Wednesday, June 30, 2010

BILAL ATUMIA MBINU ZA JK

Kinyang'anyiro cha kuwania uteuzi wa urais wa Zanzibar ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeingia katika hatua nyingine, baada ya kambi inayomuunga mkono Waziri Kiongozi wa zamani, Dk. Mohammed Gharib Bilal, kuanza kutumia mbinu za kusaka ushindi ambazo zilitumiwa na kundi la wanamtandao waliokuwa wakimuunga mkono Rais Jakaya Kikwete wakati wa harakati za kusaka urais wa Muungano mwaka 2005

Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima Jumatano umebaini kuwa moja ya mbinu hizo za kambi ya Bilal ni pamoja na ile ya kutishia kujitoa katika chama hicho iwapo jina lake litaondolewa katika kinyang’anyiro hicho kwa njia ya mizengwe, hasa katika vikao vya chama vitakavyofanyika Dodoma.

Habari kutoka kwa watu walio karibu na kambi hiyo ya Dk. Bilal, zinaeleza kwamba iwapo hilo litatokea, Dk. Bilal ataombwa kujiunga na Chama cha Jahazi Asilia na kugombea urais.

Kumbukumbu zinaonyesha kwamba mbinu hii ya kutishia kujitoa CCM ndiyo iliyotumiwa pia na vinara wa kundi la mtandao ambao miezi kadhaa kabla ya mchakato wa kusaka mgombea wa urais wa chama hicho walipenyeza taarifa ndani ya vyumba vya habari na katika taasisi nyeti za dola kuwa mgombea wao (Kikwete) alikuwa tayari kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo () iwapo angeenguliwa katika mchuano huo kwa njia ya mizengwe.

Habari ambazo zilipatikana wakati huo zinaeleza kuwa tishio hilo la kuwapo kwa taarifa za Kikwete kuwa tayari kujitoa CCM ndizo ambazo kwa kiwango kikubwa ziliwatisha viongozi wa juu wa chama hicho hata wakalazimika kuacha mchakato wa kumsaka mgombea urais ufanyike kwa uwazi, na baadaye Mwenyekiti wa chama hicho wakati huo, Benjamin Mkapa, akatoa hotuba za kulibeba kundi la mtandao.

Hoja nyingine ambayo inajengwa na kambi ya Dk. Bilal ambayo inafananishwa na ile iliyotumika kumbeba Kikwete mwaka 2005 ni ukweli kwamba yeye ndiye aliyestahili hasa kuwa mgombea urais mwaka 2000 baada ya kuibuka mshindi wa kura kwenye mchakato wa awali ulioanzia ndani ya kikao cha Kamati Maalumu ya CCM Zanzibar.

Katika mazingira ambayo hadi sasa Tanzania Daima Jumatano haijaweza kuyanyumbulisha, kumekuwa na taarifa zinazoonyesha kwamba miongoni mwa watu wanaomuunga mkono Dk. Bilal katika mchuano wa sasa ni makamanda wa juu waliokuwa wakiongoza mtandao wa Kikwete mwaka 2005.

Kikubwa ambacho kinaonekana kuwashangaza wengi ni kwamba hatua hiyo inakuja wakati kukiwa na ushahidi wa wazi kwamba mwaka 2000 makamanda hao wa mtandao ndio waliokuwa wapinzani wakubwa wa Dk. Bilal, na ndio maswahiba waliomsaidia chaguo lao, Amani Abeid Karume, kushinda.

Tofauti pekee ambayo inaonekana kuwa inaweza ikawa doa linalomtofautisha Bilal na Kikwete katika azima yao ya kusaka urais ni hatua ya Bilal kuamua kuchukua fomu mwaka 2005, wakati akijua kuwa Karume alikuwa ana fursa nyingine ya kikatiba kumalizia ngwe yake ya pili.

Wakati uamuzi huo wa Bilal kupambana na Rais Karume miaka mitano iliyopita kwa upande mmoja ulikuwa ukionekana kuwa ni wa mwanasiasa jasiri anayesimamia kile anachokiamini pasipo kumhofia yeyote, kwa upande wa pili umekuwa ukitajwa na wapinzani wake kuwa ni kielelezo cha mwanasiasa mwenye uchu wa hatari wa kusaka uongozi kwa gharama zozote.

Hata hivyo, habari za ndani za CCM zinasema hata Kikwete (wakati huo akisubiri kugombea) alitoa pendekezo ndani ya kamati kuu mwaka 2000 akitaka chama kiruhusu rais aliye madarakani (Mkapa) ashindanishwe na mwanachama mwingine, kwa maana ya kuimarisha demokrasia; jambo ambalo lilipingwa na uongozi wa chama.

Wapinzani wa Dk. Bilal wa kundi moja la wahafidhina wa CCM wamekuwa wakikifananisha kitendo hicho cha Dk. Bilal kuwa sawasawa na kile alichokionyesha Maalim Seif Sharif Hamad wakati alipokuwa mwanachama wa chama hicho, miaka ya 1980 alipojitokeza na kumpinga waziwazi aliyekuwa Rais wa Zanzibar wakati huo, marehemu, Abdul Wakil Nombe.

Kwa mujibu wa wahafidhina hao, kitendo hicho cha Bilal kuonyesha dhamira ya kuutaka urais kwa staili ile ile ya Maalim Seif kinamweka katika mazingira ya kumfanya akose sifa ya uvumilivu na ustahimilivu ambayo alikuwa nayo Kikwete wakati alipokubali kusubiri hadi Mkapa amalize ngwe yake ya miaka 10 mwaka 2005.

Hoja hizo za wahafidhina zinapingana vikali na zile za wapenzi wa Dk. Bilal ambao wanakiona kitendo chake cha kukubali kuondoa kwake jina mwaka 2005 kwa shinikizo na ushauri wa viongozi wengine wa juu wa CCM kuwa ni cha kistaarabu na kuungwa mkono.

“Hii ni mara ya tatu Dk. Bilal anawania nafasi hiyo, mara ya kwanza alienguliwa kwa mizengwe, mara ya pili aliondoa jina lake tena kwa maandishi, safari hii hakuna sababu ya kumzuia na ikitokea hivyo, ataondoka CCM na kujiunga na upinzani na anao watu wengi nyuma yake,” kilisema chanzo kimoja cha habari kilicho karibu na mwanasiasa huyo.

Katika hatua nyingine, mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere amemtaka Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) Shamsi Vuai Nahodha, kumtanguliza Mungu mbele katika harakati zake za kuwania kuteuliwa kuwa mgombea urais wa Zanzibar.

Mama Nyerere ameyasema hayo nyumbani kwake Msasani, jijini Dar es Salaam wakati wa mazungumzo kati yake na waziri huyo kiongozi, ambapo alitumia nafasi hiyo kumuasa mambo mbalimbali ambayo yatamsaidia kufanikikisha harakati zake hizo.

Alisema jambo kuu ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu katika kila jambo, hali itakayomfanya aweze kushinda vikwazo vitakavyomkabili katika kufanikisha lengo lake la kuteuliwa na CCM kuwa mgombea urais wa Zanzibar.

“Mimi na Mwalimu tulikuwa tukitamtanguliza sana Mungu katika kila jambo na ndiyo maana tumefanikiwa kuifanya Tanzania iwe na amani, nawe mwanangu mtangulize Mungu, hakika utafanikiwa,” alisisitiza mjane huyo wa Baba wa Taifa.

