Wednesday, November 4, 2009

ANGALIA JINSI EDWARD ALIVYOMZAMISHA ELIZABETH NA KUMUOKOA RAFIKI YAKE MZAMO

Kwa mara nyengine tena Mtanzania Elizabeth amewekwa kwenye kundi la watu wanaotazamiwa kutolewa katika jumba la Big Brother baada ya Mkuu wa jumba hilo wiki hii Edward kumuokoa rafiki yake Mzamo kwa kumbadikisha na Elizabeth,hivo ikiwa kama Elizabeth atakosa kura za kuweza kumbakisha ndani ya jumba hilo basi anaweza akapishana na kitita cha $2000,000 kwa kua siku ya jumapili atafukuzwa ndni ya jumba hilo.Kanuni za jumba la Big Brother ni kua mkuu wa jumba hilo wa wiki analazimika kumuokoa mtu mmoja ambae yupo hatarini kufukuzwa na kumuweka mwengine ambae anamtaka yeye na kama hakufanya hivyo basi yeye mwenyewe anakua ameshajiweka katika orodha ya kufuzwa.

No comments:

Post a Comment