Thursday, February 11, 2010

MADE IN AFGHANSTAN


Soma Zaidi ...

KIKAO MAALUM CHA UMOJA WA ULAYA KUJADILI MZOZO WA UGIRIKI

Umoja wa Ulaya unazingatia kuisaidia Ugiriki inayokabiliwa na tatizo kubwa la madeni. Hayo alitamka Kansela wa Austria Werner Faymann siku moja kabla ya kufanywa mkutano maalum wa viongozi wa umoja huo leo hii mjini Brussels.

Hapo awali,Waziri Mkuu wa Uhispania José Luis Rodríguez Zapatero alie pia Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya, alihakikisha kuwa Ugiriki itasaidiwa na umoja huo.

Wakati huo huo nchini Ugiriki wafanyakazi kutoka sekta za kuhudumia umma,wameandamana kwa maelfu kupinga mipango ya serikali ya kupunguza matumizi yake. Kuambatana na mipango hiyo, wafanyakazi serikalini hawatopata nyongeza ya mishahara na hakuna wafanyakazi wapya watakaoajiriwa katika sekta za kuhudumia umma.

Kwa kuchukua hatua hizo,serikali ya Ugiriki inajaribu kupunguza nakisi iliyovunja rekodi ikiwa ni asilimia 13 ya bajeti yake. Lengo ni kuwa ifikapo mwaka 2014 nakisi hiyo itafikia asilimia 3 ya bajeti, ambacho ni kiwango kinachoruhusiwa na Umoja wa Ulaya. Soma Zaidi ...

HABARI KATIKA PICHA


Soma Zaidi ...

Wednesday, February 10, 2010

AJUZA WA MIAKA 80 ABAKWA BAGAMOYO

Ajuza wa miaka 80, mkazi wa kitongoji cha Kiwangwa wilayani Bagamoyo amebakwa na kijana mwenye umri wa miaka 35 na kusababishiwa majeraha makali katika sehemu zake za siri.


Tukio hilo lilitokea saa 8:00 usiku wa kuamkia jana na kwamba kijana aliyehusika na tukio hilo (jina linahifadhiwa), lakini ni mkulima wa Kiwangwa wilayani humu.


Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Absalom Mwakyoma alidhibitisha tukio hilo na kusema kuwa bibi kizee huyo alibakwa wakati akiwa amelala nyumbani kwake ambapo mtuhumiwa alitumia mbinu ya kuvunja mlango usiku huo na kuingia katika chumba cha ajuza huyo kisha kumbaka kwa nguvu.


Mwakyoma alisema tukio hilo linasikitisha na kutia aibu vijana kutokana na ukweli kwamba bibi huyo anaishi kwa shida na taabu nyingi.


"Inavyoonekana huyo jamaa, alikuwa anamvizia ajuza kwa muda mrefu na nadhani alikuwa akimfuatilia kwa karibu ili kujua mwenendo mzima,alipobaini analala mwenyewe ndipo alipotumia mbinu ya kumvizia muda huo na kuvunja mlango na hatimaye kumbaka hata imani za kishirikina zinaweza kuwa ni chanzo,"alisema Mwakyoma.


Alisema mlalamikaji anaishi mwenyewe kwenye nyumba hiyo na kwamba tayari mtuhumiwa alikamatwa na anaratajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote mara uchunguzi utakapokamilika, mlalamikaji anaendelea vizuri.


Katika tukio jingine Kamanda huyo wa Polisi Pwani alisema mkazi wa Kongowe wilayani Kibaha,(Jina linahifadhiwa) alikamatwa kwa kosa la kukutwa na meno ya tembo vipande vinne vyenye uzito wa kilogramu 15.1 vya thamani ya Sh 1.1milioni.


Tukio hilo lilitokea saa 8.00 mchana juzi katika eneo la shule ya msingi Kongowe na waliomkamata mtuhumiwa huyo ni maafisa wa maliasili wa kituo cha Kongowe kwa ushirikiano na askari polisi na kwamba mzee huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote. Soma Zaidi ...

IF YOU NOTICE THIS!!!!


Soma Zaidi ...

NGOMA TUKUTANE CHINIIII


Soma Zaidi ...

WAZIRI AKOSA LA KUJIBU BUNGENI

Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Jeremiah Sumari, jana alilishangaza Bunge baada ya kutoa jibu ambalo halikutarajiwa na wabunge.

Naibu waziri huyo alisema kuwa “hajui” mara baada ya kuulizwa swali na Mbunge wa Magogoni, Vuai Abdallah Khamis (CUF), aliyetaka kufahamu kwa nini kodi inayokatwa kwa wafanyakazi wa Zanzibar kwenye Serikali ya Muungano isibaki visiwani Zanzibar.

“Spika, napenda kumjibu mheshimiwa Mbunge kuwa sijui,” jibu hilo la Sumari lilisabaisha wabunge kuangua vicheko huku mwenyewe akiridhika na kurejea kwenye kiti chake, hali iliyosababisha Naibu Waziri mwenzake, Omar Mzee kumsaidia kujibu swali hilo.

Wakati akiuliza swali la nyongeza, mbunge huyo alitaka kujua kwa nini kodi za mishahara ya wafanyakazi wa Jamhuri ya Muungano walioko visiwani humo zisiwanufaishe wananchi wa huko.

Katika swali lake la msingi, mbunge huyo alisema kuwa wafanyakazi wamekuwa wakikatwa kodi kutoka katika mishahara yao ili kuchangia huduma za jamii na mambo mengine kwanini walioko Zanzibar wasikatwe na fedha zibaki huko kwa ajili ya Zanzibar.