Naye Waziri Nahodha amesema ataweka mbele masilahi ya Mzanzibari na Mtanzania kwa ujumla, iwapo atapata nafasi ya kuwatumikia Wazanzibari katika nafasi ya urais.
. Soma Zaidi ...

UJERUMANI KUMPTA RAIS MPYA

Rais mpya wa Ujerumani anachaguliwa , leo na baraza maalumu la shirikisho lenye wajumbe 1244.

Atakaechaguliwa leo atachukua nafasi ya rais wa hapo awali, Horst Köhler, aliejiuzulu mwezi uliopita.

Wanagombea wadhifa huo ni waziri mkuu wa sasa wa jimbo la Lower Saxony, Chrsitian Wullf, na aliekuwa anasimamia idara kuu ya nyaraka za siri za idara ya ujasusi wa ndani ya Ujerumani Masharrikiya hapo awali, Bwana Joachim Gauck, mwenye umri wa miaka 70.

Waziri Mkuu Christiana Wullf ni mjumbe wa vyama vya serikali ya mseto na CDU na chama cha Waliberali, FDP. Vyama hivyo kwa pamoja na chama ndugu cha CSU vitawapeleka wajaumbe 644 yaani 21 zaidi ya wingi unaohitajika ili mjumbe wao ashinde .Juu ya hayo mgombea huyo amesema:

Mgombea mwingine, Joachim Gauck, ni mgombea anaeungwa mkono na vyama vya upinzani-SDP na chama cha kijani. Kwa pamoja vyama hivyo vitawapeleka wajumbe 462.

Lakini Gauck mwenyewe hayumo katika chama chochote .

Kwa hiyo, hesabu zinaonyesha kwamba mgombea wa vyama vya serikali anatarajiwa kupita katika kinyang'anyiro cha leo.

Wagombe hao ni watu wanaotofautiana kwa namna nyingi .

Kwanza kabisa mgombea wa vyama vinavyoongoza serikali, Christian Wullf, amekulia katika upande wa Magharibi wa Ujerumani. Mgombea wa vyama vya upinzani, Joachim Gauck, alikuwa mwanaharakati wa kupigania uhuru katika sehemu ambayo hapo zamani ilikuwa inaitwa Ujerumani ya mashariki.

."Tulikuwa Mashariki kwa sababu tulilazimishwa .Lakini katika fikira zetu tulikuwa na wazo la uhuru ambao haukuwapo katika upande wa Mashariki, lakini ulistawi katika Magharibi."

Joachim Gauck, asiyekuwa na chama chochote, hana matatizo na wahafidhina na Waliberali. Kwani angeliweza kuwa mgombea wa vyama vya serikali na vyama vya upinzani kadhalika.

Vyama vya upinzani vilimpendekeza Gauck. Kansela wa Ujerumani alipewa taarifa lakini alilikataa pendekezo hilo japo anamthamini sana Bwana Gauck.

Mgombe mwingine Christian Wullf aliependekezwa na vyama vinavyoingoza serikali . Christian Wullf alianza kuvuta pumzi ya uhuru tokea siku ya kwanza alipozaliwa katika Ujerumani magharibi.

Wullf mwenyewe anasema.

´´Muhimu ni kwamba natoka katika nasaba ya kati na nadhamiria kubakia katika nasaba hiyo. Kwangu ni jambo la kuvutia ikiwa rais atakaefuatia atakuwa mtu anaetoka katika rika la kati. Mtu mwenye uzoefu wa kuleta pamoja kazi na majukumu ya familia´´.

Christiana Wullf ana nafasi kubwa ya kuchaguliwa leo kuwa rais mpya wa shirikisho la jamhuri ya Ujerumani.

Amesema akichaguliwa ataendeleza sera za Horst Köhler, rais wa hapo awali alieliweka bara la afrika moyoni.

Köhler alizetembelea nchi kadhaa za Afrika kuhudhuria vikao na ushiriki katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Mwanasiasaa huyo amesema kwake ni wazi kabisa kwamba Ujerumani inapaswa kuuendeleza uhusiano na Afrika ulioanzishwa na rais wa hapo awali. Soma Zaidi ...

Tuesday, June 29, 2010

JAHAZI LAVAMIA BOTI DAR

Boti za mamlaka ya bandari zikifanya kazi ya uokoaji baada ya jahazi moja kugongana na boti ya Seagul baada ya kubadilika kwa upepo karibu na eneo la bandari ya Dar-es-salaam jana, watu wote waliokolewa wakiwa salama.
Soma Zaidi ...

DR SHEIN, NAHODHA WARUDISHA FOMU

Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohammed Shein na Waziri Kiongozi wa Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha, ni miongoni mwa wanachama waliorejesha fomu ya kuomba kuchaguliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa mgombea wa kiti cha urais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Wana CCM wengine waliorudisha fomu jana ni pamoja na Kamishna mstaafu wa Utamaduni, Hamadi Bakar Mshindo, Balozi Ali Karume na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mohamed Aboud.

Nahodha alirejesha fomu yake Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui baada ya kukamilisha kazi ya wanachama wa CCM waliomdhamini katika mikoa mitatu, mmoja kati ya hiyo ukiwa wa Pemba.

Baada ya kukamilisha kwa kazi hiyo, Mjumbe huyo wa Kamati Kuu na Hamashauri Kuu ya Taifa ya CCM, aliwashukuru wanachama waliomdhamini akiamini kuwa imani walioionesha kwao, bila shaka inampa matumaini mazuri katika safari yake.

“Ninawashukuru sana wanachama wenzangu wa CCM, tumekwenda Pemba na Unguja wamenipa ushirikiano mkubwa sana…Ninawahakikishia sitawaangusha,” alisema Nahodha (48) na kuongeza:

“Kama nilivyosema siku ya Jumatatu, sikuchukua fomu kwa kutania, nimejiandaa vya kutosha.”

Mapema wiki hii, Waziri Kiongozi alikuwa mtu wa kwanza kuchukua fomu ya kuwania urais wa Zanzibar, ambako katika mkutano wake na wanahabari alieleza masuala kadhaa ya kuinyanyua hali ya uchumi kwa wananchi.

Dk. Shein aliwashukuru wanachama wa CCM wa mikoa mitano ya Unguja na Pemba kwa kumdhamini bila ya matatizo katika maeneo mbalimbali aliyotembelea.

“Nawashukuru wanachama wa Chama Cha Mapinduzi walionidhamini katika mikoa yote mitano ya Unguja na Pemba....tupo katika mchakato na nikimaliza basi nitawashukuru wote wale,” alisema Dk. Shein ambaye kama Nahodha, ni Mjumbe wa Kamati Kuu pamoja na NEC.

Kazi ya urejeshaji wa fomu kwa wagombea mbalimbali wanaowania nafasi ya urais wa Zanzibar, iliratibiwa na Katibu wa Kamati Maalumu ya CCM Zanzibar, Idara ya Organizesheni, Asha Abdalla Juma.
.
Soma Zaidi ...

Monday, June 28, 2010

WAISLAMU WAMGEUKA KIKWETE

Baraza la Habari la Kiislam Tanzania (BAHAKITA) limewahamasisha Waislamu nchini kutokipigia kura Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi mkuu ujao kutokana na kuwadanganya kuhusu uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika Msikiti wa Kisumo ulioko Magomeni, Dar es Salaam, Katibu wa Baraza hilo, Sheikh Said Mwaipopo, alisema kutokana na CCM kuwafanyia utapeli wa kisiasa, watazunguka nchi nzima kuhakikisha CCM haichaguliwi katika uchaguzi wa mwaka huu.

