 0 - 0 Northern Ireland
Poland 0 - 1 Slovakia
San Marino 0 - 3 Slovenia
Turkey 2 - 0 Armenia
Bosnia-Herzegovina 2 - 5 Spain
Republic of Ireland 0 - 0 Montenegro
Italy 3 - 2 Cyprus
Bulgaria 6 - 2 Georgia
Romania 3 - 1 Faroe Islands
Lithuania 2 - 1 Serbia
Switzerland 0 - 0 Israel
Greece 2 - 1 Luxembourg
Latvia 3 - 2 Moldova
Liechtenstein 0 - 2 Wales
Azerbaijan 1 - 1 Russia
Germany 1 - 1 Finland
Andorra 0 - 6 Ukraine
Kazakhstan 1 - 2 Croatia Soma Zaidi ...
BABA WA MAVAMIZI
Assalaam Alaaykum, (Toleo maalumu)
UMOJA, UHURU, UADILIFU
Baba wa mavamizi
Watawala Tanganyika wanatutia na sisi Zanzibar katika hekaheka za kumbukumbu za kifo cha “Mvamizi Nyerere”, huku wakidai kuwa ni kumbukumbu za kifo cha Baba wa Taifa. Kwa Zanzibar Nyerere ni “Baba wa Mavamizi”, si baba wa taifa. Baba wa Taifa havamii nchi za jirani zake. Haiwi iwe Nyerere Baba wa taifa na ndie alieleta majeshi ya Tanganyika kuivamia na kuiondoa Dola Huru ya Zanzibar mara tu baada ya Zanzibar kupata Uhuru wake na kujiunga na Umoja wa Mataifa ile Disemba 1963. Kutokana na mavamizi haya ndio ikafikishwa kuwa “Zanzibar si Nchi”. Lakinibasi, Wazanzibari kwa umoja na mshikamano wataendeleza juhudi zao mpaka Zanzibar ikomboke kutokana na ukoloni wa mvamizi Tanganyika na irejee kuwa ni Dola Huru Kaamili kama ilivyokuwa pale ilipojiunga na Umoja wa Mataifa ile 1963.
Wa Billahi Tawfiiq
Umoja wa Wazalendo
Zanzibar,
Jumaane, Oktoba 13, 2009
“…. وأمرهم شورى بينهم ……”.
“….., na mambo yao yakawa ni kwa kushauriana baina yao,…..”. Soma Zaidi ...
Wednesday, October 14, 2009
MECHI ZA KUFUZU KOMBE LA DUNIA KUENDELEA LEO
16:30Kazakhstan v Croatia
17:00Azerbaijan v Russia
17:00Germany v Finland
19:00Turkey v Armenia
19:00Bosnia-Herzegovina v Spain
19:00Republic of Ireland v Montenegro
19:00Italy v Cyprus
19:00Bulgaria v Georgia
19:00Romania v Faroe Islands
19:00Lithuania v Serbia
19:0Switzerland v Israel
19:00Greece v Luxembourg
19:00Latvia v Moldova
19:00Liechtenstein v Wales
19:30Estonia v Belgium
19:30Czech Republic v Northern Ireland
19:30Poland v Slovakia
19:30San Marino v Slovenia
19:45Sweden v Albania
19:45Denmark v Hungary
19:45Portugal v Malta
20:00France v Austria
20:00England v Belarus Soma Zaidi ...
Tuesday, October 13, 2009
Monday, October 12, 2009
WAPELEKA MALALAMIKO YAO KWA ALLAH
Soma Zaidi ...
Sunday, October 11, 2009
WENYE KAZI HII WAKO WAPI?
Soma Zaidi ...
ZOMBE AACHA KAZI
Abdallah Zombe aandika barua ya kucha kazi baada ya serekali kukata rufaa kupinga hukumu iliyotolewa na mahakama dhidi yake. Soma Zaidi ...
