Manchester Utd leo hii wameshika usukani wa ligi kuu Uingereza baada ya kuwafunga Potmouth kwa jumla ya magoli 5-0 katika mchezo uliofanyika uwanja wa Oldtrafford, kwa matokeo hayo Man Utd sasa wanakua na alama 56 wakati timu ya Chelsea ikishikilia nafasi ya pili kwa alama 55 lakini Chelsea wana nafasi kubwa bado ya kuongoza ligi hio ikiwa watashinda katika mechi yao ya kesho dhidi ya washika bunduki Arsenal, nao Arsenal wapo katika nafasi ya tatu kwa alama 49 huku walemavu Liverpool wamejikomboa na kufika katika nafasi ya nne baada ya kushinda mechi yao ya leo 1-0 dhidi ya Everton.
No comments:
Post a Comment