Akijibu swali lililomshinda Sumari, Mzee alisema pale ambapo mishahara inakokotolewa ndipo ambapo kodi inakatwa na kuwa mishahara aliyoizungumzia mbunge huyo huwa inakokotolewa Tanzania Bara.

Awali akijibu swali la msingi la Khamis Sumari alisema kodi ya mapato ni kodi ya muungano na hutozwa kwa utaratibu wa zuio kama ilivyoainishwa katika sheria ya kodi ya mapato.

Alisema utaratibu unampa mwajiri kukata kodi mahali ambapo hati ya kutayarisha mshahara wa mfanyakazi huandaliwa.

Alibainisha kuwa hati ya malipo hutayarishwa Bara, kodi ya mapato hukatwa Bara na kuingizwa katika mfuko mkuu wa serikali ya Jamuhuri ya Muungano na kama hati hiyo ya malipo hutayarishwa Zanzibar, kodi ya makato hukatwa Zanzibar na huingizwa katika mfuko Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Soma Zaidi ...

MAJI NI AFYA

Correct timing to take water, will maximize its effectiveness to Human body. Two (02) glass of water - After waking up - Helps activate internal organs

One (01) glasses of water - 30 minutes before meal - Help digestion

One (01) glass of water - Before taking a bath - Helps lower blood pressure

One (01) glass of water - Before sleep - To avoid stroke or heart attack



Soma Zaidi ...

Tuesday, February 9, 2010

TIMU YA TAIFA YA BENIN YAVUNJWA


Shirikisho la mchezo wa soka nchini Benin, limevunja kikosi kizima cha timu ya taifa ya nchi hiyo kufuatia matokeo mabaya katika michuano ya kuwania kombe la mataifa bingwa barani Afrika.

Kocha wa timu hiyo raia wa Ufaransa Michel Dussuyer na maafisa wote wa kiufundi pia wamefutwa kazi. Kwa mujibu maafisa wakuu wa shirikisho hilo, kikosi hicho kimevunjwa kutokana na utovu wa nidhamu na kutowajibika kama wazalendo.

Timu hiyo inayojulikana kama The Squirrels, iliyaaga mashindano hayo nchini Angola, baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu katika kundi lake na alama moja pekee.
Soma Zaidi ...

DR CONRAD MURRAY ABURUZWA MAHAKAMANI

Daktari wa Michael Jackson, Conrad Murray alifikishwa katika mahakama mjini Los Angeles na kushtakiwa kwa kusababisha kifo cha mwanamuziki huyo miezi saba iliyopita.

Murray alikuwa ameajiriwa kumsaidia Michael Jackson kujiandaa kwa tamasha kadhaa mjini London na inaaminiwa kuwa alikuwa mtu wa mwisho kumwona mwanamuziki huyo akiwa hai.

Inadaiwa kuwa daktari Murray aliwaeleza wapepelezi kuwa alimpa Jackson dawa kadhaa ikiwemo ile yenye nguvu nyingi ya Propofol ambayo kwa kawaida hutumika hospitalini pekee.

Inadaiwa baada ya kumpa dawa hiyo Murray aliondoka kwa muda mfupi kutoka chumbani mwa Jackson ili kupokea simu na aliporudi akampata mwanamuziki huyo hapumui.

Afisa wa upelelezi alimpata daktari huyo na hatia ya kumpa Michael Jackson propofol kwa kupita kiasi kilichostahili na hivyo kusababisha kifo chake. Lakini alipofikishwa mahakamani kwa kosa hilo ambalo linaweza kumpa kifungo cha miaka 4 gerezani, Daktari Murray alisisitiza kuwa hakuna na hatia.

Daktari Murray aliachiliwa kwa dhamana ya dola 75,000 akisubiri kusikilizwa kwa kesi yake mwezi april Soma Zaidi ...

Monday, February 8, 2010

VITAMBULISHO VYA KITAIFA KUGHARIMU BILIONI 200/-


Serikali imetenga sh bilioni 200 kwa ajili ya mradi wa utambuzi na usajili wa raia wake ambapo wakimbizi na wageni wataingia kwenye orodha hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Dickson Maimu, alisema fedha hizo zitatumika kwa miaka mitano.

Alisema fedha hizo zitahudumia miradi midogo midogo 14 ikiwemo kuanzisha ofisi kwa kila wilaya nchini kabla ya kuanza rasmi kwa kazi ya utambuzi na usajili ikishirikiana na wadau mbalimbali.

Mkurugenzi huyo alisema pia mradi utawaandikisha watu wote waliopo Tanzania bila kujali uraia wao na kwamba wakimbizi wataingia kwenye mradi huo.

“Hizi pesa ni nyingi kuzitaja, lakini ukweli ni kwamba zitatumika kwa miaka minne kutekeleza miradi midogo midogo ikiwemo ujenzi wa ofisi kila wilaya, ili kuwafikia wananchi wote.

“...Vitambulisho vya utaifa ni kwa ajiri ya usalama, wapo wanaofikiri sisi tunachapisha vitambulisho. Hapana! tunafanya utambuzi na kusajili watu walioko nchini kwa usalama wa nchi.

“Hivi vitasaidia kujua nani ni nani, anafanya nini na anamiliki nini. Hii itatusaidia hata kwa wageni. Mfano mzuri ni maafa ya Mbagala pale kusingekuwa na usumbufu kama mradi huu ungekuwepo watu wangetambuliwa,” alisisitiza Maimu na kubainisha kwamba watakaotambuliwa na kusajiliwa ni watu wenye miaka 18 na zaidi.