“Huu ni utapeli wa kisiasa na ni unafiki na kwa mujibu wa dini yetu, Mtume anatuambia alama za mnafiki ni tatu: moja, akiahidi hatimizi; pili, akisema anasema uongo; na mwisho akiaminiwa haaminiki.

“Haya yote CCM wanayo na yamejionyesha, sisi kama Waislamu hatukuwatuma kuweka suala la Mahakama ya Kadhi ndani ya Ilani yao,” alisema Mwipopo.

Aidha, alisema kwa kushirikiana na baadhi ya wahadhiri wa Kiislaamu Julai 2 wanatarajia kufanya maandamano ya kulaani kitendo hicho cha CCM.

Alisema maandamano hayo yataanzia viwanja vya Mnazi Mmoja na kuishia kiwanja cha Kidongo Chekundu na baadaye kufanyika nchi mzima kwa lengo la kuwashawishi Waislamu kukikataa chama hicho.

Alisema wamelazimika kufikia hatua hiyo kutokana na kadhia iliyotokea iliyosababishwa na matamshi ya viongozi wa CCM akiwemo Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara, Pius Msekwa, Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe.

Katibu huyo alisema CCM imeshindwa kutekeleza ahadi zake kwa Waislamu, hivyo inaonyesha wazi kuwa chama hicho kiliwadanganya Waislamu kwa kuliweka suala hilo katika ilani ya uchaguzi wa mwaka 2005.

Alieleza kuwa Katiba ya nchi inaeleza kuwa serikali haina dini, lakini kwa sasa chama hiki kinaonyesha kinawachonganisha Watanzania na kurukia masuala ya dini katika kufanya kampeni za kisiasa.

Alisema suala la Mahakama ya Kadhi ni suala la Kikatiba, hivyo haihusiani na masuala ya kisiasa na kwamba mwaka 2005 CCM ilifanya utapeli, ili iweze kupita kwa kuahidi kuingiza Mahakama ya Kadhi.

Katibu huyo alisema kutokana na hilo wamejipanga na fedha wanazo, hivyo watazunguka nchi nzima kufanya mikutano ya hadhara na hata misikitini ili mradi wanachama wa CCM waliokuwa Waislamu wahakikishe kuwa wanarudisha kadi hizo na kujiunga na vyama vingine.

“Sisi hatujatumwa kisiasa lakini naamini kampeni zitakazofanyika hata kama wakikataza tutapambana kuhakikisha kuwa CCM inang’oka madarakani kwani si chama hicho tu kuna vyama vingine vingi ambavyo vinaweza kuwatimizia mahitaji yao Waislamu,” alisema Mwaipopo.

Naye Kiongozi wa Khid Mat Dawat Islamia, Alhaji Abubakar Kabunda kutoka Kanda ya Ziwa, alisema tangu awali walieleza kutokuwa na imani na Kamati ya Mufti Issa Shaaban Simba juu ya uanzishwaji wa mahakama hiyo.

“Tangu awali hatukuwa na imani nayo kwa kuwa hata suala hili limeondolewa kihuni na kwa dharau, lakini hakuna kiongozi yeyote wa BAKWATA aliyewahi kulizungumzia suala hilo; wote wamekuwa kimya kutokana na kufumbwa mdomo kwa kupewa ‘kitu kidogo’,” alisema Alhaji Kabunda.

. Soma Zaidi ...

NAHODHA, KARUME KURUDISHA FOMU LEO

Wanachama wanne wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliochukua fomu kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya urais Zanzibar, akiwemo Waziri Kiongozi, leo wanatarajiwa kurejesha fomu.

Katibu wa Kamati Maalumu ya NEC, Vuai Ali Vuai amesema, hadi sasa waliothibitisha kurudisha fomu hizo ni Hamad Bakari Mshindo (61), Ali Abeid Karume (60), Mohamed Aboud Mohamed (50) na Shamsi Vuai Nahodha (48).

“Wanachama hao watarudisha fomu saa 6 mchana (Mshindo), saa 9 alasiri (Karume), saa 10.30 jioni (Aboud) na saa 11 jioni atarejesha Nahodha,” amesema Vuai.

Naibu Waziri Kiongozi ambaye ni Waziri wa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Ali Juma Shamuhuna (66), amesema atarejesha fomu leo.

Kwa mujibu wa Vuai, kila mgombea ametakiwa fomu yake iwe na wadhamini 250 kutoka Zanzibar.

Baada ya kurejeshwa, fomu hizo zitapitiwa na Kamati Maalumu ya NEC Jumamosi na baadaye majina kuwasilishwa kwenye kikao cha Kamati Kuu cha Julai 6, mwaka huu kabla ya maamuzi ya mwisho ya kumteua mgombea mmoja yatakayofanywa na NEC mjini Dodoma Julai 9, mwaka huu.

Dk. Mohamed Gharib Bilal (65), ni mgombea wa kwanza kurejesha fomu, aliirejesha juzi. Hii ni mara ya tatu anagombea nafasi hiyo.

CCM imepanga kati ya Juni 23 na Julai mosi kwa wanachama wake kuchukua na kurejesha fomu kwa ajili ya kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya urais kwa Tanzania Zanzibar na Tanzania.
Soma Zaidi ...

Sunday, June 27, 2010

DR BILA: NITAPAMBANA

Awaambia Wazanzibari wakimtuma atatumika

Mgombea anayewania uteuzi wa kiti cha urais visiwani Zanzibar, Dk. Mohamed Gharib Bilal, amekuwa wa kwanza kurejesha fomu yake huku akisema kwamba safari hii atapambana hadi dakika ya mwisho.

Dk. Bilal ambaye ni mara yake ya tatu kuwania uteuzi wa kiti hicho kinachoshikiliwa na Rais Aman Abeid Karume, alirejesha fomu jana majira ya saa nne katika ofisi ya Makao Makuu ya CCM Kisiwandui kwa mbwembwe, huku akisindikizwa na umati mkubwa wa mashabiki wake.

Wakati akirejesha fomu, Dk. Bilal ambaye ni Waziri Kiongozi Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), aliongozana na wake zake wawili.

Alisindikizwa pia na baadhi ya wazee wenye ushawishi wa siasa za Zanzibar, huku wengine wakimsubiri kandokando ya barabara kutoka katika ofisi hizo za Makao Makuu ya CCM, hadi katika tawi la wakereketwa la Kisonge, eneo la Michenzani.

Pia alisindikizwa na vijana waliokuwa kwenye msafara wa pikipiki zilizopambwa kwa bendera za CCM pamoja na vikundi mbalimbali vya burudani.

Akizungumza na wafuasi hao wa CCM waliokuwa wamevalia sare za chama chao, Dk. Bilal alisema kuwa kazi waliyomtuma ya kuchukua fomu na kurejesha, ameimaliza na kuwataka mashabiki wake kuwa na subira.

“Ndugu zangu, nawashukuru kwa michango yenu ya fedha za kuchukulia fomu, kazi mliyonipa nimefanya vizuri, tusubiri taratibu zingine zitakazoendelea ndani ya chama Inshallaah Mwenyezi Mungu atatusaidia, Amen,” alisema Dk. Bila huku akishangiliwa na mashabiki wake.

