Majumba ya michenzani ambayo yalijengwa na Rais wa mwanzo wa Zanzibar Mh, Abeid Aman Karume, majumba kama haya yalijengwa sehemu tofauti ndani ya Zanzibar kama vile kikwajuni, kilimani, makunduchi, Gamba, (kama sijakosea jina) hii ni kwa upande wa Unguja na kwa upande wa Pemba ni Chake chake(madungu), Mkoani (mapinduzi), Wete(mtemani) na Micheweni, na pia Rais Mh, karume alijenga nyumba za vijiji ambazo zipo sehemu nyingi pia Unguja na Pemba.
Tukashuhudia tena mambo angalau mfano wa haya kwa Rais wa awamu ya tano Komandoo Dr, Salmin Amour juma ambae alijenga majumba ya Mchina, akajenga pia nyumba za kijiji ziliopo huko huko maeneo ya mombasa sokoni, na kumalizia jumba moja ambalo liliachwa tokea awamu ya kwanza jumba nama 9 upande wa madema.
Na awamu ya sita ikamalizia pia jumba nambari 10 ambalo lilijengwa kwa nguvu kubwa kutoka kwa vikosi vya SMZ.
Hapa ninahisi kama wananchi wangefaidika vizuri sana kama kila Rais angekua anafanya mambo kama aliofanya Mzee Karume na Dr Salmin lakini naona kila kukicha ni vurugu mechi tu hakuna moja la maana linalofanyika zaidi ya watu kuvunjiwa nyumba zao ambazo wanazijenga kimasikini masikini tena kwa muda wa miaka mingi eti kwa kisingizio cha kua wamejenga maeneo yasioruhusiwa sasa mimi najiuliza kama ni maeneo yasio ruhusiwa hivi Serikali ilikua wapi wakati wananchi wanaanza kujenga katika maeneo haya? lakini hili kwa leo naliacha kwa sababu sio pahali pake kulizungumzia.
No comments:
Post a Comment