Alisema awali yalijitokeza makampuni 104 kutaka kupewa zabuni ya kufanya kazi hii kutokana na kushindwa kuelewa ugumu wa kazi na kwamba katika mchujo wa pili wa kumpata mkandarasi yamebaki makampuni matano yote kutoka nje ya nchi.

Kuundwa kwa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ni kutokana na uwezo alionao rais chini ya Ibara ya 36 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano na kwamba hicho ni chombo cha Muungano.

“Mpaka sasa mshauri mwelekezi amepatikana nayo ni kampuni ya Gotham iliyoshiriki katika upembuzi yakinifu ili kumpata mkandarasi atakayemudu kazi hii..,” alisema mkurugenzi huyo aliyeanza kazi Desemba mwaka jana.
Soma Zaidi ...

WASOMALI WAWAOKOA WAHAMIAJI

Takriban watu 126 wameokolewa na wavuvi wa kisomali kutoka ghuba ya Aden baada ya wafanyabiashara wanaouza watu walipowalazimisha kuingia baharaini huku wakiwa wamewaelekezea bunduki.

Wahamiaji, wengi kutoka Somalia na Ethiopia, wamesema walitokea kaskazini mwa Somalia wiki moja iliyopita.

Wamesema boti yao ilipata hitilafu katika injini na kuelea kwa siku kadhaa kabla ya watu hao wanaouza binadamu kuanza kuwalazimisha kuingia baharini.

Watu sita mpaka sasa hawajulikani walipo.

Mwandishi wa BBC Peter Greste amesema matukio kama haya si aghlabu kutokea.

Mlinzi wa pwani katika eneo lililojitenga la Somaliland aliwagundua watu watano wa awali walionusurika wakielea kwenye maji siku ya Jumapili. Soma Zaidi ...

KIKWETE ZIARANI KILOSA

Rais Kikwete jana alitembele maeneo yaliyokumbwa na mafuriko huko Mkoani Kilosa kufuatia mvua zilizonyesha hivi karibuni.


Soma Zaidi ...

MWIZI SUGU ATIWA MOTO MOMBASA

Jamaa mmoja anaejuilikana kwa jina la Big man alikamatwa na wananchi wenye hasira na kuchomwa moto hadi kufariki dunia, jamaa huyo ambae inasemekana ni mwizi hatari ambae anawasumbua sana wakaazi wa mtaa wa Bush bar mjini Mombasa alikamatwa na kuchomwa moto juzi mnamo majira ya saa mbili asubuhi, wakaazi wa maeneo ya Bush bar walionesha kufurahishwa na kifo cha mwizi huyo kwani imeelezwa kuwa jamaa huyo alikuwa kero sana hasa kwa akina mama ambao walikua wakenda sokoni huwa anawavamia na kuwapiga baadae kuwanyang'anya vitu vyao. Soma Zaidi ...

Sunday, February 7, 2010

DROGBA AWALIZA ARSENAL

Magoli mawili yaliyopachikwa na mshambuliaji machachari wa Chelsea Drogba leo hii walipocheza dhidi ya washika bunduki Arsenal imewarudisha tena Chelsea kileleni mwa ligi kuu ya Uingereza, mechi hio iliyochezwa katika uwanja wa Stamford Bridge ulikua ni wa upande mmoja ambapo Chelsea waliutawala sana mchezo na washika bunduki kuonekana si lolote si chocho huku wakicheza pasi zao fupi fupi zisizo na mafanikio, kwa matoke hayo Chelsea wanaongoza msimamo wakiwa na alama 58 ikiwa ni tofauti ya alama mbili tu MANU ambao wako nafasi ya kwa alama 56 na nafasi ya tatu wapo washika bunduki na alama zao 49. Soma Zaidi ...

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE

Mtokeo ya kidacho cha nne ( form iv) yametoka kwa kuangalia matokeo hayo tembea link ifuatayo:

http://www.necta.go.tz/html_csee209/olevel.htm Soma Zaidi ...

Saturday, February 6, 2010

MANCHESTER YAPAA KILELENI KWA 5-0

Manchester Utd leo hii wameshika usukani wa ligi kuu Uingereza baada ya kuwafunga Potmouth kwa jumla ya magoli 5-0 katika mchezo uliofanyika uwanja wa Oldtrafford, kwa matokeo hayo Man Utd sasa wanakua na alama 56 wakati timu ya Chelsea ikishikilia nafasi ya pili kwa alama 55 lakini Chelsea wana nafasi kubwa bado ya kuongoza ligi hio ikiwa watashinda katika mechi yao ya kesho dhidi ya washika bunduki Arsenal, nao Arsenal wapo katika nafasi ya tatu kwa alama 49 huku walemavu Liverpool wamejikomboa na kufika katika nafasi ya nne baada ya kushinda mechi yao ya leo 1-0 dhidi ya Everton. Soma Zaidi ...

NA MIMI BADO NIMO!!!!

Waziri Khatibu akimuonesha Bi Teddy Mapunda kama na yeye bado wakati unamruhusu kuserebuka.
Soma Zaidi ...

KAWIA UFIKE


Soma Zaidi ...

UPEPO MKALI WAATHIRI MORO

Upepo mkali ulioambatana na mvua kubwa umeleta athari kwa wakaazi wa maeneo ya Morogoro Mjini, upepo huo ulitokea jana mnamo majira ya saa nane mchana umeangusha miti na kuharibu nyumba pamoja na mali nyengine za wakaazi wa maeneo hayo. Soma Zaidi ...