“Napenda kuwaeleza kwamba sikupata shida ya kutafuta wadhamini na nawaomba wote mnaoniunga mkono, mzidi kuomba Mungu mchakato umalizike salama na tukibahatika tutakwenda NEC. Mmenisubiri kwa muda wa miaka kumi, tumebakiza siku chache, nawasihi muwe wavumilivu,” alisisitiza Dk. Bilal.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika nyumbani kwake Mazizini, alipoulizwa atachukua hatua gani endapo CCM haitamteua kuwania kiti hicho, Dk. Bilal alisema safari hii atahakikisha anapambana hadi dakika ya mwisho kwa kuwa ridhaa ya kugombea nafasi hiyo kwa mara ya tatu imetoka kwa wananchi.

Akijibu swali kwamba atakubali matokeo kama atashindwa kwa haki, Dk. Bilal alisema yuko tayari kukubaliana na matokeo ya aina yoyote ile kama atashindwa kwenye kura za maoni.

Alipoulizwa kama kuna ahadi yoyote alipewa wakati alipowania kiti hicho mwaka 2005 na baadaye kushinikizwa kuondoa jina lake ili kumpisha Rais Aman Abeid Karume, Dk. Bilal alisema hakuna ahadi iliyotolewa pamoja na kwamba alijitoa kwa maandishi.

Alisema mwaka 2005 alipogombea urais wa Zanzibar, baadhi ya wanachama wenzake walimwona kana kwamba amefanya dhambi kubwa wakati alikuwa sahihi.

“Sikutenda dhambi na hata jina langu lilivyopelekwa kwenye vikao vya juu vya chama, walinisihi sana niondoe jina, nami nilifanya hivyo kwa maandishi lakini hadi leo sijajibiwa hiyo barua yangu, madai kwamba chama kiliniahidi cheo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, hizo ni hisia tu za watu,” alisema Dk. Bilal.

Hata hivyo alipoulizwa ni mambo gani atayafanya endapo atapatiwa ridhaa ya kuwaongoza Wazanzibari, Dk. Bilal alisema anategemea kufanya mabadiliko makubwa na kutekeleza yatakayoachwa na kiongozi aliyetangulia kwa mujibu wa ilani ya chama chake.

Alisema Zanzibar haina msisimko katika masuala ya maendeleo na kukuza uchumi, endapo ataingia madarakani, alisema, atahakikisha anavibadilisha visiwa hivyo ili viweze kwenda sambamba na nchi nyingine ambazo zimo katika Jumuia ya Afrika Mashariki.

Baadhi ya wazee wa Zanzibar ambao wamepata kushika nyadhifa serikalini, Abdul Razak Mussa (Kwacha), Hamidi Amiri Ally na Ibrahim Aman Ibrahimu, walisema kwa nyakati tofauti kuwa ndiyo waliomtuma Dk. Bilal kuchukua fomu kwani safari hii, ndiyo chaguo lao.

Wazee hao walitaka viongozi wa juu wa CCM, kusikiliza matakwa na si kufanya maamuzi yao kama walivyozoea katika miaka mingine ya kipindi cha kumtafuta mgombea urais kwa tiketi hiyo.

“Vikao vya NEC vinatakiwa kujua kwamba mchujo wa kwanza tunao sisi wazee wa mkoa huu na si vinginevyo,” alisema Abdurazak Musa Simai maarufu kwa jina la Mzee Kwacha.

Mzee Kwacha ambaye aliwahi kushika nyadhifa tofauti za juu katika kipindi cha rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani Karume, alisema kwa kuwa walishawahi kumpigia kura mara mbili na kushinda katika nafasi hiyo, wanaviomba vikao vya juu vya CCM, safari hii vimpitishe kwani hawataki kuongozwa na mtu mwingine.

“Sijatumwa kuzungumza maneno haya na mtu yeyote…hii ni mara yangu ya kwanza kuzungumza maneno haya, hata nikiwa katika shughuli za chama na serikali…nasema Dk. Bilal sasa apewe nafasi ya kuongoza kwani wananchi ndiyo waliomchangia fedha za fomu,” alisema Mzee Kwacha.

Mbali ya Dk. Bilal, wengine waliochukua fomu kuwania kiti hicho Zanzibar ni pamoja na Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha, Balozi Ali Karume na Naibu Waziri Kiongozi, Ali Juma Shamhuna.

Wengine ni Makamu wa Rais wa Serikali ya Muungano, Dk. Ali Mohammed Shein, Hamad Bakari Mshindo na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mohamed Aboud Mohamed, Mfanyabiashara Mohamed Darammushi Raza, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amari, Harouna Ali Suleiman na Mohamed Yusuf Mshamba. Soma Zaidi ...

MJAMZITO AISHI KWENYE KALAVATI

Ama kweli duniani kuna mambo, kwani mwanamke raia wa Kenya, Saida Kimuna (39), ameweka makazi ndani ya kalavati la kupitisha majitaka katika barabara ya Boma, mjini hapa kutokana na sababu zisizofahamika, imegundulika.

Mwanamke huyo anayejitambulisha kutoka Kisii, Kenya, amegunduliwa na wananchi wa mtaa wa Liti Kilimo, akiwa ndani ya kalavati aliloligeuza makazi yake ya kulala usiku kwa muda mrefu sasa.

Akizungumza juzi katika eneo la makazi ya mwanamke huyo, Balozi wa Mtaa wa RDD, Samwel Mpeka, alisema baada ya kupata taarifa ya kuwapo mwanamke aliyeweka makazi ndani ya kalavati hilo, waliwasilisha taarifa Polisi.

Hata hivyo, alisema baada ya polisi kuarifiwa mkasa huo, walimchukua na kumpeleka hospitali ya mkoa ili kufanyiwa uchunguzi ikiwamo na kupimwa akili.

“Tuliwaarifu polisi juu ya jambo hilo na walimchukua na hadi hospitali ya mkoa…lakini baadaye mwezi mmoja uliopita, alirudi kuendelea kulala ndani ya kalavati hili,” alisema Mpeka.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Liti Kilimo, Bashir Mambo, alisema viongozi wa mtaa huo wameshindwa kufahamu kilichomrudisha mwanamke huyo hapo.

“Sisi hatujui kama ametoroka wodini … tumemwona tena akiishi ndani ya kalavati hili … jambo ambalo ni la hatari hasa wakati wa usiku,“ alisema Mambo.

Yeye alipohojiwa kuhusu maisha yake ndani ya kalavati hilo, alidai alifika mjini hapa siku nyingi akiwa na lengo la kumfuata shangazi yake, Mary Kiluo.

Hata hivyo, alisema: “Nimetoka Kisii, Kenya … nina wiki mbili sasa nalala ndani ya kalavati, kwa sababu sina ndugu,” alisema mwanamke huyo ambaye alionekana kuwa na ujauzito, naye alipoulizwa alikiri akisema: “ndiyo nina mtoto ndani”.

Kitendo cha mwanamke huyo kuishi hivyo, kuliwashangaza watu wengi walioshindwa kupata majibu sahihi iwapo Mkenya huyo ana matatizo ya akili au la.
. Soma Zaidi ...

WATU 16 WAKAMATWA SOMALILAND

Polisi katika jimbo lililojitenga la Somalia, Somaliland, wamewakamata watu 16 kwa madai ya kuhusika na vitendo vya kigaidi, huku raia katika jimbo hilo wakijitayarisha kupiga kura katika uchaguzi wa rais.

Kulingana na vyanzo vya habari maafisa wa usalama waliwakamata washukiwa hao wa kundi la Al-Shabab baada ya kufanya msako, katika hoteli mbili katika mji mkuu wa Somaliland, Hargeisa.

Maafisa wa usalama walihofia kuwa washukiwa hao walikuwa na nia ya kuvuruga uchaguzi huo,.

