Watu wanne wa familia moja wamekufa baada ya jenereta lililokuwa limefungiwa ndani ya nyumba hiyo kupasuka na kuwaka moto.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamka leo, Kibwenzini Zanzibar wakati familia hiyo ikiwa bao imelala.
Wakizungumza kwa masikitiko baadhi ya majirani wamedai kuwa familia hiyo isingeteketea kwa maoto kama suala la umeme lingepatiwa ufumbuzi muda mrefu.
"Tumesikitishwa na vifo vya hawa ndugu zetu kwani kama Serikali ingelitafutia ufumbuzi suala la umeme muda mrefu wasingeteketea, " amesema jirani mmoja aliyejitambulisha kwa jina Yahyaa Juma Salehe mkazi wa Kibwenzini.
Amedai kuwa kutokana na kutokuwepo kwa umeme muda mrefu baadhi ya wakazi wenye uwezo wamenunua majenera ili kuweza kukabiliana na kero ya umeme.
Kutokana na hali hiyo kumekuwepo na kero ya kelele mitaani huku wamiliki wa majenereta hayo wakiweka ulinzi ili kuhakikisha kuwa hayaibiwi.
Amedai kuwa familia hiyo ilinunua jenera hiyo kutokana na kero hiyo ya umeme ambapo lilikuwa linafanyakazi likiwa ndani kila siku.
Amedai kuwa ilipofika sa 11 alfajiri wakati familia hiyo ikiwa bado wamelala moshi wa jenereta hilo ulijaa ndani ya nyumba hio ambayo milango na madirisha ya vioo ilikua imefungwa.
Amedai kuwa waliokufa katika ajali hiyo ni Safia Shaaban Shadadi (51), Ahmed Shaban Shadadi(48), Anwar Saleh (26) ambae alikua akiishi Canada, na msichana wa kazi nyumbani hapo
Sikudhani Nasorr.
Walionusurika katika ajali hio ni pamoja na mmiliki wa nyumba hio bwana Ali Shamsi Salum ambae siku ya tuki hakulala katika nyumba hio, Sharifa Ramadhan Mohammed (35) pamoja na mwanawe Nahad Ali Said (12) ambao walikimbizwa Hospitali ya Mnazi Mmoja kwa matibabu baada ya kupata mshtuko na kumeza hewa chafu iliyosababishwa na Jenereta hilo.
Naibu mkurugenzi huyo amesema chanzo cha vifo hivyo kimetokana na kukosa hewa katika nyumba waliyokuwa wamelala wakati huo generetar likiwa likifanya kazi na kusababisha moshi wake kushindwa kutoka nje na watu hao kuvuta hewa ambayo ni mchanganyiko wa sumu ya carbon mono.
No comments:
Post a Comment