LEO OLD TRAFFORD



Premier League
13:45 Liverpool v Everton
16:00 Bolton Wanderers v Fulham
16:00 Burnley v West Ham United
16:00 Hull City v Manchester City
16:00 Manchester United v Portsmouth
16:00 Stoke City v Blackburn Rovers
16:00 Sunderland v Wigan Athletic
18:30 Tottenham Hotspur v Aston Villa

La Liga
18:00 Valencia CF v Real Valladolid
20:00 FC Barcelona v Getafe CF
22:00 Real Madrid v RCD Espanyol

Serie A
18:00 Palermo v Parma
20:45 Livorno v Juventus

Bundesliga
15:30 VfL Bochum v Bayer Leverkusen
15:30 1. FC Köln v Hamburger SV
15:30 Hoffenheim v Hannover 96
15:30 VfL Wolfsburg v Bayern München
15:30 SC Freiburg v Schalke 04
18:30 1. FC Nürnberg v VfB Stuttgart

Dutch Eredivisie
18:45 PSV v ADO Den Haag
19:45 sc Heerenveen v FC Utrecht
19:45 Roda JC v Sparta Rotterdam
20:45 Heracles Almelo v FC Groningen

NB: Ratiba hii ni kwa (CET) Soma Zaidi ...

BAN AZUNGUMZIA VITA VYA GAZA

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon amesema bado hakuna ushahidi wa kutosha unaoonyesha iwapo Israel na Palestina zimetekeleza matakwa ya umoja huo kufanya uchunguzi wa vita vya Gaza mwaka uliopita. Taarifa iliyotolewa na Bwana Ban kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, imeeleza kuwa hakuna uamuzi unaoweza kutolewa juu ya utekelezaji wa azimio la pande zote zinazohusika.

Jana Ijumaa Israel ilisema kuwa uchunguzi wa kijeshi ilioufanya kuhusu vita hivyo ulikuwa wa kuaminika, lakini kundi la kutetea haki za binaadamu la Gaza limedai kuwa uchunguzi wa Israel haukukidhi matakwa ya Umoja wa Mataifa ya kufanya uchunguzi huru.

Taarifa zinazokinzana zimetolewa baada ya tarehe ya mwisho ya miezi mitatu iliyowekwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa Israel na kundi la Hamas kuchunguza madai kwamba wanahusika katika uhalifu wa kivita wakati wa vita vya Gaza Disemba mwaka 2008 hadi Januari mwaka uliopita, kumalizika siku ya Ijumaa. Soma Zaidi ...

Friday, February 5, 2010

RADA YA TANZANIA YAIGHARIMU BAE

BAE Systems, mojawapo ya makampuni makubwa kabisa duniani ya uundaji wa vifaa vya kijeshi, itatozwa faini ya dola milioni 400.

BAE inalipa faini hiyo baada ya kukiri hatia ya kufanya njama ya kuwasilisha taarifa za fedha zenye udanganyifu mbele ya serikali ya Marekani.

Vile vile, imekubaliana na Idara ya Upelelezi wa Makosa Mazito ya Ugandanyifu ya Uingereza (SFO), kukiri kuwa na hatia ya kushindwa kutekeleza wajibu wake.

Wajibu huo ulikuwa ni kuweka kumbukumbu sahihi za mahesabu katika malipo yaliyofanywa kwa mshauri wake wa masoko nchini Tanzania ili kufanikisha mauzo ya rada ya kuongozea ndege.

BAE Systems imeagizwa na idara hiyo ya Uingereza, kulipa faini ya dola milioni 30, ambapo kati ya hizo, kiasi kitapelekwa Tanzania kusaidia shughuli za hisani.

Hata hivyo, hatua hiyo ni fedheha kubwa kwa BAE kutokana na kukiri kuwa na hatia ya mashtaka ya jinai Marekani na Uingereza.

Ingawa adhabu ya Uingereza inaonekana kuwa ndogo kuliko ile ya SFO iliyokuwa ikitaka, inaaminika kuwa ni rekodi ya kipekee kwa kampuni ya Uingereza kukutwa na hatia ya jinai.

Mashtaka ndani ya Uingereza yanahusiana na kampuni hiyo kuiuzia Tanzania rada ya kuongozea ndege kwa mamilioni ya dola katika mkataba wenye utata uliosaniwa mwaka 1999. Soma Zaidi ...

KARATA TATU DARAJANI USIKU

Assalaam alaikum
Hakuna mchezo mbaya kati ya michezo ya hadaa ambao ni wizi mtupu kama karata tatu, mchezo huu huchezwa kwa kutumia vibiriti ama kifunikio vya chupa, ambapo kundi la vijana kama 7 hukaa pamoja ili kuvutia watu.
Huku wajifanya nao ni wateja huku wakijishindia pesa na unapokaribia wewe huvutika na kuanza kuchagua kibiriti chenye njiti kwa kubadilishwa cha kati kuletwa kushoto na cha kushoto kati au kulia.
Baada ya kwisha hutulia na kukutaka uchague chenye njiti hapo huchagua chenye njiti na kukuonyesha umeshinda toa elfu 10000 ushinde elfu 40000, na ukiwa mbioni kujifundua mmoja wao hukupiga kibega na unapoangalia basi haraka hubadilishwa na baada ya kutoa pesa basi huwambiwa umekosa jaribu bahati yako tena.
Na unapotaka kuleta fujo basi hudhibitiwa na hata kupigwa mateke huo ni mmoja kati ya michezo ya wizi ya Kitanganyika au wabongo na sasa mchezo huu huchezwa Darajani usiku karibu na duka la madawa la Fahud.