Rais wa sasa Dahir Rayale Kahin anayepigania muhula wa pili anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa kiongozi wa upinzani Ahmed Mahamoud Silanyo.

Uchaguzi huo wa rais unafanyika baada ya kuahirishwa mara tatu, tangu Aprili 2008. Somaliland ilijitangazia uhuru wake kutoka, Somalia mwaka wa 1991, wakati nchi hiyo ilipotumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Tangu hapo Somaliland imekuwa na utulivu, ingawa hakuna nchi yeyote inautambua uhuru wa Somaliland.
. Soma Zaidi ...

Saturday, June 26, 2010

MTOTO WA SALMIN AMOUR AAHIRISHA KUGOMBEA ZANZIBAR

Mtoto wa Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Salmin Amour aitwaye Amini, ametangaza kujiondoa kugombea nafasi ya uwakilishi katika jimbo la Magogoni, visiwani humo.

Kadhalika, Amini amemuomba Rais Jakaya Kikwete kuchukua tahadhari kubwa ikiwemo kuhakikisha mgombea wa nafasi ya urais visiwani Zanzibar anatokana na mapenzi ya Wazanzibar wenyewe na sio mizengwe ama utashi wa kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC).

Alitangaza hatua hiyo jijini Dar es Salaam katika mahojiano maalum na Nipashe ambapo alisema uwakilishi sio sehemu ya kujifunzia "bembea".

Alisema vijana wengi wamejitokeza kama utitiri kugombea nafasi hiyo huku wengi wao wakiwa hawajui historia ya Zanzibar na ya kwao wenyewe.

Salmin mwenye umri wa miaka 37 alitangaza nia ya kugombea nafasi hiyo ya uwakilishi mapema mwaka huu lakini amesema ameahirisha nia hiyo.

“Kwa sasa ninakwenda kusoma. Miaka mitano ijayo itanikuta nimesharudi, nitagombea inshallah,” alisema.

Aliliambia Nipashe kuwa wakati anatangaza nia ya kugombea, alishauriana na Baba yake, Dk. Salmin Amour ‘Komandoo’aliyekuwa Rais wa Zanzibar kati ya mwaka 1990 hadi 2000.

Alisema hata wakati wa kujiondoa pia alipata ushauri kutoka kwa watu wake wa karibu ambapo alikubaliana nao.

Kwa upande wa mchakato wa kugombea urais visiwani humo. Amini alimuomba Rais Kikwete na wajumbe wa NEC kuhakikisha wanawapatia Wazanzibar mtu wanayemtaka.

Alisema ingawa Zanzibar ina wajumbre 80 wanaoingia katika kikao cha NEC ambacho hufanyika mkoani Dodoma kwa ajili ya kupitisha jina la mgombea urais visiwani humo, lakini uchache wao usiwafanye Wazanzibar wachaguliwe mtu wasiomtaka.

Alikiri kwamba mwaka huu hali ya kisiasa Zanzibar, hususani ndani ya CCM ni ngumu kuliko watu wanavyofikiria na kwamba Rais Kikwete kama mwenyekiti wa chama tawala anatakiwa kutumia busara zake.

"Ili kuweka mambo vizuri ni lazima Wazanzibari wapatiwe mtu anayekubalika na wanachama wa CCM pamoja na wale wa vyama vingine vya upinzani," alisema.

Amini Salmin Amour alisema kama CCM kitatumia utaratibu wa zamani wa kumpitisha mgombea anayetakiwa na NEC watakuwa na wakati mgumu katika kumnadi kwa kuwa atakuwa sio chaguo la watu wa Zanzibar.

"Apitishwe mtu ambaye ana mvuto kwa CCM na upinzani… Wazanzibar wanamjua mgombea wao wanayemhitaji na wanachosubiria ni muda ufike ili wamchague," alisema.

Alisisitiza kwamba CCM visiwani humo hakina hamasa kama ilivyokuwa miaka ya nyuma kutokana na kuwepo kwa mpasuko, hatua ambayo alisema imesababisha wanachama wake kugawanyika na kusema kwamba tatizo lipo ngazi za juu.

Alikiri kuwa mwaka huu wagombea wa nafasi ya urais pamoja na ile ya uwakilishi wamekuwa wengi kupita kiasi tofauti na miaka mingine iliyopita.

Kuhusu vitendo vya rushwa alisema Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imefanya kazi nzuri lakini bado haijaweza kudhibiti hali hiyo.

Alidai bado wanachama na wajumbe wa NEC visiwani humo wanaendelea kufuatwa na kurubuniwa kwa kuahidiwa fedha ili wawaunge mkono baadhi ya wagombea. Soma Zaidi ...

DR BILAL AREJESHA FOMU ZA URAIS ZANZIBAR

Mfanyabiashara maarufu wa Zanzibar, Mohammed Raza, amesema ataacha kujishughulisha na biashara ikiwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitampitisha kuwania urais wa Zanzibar na kushinda kiti hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Wakati Raza akitangaza hivyo, mmoja wa waliochukua fomu za kuomba kuwania urais wa Zanzibar, Waziri Kiongozi mstaafu, Dk. Mohammed Gharib Bilal, amekuwa wa kwanza kukamilisha kazi ya kutafuta wadhamini na anatarajia kuziwasilisha leo saa 4:30 ofisi za CCM Kisiwandui.

Kwa upande wake, Raza aliyekabidhiwa fomu na Naibu Katibu Mwenezi wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai, alisema ataacha biashara ili kulinda misingi ya utawala bora, isiyotoa fursa kwa kiongozi kama Rais wa Zanzibar kujihusisha na biashara.

Pia Raza, alisema ikiwa atafanikiwa kuteuliwa na hatimaye kuwa Rais wa Zanzibar, ataunda Baraza la Mawaziri lenye watu waadilifu na wanaoheshimika katika jamii.

Raza alisema akipata nafasi hiyo, vipaumbele vya serikali yake vitakuwa ni kuleta mabadiliko katika maisha ya wananchi wa Zanzibar na kuboresha sekta za viwanda, uvuvi, ukusanyaji wa mapato na kuanzisha mfuko wa mikopo kwa wakulima.

“Maisha bora kwa kila Mzanzibari yanawezekana, tupo Wazanzibari milioni moja, lakini mazao Zanzibar yanaoza kutokana na tatizo la ukosefu wa masoko”, alisema Raza.

Raza aliusifu mfumo wa utoaji fomu za kuomba kuteuliwa kugombea urais kupitia CCM, kwamba hautoi nafasi kwa ukabila, ubaguzi wa rangi ama jinsia. Aliahidi pia kuwa ikiwa atachaguliwa, atawatumikia wananchi wa Zanzibar kwa kuendeleza misingi ya mapinduzi ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hata hivyo alisema ili kuwa na Muungano imara, kuna haja ya kero zinaoukabili zitatuliwe kwa muda mwafaka, ambapo kwa upande wake, alieleza umuhimu wa kuwashirikisha marais wastaafu katika mchakato wa utatuzi huo.

Naye mgombea wa nafasi hiyo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Haroun Ali Suleiman, alisema kwamba serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar ni msingi pekee wa kujenga umoja kwa wananchi wa Zanzibar.

Alisema iwapo CCM itampa ridhaa hiyo na hatimaye kuwa Rais, atahakikisha anafanikisha wazo lililoanzishwa na Rais Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, kuhusu kuunda serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Alieleza kwamba wananchi wa Zanzibar waondoe wasiwasi kuhusu uwezo wake katika masuala ya siasa na utawala, kwa vile ana uzoefu baada ya kushika nyadhifa mbalimbali ndani ya serikali ya CCM.

