
Birmingham watakua ugenini leo hii wakipambana na bernly huku wkaimkosa mshambuliaji wao Christian Benitez ambae amesafiri kwenda kwao Ecuado baada ya baba yake kupata ajali ya gari.
Nao Bolton watacheza dhidi ya Tottenham bila ya mshambuliaji wao msweeden Johan Elmander baada ya kushtuka mshipa wa nyuma ya goti,kwa upande wa Tottenham wanatarajia kumchezesha Jermain Defoe licha ya kua na maumivu ya mkno.
Nao Huul watakua nyumbani kukwaruzana na Wigan huku Hull wakitaka kumjaribu Anthony Gadner kabla ya mechi kusudi kuona kama ataweza kucheza baada ya kukaa juu kwa mechi nne kutokana na kusumbuliwa na goti ambapo Liam Cooper akiwa pia anasumbuliwa na mshipa wa nyuma ya goti.
Wolves watawakaribisha Portmouth wakiwa bila ya David Johns ambae amefanyiwa upasuaji wa goti na atakua juu kwa muda wa miezi miwili.
No comments:
Post a Comment