Saturday, October 10, 2009
ENGLAND YASHINDWA KUWEKA REKODI
MECHI ZA KUFURU KOMBE LA DUNIA ZINAUNGURUMA LEO
16:00Belarus v Kazakhstan
16:00Russia v Germany
16:45Luxembourg v Switzerland
17:00Estonia v Bosnia-Herzegovina
17:00Armenia v Spain
17:15Ukraine v England
18:00Montenegro v Georgia
18:00Cyprus v Bulgaria
19:00Denmark v Sweden
19:00Liechtenstein v Azerbaijan
19:30Serbia v Romania
19:30Austria v Lithuania
19:30Czech Republic v Poland
19:30Slovakia v Slovenia
19:30Greece v Latvia
19:45Belgium v Turkey
20:00Republic of Ireland v Italy
20:00France v Faroe Islands
20:00Israel v Moldova
20:45Portugal v Hungary Soma Zaidi ...
Friday, October 9, 2009
Ahadi nono ya Bosi huyo ameitoa mbele ya viongozi wa timu hiyo wakati akiwa ziarani nchini humu hivi karibuni,akisimulia kuhusu hadi hiyo huko Rahaleo Mjini Unguja,
Meneja wa klabu hiyo Abubakar Wakili , alisema kuwa Bosi huyo tayari ameshafanya mazungumza ya awali na uongozi wa timu hiyo juu ya dhamira yake ya kukisaidia kikosi cha Miembeni.
Wakili alifahamisha kuwa mazungumzo hayo ya awali kwa uongozi wa Miembeni na Bosi Abramovic, yalimefanyika huko Mkoani Arusha Tanzania Bara, lakini bosi huyo hakuweza kumaanisha ni msaada gain atakaoutoa kwa klabu hiyo.
Hata hivyo Kaimu katibu huyo alisema kuwa hivi sasa kilichobakia ni umalizaji wa mazungumzo yao na Bosi huyo, ambapo wanataraji hivi karibuni watakamilisha.
Hatua ya Miembeni ya kusaka mfadhili kwa klabu yao imekujaa baada ya aliyekuwa mfadhili wa mwanzo Amani Makungu kuiwachia mkono timu hiyo na hivi sasa klabu hiyo inaendeshwa na Wazee wa dhama zilizoipita wa timu hiyo.
Tuesday, October 6, 2009
VIDIO YA JOHN LEGEND ALIYORIKODI ZNZ
I realized as I lay down to sleep
We haven't spoke in weeks-
So many things that I'd like to know
Come have a talk with me
I need a sign, something I can see
Why all the mystery?
I try not to fall for make believe
But what is reality?Where do we go?
What do we know?
Life has to have a meaning
Show me the light
Show me the way
Show that you're listening
Show me that you love me
Show me that you walk with me
Hopefully, just above me
Heaven's watching over me
Guess it's funny how I say thanks to you
For all you've given me
Sometimes the price of what you gave to me
I can't stop questioning
O God of love, peace, and mercy
Why so much suffering?
I pray for the world, it gets worse to me
Wonder if you're listening
When people go
Why do they go?
Why don't you choose me?
But someday I know
I'm gonna go
I hope you're waiting for me
Show me that you love me
Show me that you walk with me
Hopefully, just above me
Heaven's watching over me
Maybe we'll talk
Some other night
Right now I'll take it easy
Won't spent my time
Waiting to die
Enjoy the life I'm living
Show me that you love me
Show me that you walk with me
Hopefully, just above me
Heaven's watching over me
Soma Zaidi ...Monday, October 5, 2009
HUWEZI KUNUNUA MAYAI ZIMBABWE KAMA SIO BILIONEA
WABONGO NA VITAMBAA VYA SHINGO
Sunday, October 4, 2009
LIVERPOOL WASHINDWA KUPUMUA KWA STAMFORD BRIDGE
Soma Zaidi ...
Saturday, October 3, 2009
Umoja na mshikamano ndio ngao zetu
“Na shikamaneni kwa Dini ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja,
wala msifarikiane…”.