Aliahidi kulinda misingi ya Mapinduzi na Muungano, na kuweka kipambele kwa kuimarisha sekta za elimu, uvuvi, kilimo na viwanda ili kuongeza ajira na kipato kwa wananchi wa Zanzibar.

Kwa upande wake, mgombea mwingine wa nafasi hiyo, Mohammed Yussuf, alisema iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar, atayauza kwa mnada magari ya kifahari yanayotumiwa na mawaziri, ili kupunguza gharama za uendeshaji kwa serikali.

Alisema kutokana na mazingira ya kijografia ya Zanzibar, mawaziri na watendaji wakuu serikalini wanastahili kutumia gari aina ya RAV4.

Pia aliahidi kuimarisha Muungano wa Tanzania kwa kufanya marekebisho ya Katiba ili kuwa na Muungano wenye maslahi kwa pande zote.

Katika hatua ya Dk Bilal kurejesha fomu, waratibu wa kutafuta wadhamini wake walisema mgombea huyo, anatarajia kurejesha fomu ya kuwania nafasi hiyo leo saa 4:30 za asubuhi.

.
Soma Zaidi ...

Soma Zaidi ...

Friday, June 25, 2010

WIMBI LA UKURASA MPYA ZANZIBAR

Assalam Aleykum!

Zanzibar inapita kipindi cha Wimbi la Political Stress ambayo hutokea kwa Nadra kwenye Historia.Zanzibar inakabiliwa na Mtihani Mgumu katika kuleta Mabadiliko ya Jamii yake.

Matokeo ya Kura za Maoni hapo 31.07.2010 ndio matokeo ya Rais Mtarajiwa ZNZ. Katika safu ya wale wa mwanzo yaani Maalim Seif , Balozi Karume na dr. Shein amejitokeza Bwa. Nahodha mwenye kuleta matumaini kwa kizazi kipya . Kati ya hao wote Bw. Nahodha ndie kijana waleo tukumbuke kuwa 2/3 ya Wapiga Kura ni kati ya miaka 18 na 45 ambao hawajayaona mapinduzi ya Jan 12 licha kuona Uhuru wa Dec.10. Mambo yanaweza kugeuka kuelekea kizazi kipya . Jee ndo tuseme YES WE CAN !! ipo ZNZ .

Jengine ni hili la Kura za Maoni

Tumebakiza wiki sita tu tufikie Kura za Maoni kuhusu Serikali ya Mseto kati ya Vyama vyenye Uwakilishi Barazani. Hii ni Neema kubwa kwani kumalizika kuundwa huko kwa Serikali ya namna hio kutafuata yale ambayo Wa-ZNZ tunayatarajia yaani Maendeleo na Amani Nchini mwetu. Tutaepukana na Sarakasi zisizoisha!! Inshallah . Ijapokuwa kula Mseto ni hiari sio lazima lakini tukae tukijuwa Mseto ni mtamu ukiwa ule tuliouzoea au ule wa Kande!
Call it what you will , the Rose smells sweet!!!

Wale ambao wanaosema Ndio tunawategemea kuwa Wingi Sana kuliko wanaosema Hapana kwani Wa-ZNz wanaitakia Umoja na Amaan Nchi mwao!!.

Zanzibar Zindabaad!!


***AMUR
Soma Zaidi ...

HEKA HEKA ZA KOMBE LA DUNIA

Soma Zaidi ...

Thursday, June 24, 2010

MGOMBEA URAIS ZANZIBAR HADHARANI JULY 9

MGOMBEA urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, atajulikana Julai 9 mwaka huu mjini Dodoma, wakati Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama hicho, itakapokutana na kupiga kura kumpata mgombea huyo.

Kwa mujibu wa Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi ya NEC, John Chiligati, siku inayofuata mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM atapigiwa kura na Mkutano Mkuu na ndipo pia mgombea mwenza atajulikana.

Chiligati alisema hayo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari kutoa taarifa ya kikao cha siku moja cha kawaida cha NEC kilichokutana juzi kujadili masuala mbalimbali ukiwamo Mkutano Mkuu wa CCM utakaofanyika Julai 10 na 11, mwaka huu.

“Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa CCM utakaofanyika Julai 10 na 11 yanakwenda vizuri … mkutano huo ndio utakaopiga kura ya kuchagua mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Kama watajitokeza wagombea wengi, zitapigwa kura na kama atajitokeza mmoja, pia zitapigwa kura za Ndiyo na Hapana, ili litoke jina la mgombea urais,” alisema Chiligati na kuongeza:

“Halmashauri Kuu ya Taifa itakaa Julai tisa kuchagua mgombea urais wa Zanzibar na tutakwenda katika Mkutano Mkuu kuchagua mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hapa tutajua mgombea mwenza na CCM itakuwa na timu kamili.”

Hadi sasa, Rais Jakaya Kikwete ndiye aliyejitokeza kuwania urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, akielekea kuwa mgombea pekee wa kiti hicho kwa chama hicho ambacho kimepanga Julai mosi kuwa siku ya mwisho ya kuchukua na kurudisha fomu za kuwania kiti hicho.

Akizungumzia masuala mengine yaliyojadiliwa na NEC, Chiligati alisema walipokea malalamiko 163 kuhusu rafu zinazodaiwa kuchezwa katika majimbo mbalimbali wana-CCM waliotangaza nia pamoja na wabunge wa sasa.

Alisema malalamiko hayo yanashughulikiwa kwa ngazi mbalimbali yakiwamo 40 yaliyopelekwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa sababu yanahusu rushwa.

Aidha, Chiligati alisema kura za maoni kwa wanachama wa CCM wanaotaka kuwania ubunge katika majimbo zitafanyika Agosti mosi mwaka huu; takriban wiki mbili baada ya Bunge la Tisa kuvunjwa Julai 16, kupisha Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31 mwaka huu.

Alisema CCM imesogeza mbele uandikishaji wa wanachama na upokeaji wa wanachama wapya katika Daftari la Wanachama litakalotumika katika kupiga kura za maoni kuanzia Juni 30 hadi Julai 15 mwaka huu, baada ya watu wengi kujitokeza.

Mbali na hayo, CCM pia imebadilisha utaratibu wa mgawo wa viti maalumu vya ubunge katika mikoa ambapo sasa mikoa itakuwa na viti viwili kama ilivyo sasa, badala ya vitatu vilivyopangwa awali, kutokana na kuongezwa kwa mikoa mipya mitatu ya Simiyu, Geita na Njoluma.

Naye Amir Mhando anaripoti kutoka Zanzibar kwamba
mfanyabiashara maarufu mjini hapa, Mohammed Raza amechukua fomu ya kuwania urais wa Zanzibar kupitia CCM na kusema atahakikisha kila jimbo linapata zahanati kwa ajili ya wajawazito.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jana, Raza aliyepata kuwa Mshauri wa Michezo wa Rais wa Awamu ya Tano wa Zanzibar, Dk. Salmin Amour, alisema ataleta maendeleo na atasimamia pia umoja, mshikamano na kuwaunganisha Wazanzibari.

"Nikishapata nafasi ya kuwa Rais, nitaacha biashara zangu zote, maana siasa na biashara haziendani, pia katika Serikali yangu nitaweka wasaidizi waadilifu, nitasimamia utawala bora, nitahakikisha haki za binadamu zinafuatwa na maadili ya kazi yanakuwapo.