Wazanzibari amkeni!!!
Soma Zaidi ...

WAMAREKANI WAKUTWA NA MAKOSA YA KUTEKA WATOTO HAITI

Wamisionari 10 wa Kimarekani wameshtakiwa kwa makosa ya kujaribu kuwateka nyara watoto 33 wa Haiti, wakitumia mwanya wa tetemeko kubwa la ardhi lililoikumba Haiti mwezi uliyopita.

Wamarekani hao wanaume watano na wanawake watano, walizuiwa na kukamatwa katika mpaka wa nchi hiyo na Jamuhuri ya Dominica wakati walipokuwa wakijaribu kuvuka mpaka huo wakiwa katika basi pamoja na watoto hao.

Watuhumiwa hao ambao wengi wao ni watumishi wa kanisa katika jimbo la Idaho nchini Marekani, wamesema kuwa walikuwa wakijaribu kuwaokoa watoto hao waliyotelekezwa na ambao walikuwa ni mayatima, na kwamba hawakujua kuwa walikuwa wakitenda kosa la kihalifu.

Iwapo watapatikana na hatia wanaweza kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka 15 gerezani.Tetemeko hilo nchini Haiti limesababisha takriban watu millioni moja kukosa makaazai na wamekuwa wakiishi mitaani. Soma Zaidi ...

WABONGO NA UBINAFSISHAJI

Hii inaonyesha ni jinsi gani Watanzania walivyobobea katika mambo ya ubinasishaji, maana wamefiki mpaka kubinafsisha alama ya Negative na kutokana na alama hio hawana kazi nayo, kwa sasa kila kitu kwao ni Positive tu.


Soma Zaidi ...

HABARI KATIKA PICHA


Soma Zaidi ...

SARATANI YA KIZAZI YAKITHIRI TANZANIA

Tanzania imekuwa ikipoteza watu 30,000 kati ya 40,000 kila mwaka kutokana na ugonjwa wa saratani.
Wanawake ndio wanaotajwa kuathirika zaidi kwa saratani ya shingo ya kizazi.

Kutokana na Tanzania kuwa na hospitali moja tu ya kutibu maradhi hayo iliyopo mjini Dar Es Salaam wagonjwa hulazimika kulala chini kutokana na msongamano.

Wengine hutibiwa majumbani kwa ukosefu wa nafasi za kuwalaza.

Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya saratani Tanzania, Dr Twalib Ngoma amesema wazazi washauriwe kuwapa chanjo watoto licha ya kuwa gharama kubwa.

Gharama ya chanjo hiyo ni dola 900 sawa na zaidi ya shilingi milioni moja na laki mbili za kitanzania. Soma Zaidi ...

Thursday, February 4, 2010

RAIS OBAMA ALAANI MUSWADA WA UGANDA

Rais wa Marekani Barack Obama amekosoa pendekezo la sheria lililotolewa Uganda la kupinga mapenzi ya jinsia moja na kulieleza kuwa jambo la kuchukiza.
Muswada huo unapendekeza mwenye hatia kufungwa jela kwa muda mrefu au hata adhabu ya kifo katika baadhi ya matendo hayo ya jinsia moja.

Bw Obama amewaambia wanasiasa na viongozi wa dini katika maombi ya kitaifa ya Marekani mjini Washington, "Kuwalenga wapenzi wa jinsia moja kwa jinsi walivyo ni kuvuka mipaka".

Vitendo vya mapenzi ya jinsia moja tayari ni kinyume na sheria nchini Uganda na adhabu yake ni kifungo jela kwa takriban miaka 14.

Mswada huo unatarajiwa kuongeza uzito wa adhabu hiyo kwa kupewa kifungo cha maisha.
Soma Zaidi ...

ADHA YA USAFIRI

Serikali inapaswa kutafuta ufumbuzi wa tatizo la usafiri kwa wanaunzi, kwa kweli wanapata tabu sana katika usafiri wao wa kwenda na kuduru maskulini
Soma Zaidi ...

NO PARKING

Hawa tena wamezidi hii alama ya NO PARKING imewekwa mpaka hapa mwituni kuna nini hapa? Soma Zaidi ...

TAXI ZA KENGEJA

Nakumbuka mnamo mwaka 1995/96 nilikwenda kutembea Kengeja Pemba nikakutana na hizi Taxi, uzuri wa Taxi hizi kwanza ni tofauti na zile za kawaida, hizi zilikua ni kama dala dala wewe utapanda na akitokezea mwngine anapanda,huwa hazijai zina uwezo wa kuchukua abiria mpaka 10 na dereva huwa anapata nafasi ndogo tu ya kukaa na safari inakua raha mustarehe. Soma Zaidi ...

WAPI HAPA?


Soma Zaidi ...

Wednesday, February 3, 2010

AL-BASHIR HUENDA AKASHTAKIWA

Majaji rufaa wameiambia mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC kuangalia upya iwapo Rais wa Sudan, Omar al-Bashir ashitakiwe kwa mauaji ya kimbari mjini Darfur.

Majaji walibatilisha uamuzi wa awali kwa madai kuwa waendesha mashitaka hawakutoa ushahidi wa kutosha.

