Thursday, October 15, 2009

BABA WA MAVAMIZI

Wazee wetu, Ndugu zetu;
Assalaam Alaaykum, (Toleo maalumu)
UMOJA, UHURU, UADILIFU
Baba wa mavamizi


Watawala Tanganyika wanatutia na sisi Zanzibar katika hekaheka za kumbukumbu za kifo cha “Mvamizi Nyerere”, huku wakidai kuwa ni kumbukumbu za kifo cha Baba wa Taifa. Kwa Zanzibar Nyerere ni “Baba wa Mavamizi”, si baba wa taifa. Baba wa Taifa havamii nchi za jirani zake. Haiwi iwe Nyerere Baba wa taifa na ndie alieleta majeshi ya Tanganyika kuivamia na kuiondoa Dola Huru ya Zanzibar mara tu baada ya Zanzibar kupata Uhuru wake na kujiunga na Umoja wa Mataifa ile Disemba 1963. Kutokana na mavamizi haya ndio ikafikishwa kuwa “Zanzibar si Nchi”. Lakinibasi, Wazanzibari kwa umoja na mshikamano wataendeleza juhudi zao mpaka Zanzibar ikomboke kutokana na ukoloni wa mvamizi Tanganyika na irejee kuwa ni Dola Huru Kaamili kama ilivyokuwa pale ilipojiunga na Umoja wa Mataifa ile 1963.

Wa Billahi Tawfiiq
Umoja wa Wazalendo
Zanzibar,
Jumaane, Oktoba 13, 2009
“…. وأمرهم شورى بينهم ……”.
“….., na mambo yao yakawa ni kwa kushauriana baina yao,…..”.

No comments:

Post a Comment