"Kutokana na ukereketwa wangu wa CCM nimezunguka majimbo yote 50 ya Unguja na Pemba, jambo nitakalolipa kipaumbele ni huduma za afya, nitaweka zahanati katika kila jimbo la Zanzibar.

"Pia kila jimbo nitaweka kituo cha kompyuta kwa ajili ya masuala ya kijamii, nitapanua wigo wa kutafutia soko wafanyabiashara wadogo, nasema maisha bora kwa kila Mzanzibari yanawezekana,
nitaweka sera maalumu kwa wafanyabiashara hao wapate mikopo," alisema Raza.

Aliwaomba wananchi wa Zanzibar kuhakikisha wanaheshimiana kwani malumbano hayawasaidii na kuongeza kuwa kwa imani yake hakuna mwana halali wa Zanzibar asiyetaka amani na mshikamano.

Alisema akipitishwa na CCM, akachaguliwa urais wa Zanzibar atashirikiana na viongozi wenzake kutatua kero za Muungano, alizoeleza kuwa zitamalizika kwa mazungumzo.

Alipoulizwa kwamba haoni kama CCM inaweza isimpitishe kwani ni miongoni mwa wagombea wasiopewa nafasi alijibu: "CCM ni chama makini, hakuna matabaka, wewe ukisema mimi ni Mhindi au Mwarabu sipitishwi si sahihi, sote ni Wazanzibari, tuache masuala ya matabaka."

Wanachama wanane wa CCM walikuwa wamechukua fomu kabla ya jana ili kuwania urais wa Zanzibar kupitia CCM; Makamu wa Rais Dk. Ali Mohammed Shein, Waziri Kiongozi Shamsi Vuai Nahodha, Balozi Ali Abeid Karume, Naibu Waziri Kiongozi na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Ali Juma Shamuhuna.

Wengine ni Kamishina mstaafu wa Utamaduni, ambaye amepata kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Hamadi Bakari Mshindo, Waziri Kiongozi mstaafu Dk. Mohammed Gharib Billal na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mohammed Aboud na Mbunge wa Chumbuni, Omari Sheha Mussa.

Wanachama wengine wawili licha ya Raza walitarajiwa kuchukua fomu jana ni Waziri wa Elimu Mafunzo ya Amali, Haroun Ali Suleiman na Mohammed Yusuph, ambaye haikuelezwa wadhifa wake.

Kulingana na taratibu zilizowekwa na CCM, wanachama hao wanatakiwa kutafuta wadhamini 250 katika angalau mikoa mitatu ya Zanzibar na kati ya hiyo, mmoja lazima uwe wa Pemba na mwisho wa kurudisha fomu ni Julai mosi mwaka huu. Soma Zaidi ...

Wednesday, June 23, 2010

MAMBO YA NONDO USWAZI


Soma Zaidi ...

BALAA LINALOSABABISHWA NA MAFUTA YANAYOMWAGIKA BAHARINI

Michelle Ridgway ni mtaalam wa elimu ya viumbe wa baharini na kawaida anakua akisomea mfumo wa ekolojia katika eneo la Alaska.Uchunguzi anaofanya ndio unaomuwezesha kutambua kwa jinsi gani mabadiliko ya hali ya hewa yanashawishi pia ukuaji wa viumbe tofauti vya baharini. Mtaalam huyo wa kimarekani anatafutwa sana hivi sasa ili aseme kama anaweza kupiga mbizi katika ghuba ya Mexico na kufanya uchunguzi.

Mtaalam huyo ameshawahi kutoa maelezo na data chungu nzima kuhusu maisha ya viumbe vya baharini na kitisho wanachokumbana nacho-tangu meli ya mafuta ya Exxon Valdez ilipovuja mwishoni mwa miaka ya 80 katika eneo la Prince-William Sund.

Kwa zaidi ya miaka 20 sasa Michelle Ridgway amekua akitumia mashua ndogo inayokwenda chini ya bahari katika eneo la Bering See huko Alaska.Mtaalam huyo wa biolojia ya viumbe vya baharini huingia ndani ya chombo kidogo na kupiga mbizi kina cha mita 100 chini ya bahari na kufanya uchunguzi wake.

Hufanya hivyo anapotaka kukusanya maelezo kuhusu kwa mfano athari zinazosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa baharini.

"Kuna mabadiliko ya hali ya hewa,hali hiyo inaonekana katika tabaka za juu za uso wa bahari kwa kuangalia jinsi mimea na viumbe vya baharini vinavyobadilika maji ya bahari yanapokua na ujoto.Na katika tabaka za chini kabisa za bahari kwenye hali ya ujoto, tunaona papa wengi,aina tofauti za papa katika Bering See."

Michelle anakuja na picha za kusisimua anazopiga katika maeneo hayo ya chini ya bahari na kuchapishwa pia katika jarida la National Geographic Magazine.Hivi sasa mtaalam huyo anaombwa akapige mbizi pia katika Ghuba ya Mexico.

Kwasababu miaka 21 iliyopita alikua wa mwanzo kufanya utafiti katika kina cha bahari meli ya mafuta ya Exxon Valdez ilipomwaga mafuta na kuchafua mazingira huko Prince William Sund katika eneo la Alaska.

Michelle Ridgway anasema:

"Wakati ule tangu idadi mpaka aina za mimea na viumbe vya baharini viliathirika.Na tunaamini hali kama hiyo inaweza pia kutokea katika Ghuba ya Mexico.Tunaelewa hofu na wasi wasi wa wakaazi wa eneo la Ghuba ya Mexico.Kile watakachojionea ni kuvurugika mfumo wa ekolojia kwa kipindi cha zaidi ya miaka kumi ijayo."

Hali kama hiyo imetokea pia Alaska.

"Maafa yana madhara ya muda mrefu,lakini katika mfumo wa ekolojia kuna baadhi ya viumbe na mimea ambayo ni sugu.Balaa lililosababishwa na mafuta yaliyomwagika limeathiri aina mbali mbali za mimea na viumbe ,lakini kwa daraja tofauti.Kuna aina fulani ya samaki wajulikanao kama heringi wameathirika vibaya zaidi.Samaki hao hawakurejea tena na hali kama hiyo inaisibu mimea na viumbe vyengine kadhaa."

Michelle Ridgway amefungua tovuti yake mwenyewe ambapo anakua anachapisha ripoti kuhusu utafiti anaofanya.Watu wengi wanapenda kufuatuilizia yaliyoandikwa na mtaalam huyo. Soma Zaidi ...

Monday, June 21, 2010

WALIOJITOKEZA KUCHUKUA FOMU ZA KUWANIA NAFASI YA URAISI KUPITIA CCM ZANZIBAR

Huku ikiwa kipindi cha uchaguzi mkuu kinakaribia viongozi kadhaa wamejitosa katika kuchukua fomu za kugombea nafasi ya Urais Zanzibar ambapo rais aliekuwepo madarakani kwa sasa Mh, Amani Karume anatarajiwa kumaliza muda wake wa uongozi.

Licha ya kua uchukuaji wa fomu hizo leo hii ulikua ni tofauti na watu walivyozoea, wagombea wengi hawakuingia kwa sherehe katika ofisi za CCM Kisiwandui lakini baadhi ya wapambe waliwasubiri wagombea wao na kuwasinidiza kwa magari wakati walipomaliza kukabidhiwa fomu hizo.

Wagomea waliochukua fomu leo hii alikua ni pamoja na Mohammed Aboud,Dr Ali Mohammed Shein,Balozi Ali Karume,Dr Mohammed Gharib Bilal,Shamsi Vuai Nahodha,Ali Juma Shamhuna,Hamad Bakari Mshindo.