Mwendesha mashitaka mkuu ameiambia BBC uamuzi wa Bw Bashir wa kuyafukuza mashirika ya kutoa misaada mwaka jana baada ya ICC kutoa kibali cha kukamatwa kwake ni ushahidi mpya wa nia yake ya mauaji hayo.

Sudan imesema uamuzi uliotolewa na jopo hilo ni sababu za kisiasa.

Rais al-Bashir amekataa kuitambua mahakama ya kimataifa ya ICC.

Umoja wa Mataifa unaamini takriban watu laki tatu wamefariki dunia kutokana na mapigano mjini Darfur. Soma Zaidi ...

TUMEVUKA MIPAKA

Mwanamke huyu ambae inasemekana ni muislamu ameutumia mwili wake kwa ajili ya kuudhalilisha uislamu,aya tukufu ya Allah ameichora kwenye mgongo wake na kubandika picha hizi kwenye website ya hi5, kwa kweli inasikitisha sana, mambo yote ya kuchora hajayaona?





Soma Zaidi ...

JENERETA LAUWA WANNE WA FAMILIA MOJA ZANZIBAR

Watu wanne wa familia moja wamekufa baada ya jenereta lililokuwa limefungiwa ndani ya nyumba hiyo kupasuka na kuwaka moto.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamka leo, Kibwenzini Zanzibar wakati familia hiyo ikiwa bao imelala.

Wakizungumza kwa masikitiko baadhi ya majirani wamedai kuwa familia hiyo isingeteketea kwa maoto kama suala la umeme lingepatiwa ufumbuzi muda mrefu.

"Tumesikitishwa na vifo vya hawa ndugu zetu kwani kama Serikali ingelitafutia ufumbuzi suala la umeme muda mrefu wasingeteketea, " amesema jirani mmoja aliyejitambulisha kwa jina Yahyaa Juma Salehe mkazi wa Kibwenzini.

Amedai kuwa kutokana na kutokuwepo kwa umeme muda mrefu baadhi ya wakazi wenye uwezo wamenunua majenera ili kuweza kukabiliana na kero ya umeme.

Kutokana na hali hiyo kumekuwepo na kero ya kelele mitaani huku wamiliki wa majenereta hayo wakiweka ulinzi ili kuhakikisha kuwa hayaibiwi.

Amedai kuwa familia hiyo ilinunua jenera hiyo kutokana na kero hiyo ya umeme ambapo lilikuwa linafanyakazi likiwa ndani kila siku.

Amedai kuwa ilipofika sa 11 alfajiri wakati familia hiyo ikiwa bado wamelala moshi wa jenereta hilo ulijaa ndani ya nyumba hio ambayo milango na madirisha ya vioo ilikua imefungwa.

Amedai kuwa waliokufa katika ajali hiyo ni Safia Shaaban Shadadi (51), Ahmed Shaban Shadadi(48), Anwar Saleh (26) ambae alikua akiishi Canada, na msichana wa kazi nyumbani hapo
Sikudhani Nasorr.

Walionusurika katika ajali hio ni pamoja na mmiliki wa nyumba hio bwana Ali Shamsi Salum ambae siku ya tuki hakulala katika nyumba hio, Sharifa Ramadhan Mohammed (35) pamoja na mwanawe Nahad Ali Said (12) ambao walikimbizwa Hospitali ya Mnazi Mmoja kwa matibabu baada ya kupata mshtuko na kumeza hewa chafu iliyosababishwa na Jenereta hilo.

Naibu mkurugenzi huyo amesema chanzo cha vifo hivyo kimetokana na kukosa hewa katika nyumba waliyokuwa wamelala wakati huo generetar likiwa likifanya kazi na kusababisha moshi wake kushindwa kutoka nje na watu hao kuvuta hewa ambayo ni mchanganyiko wa sumu ya carbon mono. Soma Zaidi ...

MTOTO WA MIAKA 13 AONEKANA KAMA NI KIZEE WA 50+

Zara Hartshorn ni mtoto mwenye umri wa miaka 13 anaeishi Rotherham Nchini Uningereza, lakini kutokana na ugonjwa wa ngozi alionao ambao kitaalamu unajuilikana kama lipodystrophy umemfanya mtoto Zara aonekane kama ni bibi wa miaka zaidi ya 50.

Mtoto huyo amekua akipata shida wakati wa kupanda mabasi, kwani pindi anapotaka kukata tiketi ya mtoto madereva humkatalia kata kata na kumtaka akate tiketi ya mtu mzima na kumwambia kua yeye si mtoto.

Skuli pia imebidi asitishe kwenda kutokana na kukosa raha, kwani wanafunzi wenzake wamembadilisha jina na kumwita jina la utani "Bibi".

Ugonjwa alionao Zara ameurithi kutoka kwa mama yake bibi Tracey Pollard, bibi huyo kwa sasa ana umri wa miaka 40 lakini anaonekana kama ni bibi wa zaidi ya miaka 70 kutokana na ugonjwa huo wa lipodystrophy.

Lipodystrophy imewahi kuwatokea watu wapatao 2,000 duniani kote na hauna tiba, hivyo Zara ataendelea kusumbuliwa na ugonjwa huo kwa maisha yake yote sawa na mama yake.

Soma Zaidi ...

Tuesday, February 2, 2010

MAPACHA WA KISOMALI WAZUILIWA HOSPITALI

Mapacha walioungana ambao wazazi wao ni wakimbizi wa kisomali nchini Kenya wameshikiliwa katika hospitali ya Nairobi kwa miezi 16 baada ya kushindwa kulipia huduma za uzazi.
Mama wa mapacha hao wa kike, Anab Fahah Hussein, amemwambia mwandishi wa BBC kwamba familia yake inadaiwa zaidi ya dola za kimarekani elfu 30, na hospitali ya Kenyatta huku deni hilo likiongezeka kila leo.