Wazee wetu, Ndugu zetu,
Assalaam Alaaykum,
UMOJA, UHURU, UADILIFU
UMOJA NA MSHIKAMANO NDIO NGAO ZETU
Maneno haya ya hikma, “Umoja na Mshikamano ndio ngao zetu”, yamebainishwa tena hivi karibuni na Rais wa Zanzibari, Mhishimiwa Aman Abeid Aman. Yamesemwa, kuandikwa kwa khati kubwa na kuwekwa sehemu mbalimbali. Yamebainishwa kwa hali hii, ili daima sisi Wazanzibari tuzidi kuyazingatia na kuyafanyiakazi. Hapana shaka maneno haya ni kulingana na Maamrisho ya Mola wetu Mlezi, Subhaanahu wa Taáala anavyotwambia:
“Na shikamaneni kwa Dini ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane…”.
Umoja wa Wazalendo, unatoa shukrani za dhati kwa Mhishimiwa Rais Aman; na kuahidi kuyazingatia kwa kina kabisa, kuyathamini na kuyafanyiakazi maneno haya kila wakati. Hivi zaidi ni kutokana na imani ya Wazanzibari kwamba “Umoja na Mshikamano” ndio nyenzo kuu ya kuendeleza juhudi za kuitoa Nchi yetu, Zanzibar kutokana na makucha ya “mkoloni mvamizi; Tanganyika” na kuirejesha Dola Huru Kaamili ya Zanzibar kama ilivyokuwa siku ile ilipojiunga na Umoja wa Mataifa, Disemba kuminasita, 1963.
Umoja wa Wazalendo, unatambuwa vyema kuwa kila ukizidi kushamiri na kudhihiri Umoja na Mshikamano wa Kizanzibari, ndivyo mkoloni mvamizi; Tanganyika anavyozidisha mbinu zake ovu za kuwagombanisha Wazanzibari ili kuwafarikisha hivyo aendeleze kwa mbinu na nguvu utawala wake wa kikoloni juu ya Zanzibar. Umoja wa Wazalendo, unatambuwa vyema kuwa huu ukatili unaofanywa na majeshi ya mkoloni mvamizi, Tanganyika katika hiki kipindi cha kuelekea uchaguzi ni miongoni mwa mbinu hizo za kuwagombanisha na kuwafarikisha Wazanzibari. Lakinibasi, lazima atambue mkoloni mvamizi; Tanganyika kwamba zama za kuwagombanisha na kuwafarikisha Wazanzibari zimeshapitwa na wakati. Wazanzibari daima watasimama begakwabega katika juhudi za ukombozi wa Nchi yao, Zanzibar.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu, Subhaanahu wa Taáala atujaalie kila kheri na atuepushe na kila shari; na atujaalie ufunguzi wa karibu, Aamyn.
Wa Billahi Tawfiiq
Umoja wa Wazalendo
Zanzibar, Ijumaa October 02, 2009
“…. وأمرهم شورى بينهم ……”.
“….., na mambo yao yakawa ni kwa kushauriana baina yao,…..”. Soma Zaidi ...
ELIMU BURE!!
Soma Zaidi ...
OWEN NJE!!!
Birmingham watakua ugenini leo hii wakipambana na bernly huku wkaimkosa mshambuliaji wao Christian Benitez ambae amesafiri kwenda kwao Ecuado baada ya baba yake kupata ajali ya gari.
Nao Bolton watacheza dhidi ya Tottenham bila ya mshambuliaji wao msweeden Johan Elmander baada ya kushtuka mshipa wa nyuma ya goti,kwa upande wa Tottenham wanatarajia kumchezesha Jermain Defoe licha ya kua na maumivu ya mkno.
Nao Huul watakua nyumbani kukwaruzana na Wigan huku Hull wakitaka kumjaribu Anthony Gadner kabla ya mechi kusudi kuona kama ataweza kucheza baada ya kukaa juu kwa mechi nne kutokana na kusumbuliwa na goti ambapo Liam Cooper akiwa pia anasumbuliwa na mshipa wa nyuma ya goti.
Wolves watawakaribisha Portmouth wakiwa bila ya David Johns ambae amefanyiwa upasuaji wa goti na atakua juu kwa muda wa miezi miwili. Soma Zaidi ...