Kundi la wasomali waishio Kenya wameanza kupokea michango ili kuwasaidia mapacha hao waweze kuondoka hospitalini.

Hospitali moja Marekani tayari imekubali kujaribu kuwatenganisha, lakini hawatoruhisiwa kusafiri mpaka walipe deni lao.

Soma Zaidi ...

MAPACHA WA KISOMALI WAZUILIWA HOSPITALI

Mapacha walioungana ambao wazazi wao ni wakimbizi wa kisomali nchini Kenya wameshikiliwa katika hospitali ya Nairobi kwa miezi 16 baada ya kushindwa kulipia huduma za uzazi.
Mama wa mapacha hao wa kike, Anab Fahah Hussein, amemwambia mwandishi wa BBC kwamba familia yake inadaiwa zaidi ya dola za kimarekani elfu 30, na hospitali ya Kenyatta huku deni hilo likiongezeka kila leo.

Kundi la wasomali waishio Kenya wameanza kupokea michango ili kuwasaidia mapacha hao waweze kuondoka hospitalini.

Hospitali moja Marekani tayari imekubali kujaribu kuwatenganisha, lakini hawatoruhisiwa kusafiri mpaka walipe deni lao.

Soma Zaidi ...

MR BEAN

MR. BEAN WHILE IN GRADE SCHOOL
Teacher: What is 5 plus 4?
Mr. Bean: 9
Teacher: What is 4 plus 5?
: Are you trying to fool me, you've just twisted the figure, the answer is 6!!

WHILE IN A DRUG STORE
Mr. Bean: I'd like some vitamins for my grandson.
Clerk: Sir, vitamin A, B or C?
: Any will do, my grandson doesn't know the alphabet yet!!

MR. BEAN ON MARRIAGE
Friend: How many women do you believe must a man marry?
Mr. Bean: 16
Friend: Why?
: Because the priest says 4 richer, 4 poorer, 4 better and 4worse.

CHATTING WITH HIS FRIEND
Friend: How was the tape you borrowed from me, Ok?
Mr. Bean: What do you mean Ok? I thought it was a horror film. I didn't see any picture.
Friend: What tape did you take anyway?
: Head Cleaner.

SPELLING LESSON
Mr. Bean's Son: Dad, what is the spelling of successful.. ..is it one c or two c?
: Make it three c to be sure!
Soma Zaidi ...

MTAFARUKU BENKI YA WATU WA ZANZIBAR TAWI LA PEMBA

Baadhi ya wateja wa Benki ya Watu wa Zanzibar Tawi la Chake Chake Pemba wakiwa katika taharuki ya kukimbizana baada ya “Fire Extinguisher” kupasuka ndani ya Benki hiyo na kudhania kuna mlipuko ama moto.

Baadhi ya wateja walikanyagana na kupata majeraha madogo madogo. Hata hivyo hali ilirejea na huduma zikaendelea kama.

Kawaida. Benki ya watu wa Zanzibar Chake imekuwa na wateja wingi sana hata wengine kushindwa kuwahudumia kwa wakati na ipasavyo kutokana na nafasi ya benki hiyo kuwa ni ndogo sana

” Kwa hakika tunahitaji jengo la benki lifanyiwe ukarabati kwa vile halitoshelezi isitoshe huduma ya ATM hakuna, Tupigieni kelele ndugu waandishi jambo hili lisikike kwa serikali hali ni mbaya sana” Alizungumza mmoja wa wateja wa Benki hiyo.

Mazingira ya Benki hiyo sio mazuri kwa majengo na kama inatokezea hatari kama ya moto inaweza kuleta hasara kubwa kwa binaadamu na mali zao ipo haja serikali kulitazama upya jengo hili na sio kulibadilisha rangi kila mwaka.
Soma Zaidi ...

HAPA KAZI IPO

Hii inaweza kutokea lakini ni Afrika tu, ndio maana rafiki yangu mrfroasty huwa anapenda kusema kwamba Afrika hata wakitengeneza gari basi watasahau kuweka wiper.
Soma Zaidi ...

ABIRIA CHUNGA MZIGO WAKO

Kuwa muangalifu na mzigo wako unapokwenda sehemu yoyote Duniani kwani mambo kama haya yanaweza kutokezea kwa upande wako

Soma Zaidi ...

TATIZO LA UMEME ZANZIBAR KUMALIZIKA HIVI KARIBUNI

Tatizo la ukosekanaji wa umeme Zanzibar linatarajiwa kumalizika ndani ya wiki tatu, kampuni ya umeme Zanzibar ilisema.

"Tunaendelea vizuri na kazi ya kurejesha umeme, kikosi cha mafundi kutoka Uingereza, Afrika Kusini, Zanzibar, na kampuni ya Ericson wamekua wakifanya kazi kwa bidii na tunatarajia umeme utarejea mnamo Febuari 20 mwaka huu, kaimu meneja ZECO" Bw. Hassan Mbarouk alisema.

Nae Ofisa Uhusiano wa ZECO alisema Bw. Salum Abdallah alisema kua Mafundi wanatarajiwa kuhamia Ras Kiromoni huko Dar-es-Salaam kwa ajili ya kwenda kufunga baadhi ya vifaa.

"Bado tunawaomba Wazanzibari kuwa wastahamilivu wakati tukiwa tunamalizia kazi hii.Tunatarajia Serikali itafanikiwa mpango wake wa kununua majenereta ya akiba" alisema.

Hata hivyo chanzo kutoka Wizara ya Maji Ujenzi Nishati na Ardhi kimesema Serikali ilitarajia kuingia mkataba na kampuni ya Katapila kwa kuleta majenereta yenye nguvu za megawatts 25.

Waziri kiongozi Mh. Shamsi Vuai Nahodha alisema wiki iliopita kwamba Serikali imeziomba nchi washirika wa maendeleo kusaidia ununuzi wa majenereta ya akiba ikiwa ni katika jitihada za kuleta umeme.

Wakati Wazanzibari wakikabiliwa na tatizo la maji na biashara kutokana na kukosekana umeme, ZECO imesema katika kipindi ambacho hakukuwa na umeme kisiwani humo, imepoteza Sh bilioni nne na Wizara ya Fedha na Uchumi imepoteza asilimia 30 ya mapato yake.

Tangu Desemba 10, mwaka huu kisiwa cha Unguja kimekosa umeme baada ya kifaa kimoja kilichopo katika kituo cha umeme cha Fumba kuharibika na kusababisha kutofanya kazi kwa waya wa kupitisha umeme wa chini ya bahari wa megawati 45 kutoka gridi ya Taifa kupitia Ras Kiromoni hadi Zanzibar.

Kwa mujibu wa Nahodha, Marekani kupitia Shirika lake la Millennium Challenge Corporation (MCC), imekubali kufadhili uwekaji wa waya huo wa megawati 100. Mradi huo utagharimu dola za Marekani zaidi ya milioni 63 ambapo tayari zabuni zimeshatangazwa na unatarajiwa kukamilika mwaka 2013.

Soma Zaidi ...

MIMI NI MMASAI BANA!!!!!

Mmasai huyu anaejuilikana kwa jina la Daniel Sakita mwenye umri wa miaka 20 yalimkuta hayo anayoonekana nayo katika picha baada ya kuamua kuchupa kutoka katika gari moja aina ya pick-up maeneo ya Silent Inn baada ya dereva wa gari hio kukataa kumshusha mmasai huyo hapo Silent Inn
Soma Zaidi ...

Monday, February 1, 2010

NDIO UMASIKINI AU DHARAU?


Hili ni darasa katika skuli ya msingi ya Mlumleni katika wilaya ya Mkuranga Mkoa wa pwani,
watu kila siku wamo katika safari sizizokwisha, ujenzi wa nyumba ya kuishi mtu mmoja tu na familia yake unagharibu shilingi Bilioni Moja huku wakiwaacha watoto walio wengi wakikosa sehemu za uhakika kwa ajili ya kupata elimu kitu ambacho ndicho kinadaiwa kuwa ni ufunguo wa maisha, hivi hii kweli hii ina hadhi ya kuitwa skuli?
Soma Zaidi ...

CCM YAADHIMISHA MIAKA 33 YA KUZALIWA KWAKE

Mh. Karume akikabidhi kadi za uwanachama kwa wanachama wapya wa CCM katika maadhimisho ya kutimiza miaka 33 ya kuzaliwa kwa hicho huko Bagamoyo jana. Hawa ni baadhi ya wanachama wa chama cha Mapinduzi CCM wakimsikiliza Makamo mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mh. Amani Karume katika sherehe za maadhimisho ya kutimiza miaka 33 ya kuzwaliwa kwa chama hicho yaliyofanyika jana huko Bagamoyo.Makamao mwenyekiti huyo ambae pia ni Rais wa Zanzibar alikua ndio mgeni Rasmin katika maadhimisho hayo.


Soma Zaidi ...

Sunday, January 31, 2010

WASHIKA BUNDUKI WASHINDWA KUTAMBA NYUMBANI KWAO DHIDI YA MASHETANI WEKUNDU

Timu ya soka ya Arsenal leo hii walishindwa kufurukuta mbele ya Man Utd katika uwanja wao wa Emirates Stadium kwa kuchukua kipigo cha magoli matatu kwa koja.

Man Utd waliandika bao la kwanza kupitia kwa winga wake wa kulia Nani baada ya kupiga krosi iliyomfanya mlinda mlango wa Arsenal Almunia kuukwamisha mpira nyavuni, bao la pili la Man Utd lilipachikwa nyavuniu na Rooney ambapo lile la tatu lilifungwa na Park.Goli la kufutia machozi kwa upande wa Arsenal limefungwa na Vermaelen.

Kwa matokeo hayo Man Utd bado wanaendelea kushikilia nafasi ya pili kwa kuwa na alama 53, na Arsenal wamebaki nafasi ya tatu kwa alama 49 huku usukani wa ligi hio bado unashikiliwa na Chelsea wakiwa na alama 54.

Kabla ya mechi hio kulikua na mechi kati ya Man City na Portmouth ambapo City walishinda 2-0

Kwa upande wa Kombe la mataifa Afrika limemalizika leo kwa mchezo wa fainali kati ya Ghana na Egypt na Egypt kuibuka kidedea kwa ushindi wa goli moja kwa zero na kuwafanya Egypt kuweza kutetea ubingwa wao. Soma Zaidi ...

NI BARAFU KWENDA MBELE

Hii barafu ya mara hii kwa kweli haitabiriki kwa sababu haishi
Soma Zaidi ...

MUHOGO - ZANZIBAR

Soma Zaidi ...