Akizungumza katika mkutano wake na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuchukua fomu Naibu Waziri wa Afrika Mashariki, Mohammed Aboud amesema Zanzibar hivi sasa iko kwenye mazingira mazuri zaidi kuliko nyakati nyengine zozote katika historia yake ya kuendeleza malengo ya maridhiano hivyo kuna kila sababu ya hali hiyo kuendelezwa.

Aboud aliahidi kuandaa mazingira mazuri ya kiuchumi yatakayovutia wawekezaji wa sekta binafsi na kuwekeza kwenye kutoa huduma ya afya ili Zanzibar iwe kituo cha kutoa huduma hiyo ndani ya afrika mashariki.


Kwa upande wake makamu wa Rais Dk ali Mohammed Shein ameahidi kuwa tahakikisha kuwa wanzanzibari wanaishi kwa amani na kuendeleza utamaduni wao wa kuvumiliana na kusaidiana na kuondosha tofauti zilizopo ambazo hazileti picha nzuri katika maisha ya mwanadamu.

Nimeamua kuichukua chanagmoto hii ya kugombea nafasi hii ya uongozi kwa nia safi, thabiti na kwa moyo mkunjufu nikiwa na dhamira ya kweli ya kuwatumikia wazanzibari kama nilivyofanya huko nyuma nikiwa mtumishi wa SMZ na ambavyo nimekuwa nikiwatumikia hivi sasa nikiwa katika serikali ya Tanzania, huku nikiamini moyoni mwangu kuwa nimefanya uamuzi sahihi, kwa manufaa ya chama changu na ananchi wa zanzibar na Tanzania” amesema Dk Shein.

Dk Shein amesema ingawa mambo mengi yanasemwa lakini yeye hana roho ya ‘korosho’ kama inavyodaiwa wala si kiongozi wa kukata utepe na kuzinduwa miradi ya maendeleo tu bali ni mchapa kazi na viongozi wengi wanalifahamu hilo akiwemo rais Mkapa.

“Wapo wanaosema kwamba mimi kazi yangu kubwa ni kufunguwa miradi ya maendeleo kwa kukata utepe …si kweli hayo ni maneno tu ambayo lengo lake kubwa ni kunikatisha tamaa uwezo wangu mkubwa rais Kikwete hata rais Mstaafu Mkapa anajunifahamu katiak uwezo wangu”alisema.

Akizungumzia suala la kujiandikisha alisema kwamba hakujiandikisha kupiga kura Zanzibar kwa zaidi ya chaguzi mbili sasa lakini huko si kuvunja katiba wala sheria za uchaguzi na kumuondoshei sifa ya kuwa rais wa Zanzibar na kukataa suala la kuwa hauziki kwa wananchi.

“Wapo watu wanasema hivyo kuwa mimi sijajiandikisha kupiga kura Zanzibar…nimekutupa kwetu….si kweli mimi naongoza kwa kuwasaidia wananchi wa kwetu Mkanyageni…na wale ambao hawajuwi katiba wakasome..wasikurupuke tu” alisema huku akiwa na mkewe pembeni.

Akizungumza katika hilo balozi wa italia Ali Karume alisema pamoja na kuwa anaunga mkono maridhiano lakini suala la kura ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa ya ndio au hapana hawezi kutaja msimamo wake kwa kuwa kura ya maoni itategemea na wakati husika lakini pia alisistiza kuendeleza kilimo ambacho ndicho kitu muhimu kwa kuinua pato ya taifa.

“Zanzibar inaweza kupiga hatua kubwa ya maendeleo kama baadhi ya sekta zitapewa kipaumbele ikiwemo kilimo kama mnavyojua kilimo ni kitu muhimu sana cha kuweza kukuza uchumi na kuwapatia wananchi chakula lakini pia pato la taifa linainuka kwa kilimo pia” alisema balozi Karume.

Waziri kiongozi Mstaafu Dk Mohammed Gharib Bilal ambaye ni mtaalamu wa fizikia amehidi kusimamia suala zima la elimu na afya na amesema ingawa kisasi ni haki lakini amewatoa khofu wazanzibari endapo watampa ridhaa ya kuongoza, hatolipa umuhimu suala hilo, na kuahidi iwapo atapata nafasi ya uongozi ataendesha nchi kwa misingi ya utawala wa sheria huku akisisitiza suala la nidhamu katika utawala wake.

“Najua kisasi ni haki lakini mimi alipoingia rais Amani hajanifanyia kisasi chochote kwa hivyo wananchi wasiwe na khofu juu ya hilo sitalipiza kisasi” alisistiza Dk. Bilal

Aidha alisisitiza suala la kuimarisha Muungano uliopo na ksuema kwamba Tanzania ni mfano wan chi nyingi katika muungali wake hivyo ni vyema kuendelezwa na kero hizo zinazoitwa kero zinapaswa kurekebishwa.

“Muungano wetu ni imara pamoja na kuwepo kwa matatizo mbali mbali jambo la msingi ni kuyapatia ufumbuzi wake matatizo hayo kwa njia za kistaarabu kama inavyofanywa sasa” alisema Dk Bilal.

Dk Bilal alisema kwamba msimamo kuhusu kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa itategemea matokeo ya kura ya maoni itakayopigwa July 31 mwaka huu lakini kimsingi anakubaliana na hali ya amani iliyopo.

Kati ya wagombea wote Dk Bilal alikuja na umati mkubwa ukiwa na vionjo mbali mbali katika mkutano wake na waandishi wa habari na kabla ya hapo wazee wa mikoa mitano ya Unguja na Pemba walimkabidhi jumla ya shilingi milioni moja kama mchango wao uchukuaji fomu za kugombea urais wa Zanzibar.

fedha hizo zilikabidhiwa na Mzee Abdulrazak Simai Kwacha kwa niaba ya wazee wa mikoa mitano ya Unguja na Pemba.

Kamishna wa Elimu na Utamaduni, Hamad Bakari Mshindo alisema kwamba Zanzibar inahitaji mabadiliko makubwa katika sekta mbali mbali kwa ajili ya kuleta maendeleo ikiwemo elimu.

“Tunahitaji mabadiliko makubwa katika sekta za kiuchumi na elimu ili tupate maendeleo katika nchi yetu” alisema na kuahidi kwamba yupo taayri kushirikiana na wengine katika kuleta maendeleo.

Waziri kiongozi, Shamsi Vuai nahodha amesema msimamo wake katika kura ya maoni yeye binafsi anataka iwepo amani, lakini katika hilo ni vyema wazanzibari wakafanya maamuzi ya busara yenye kuendeleza umoja na mshikamano na akasema iwapo atapata ridhaa ya kuingia ikulu atateuwa watu kutoka pande zote za Zanzibar ili kuondosha malalamiko ya upande mmoja kutoshirikishwa katika serikali.

Waziri kiongozi huyo amesema cheo alichonacho kwa sasa ni sawa na bendera kufuata upepo au kondakta katika gari yenye dereva wake lakini anataka apewe ridhaa ya kuongoza ili aweze kuendesha gari mwenyewe.

Naibu waziri kiongozi Ali Juma Shamhuna alijisifia uadilifu wake katika chama chake na kusema kwamba yeye ni kiongozi muadilifu na safi na ameshafanya kazi na marais wote bila ya kukwaana kisiasa na yupo tayari kukubaliana na mbadiliko yatakayoheshimu misingi ya ilani ya CCM pamoja na utawala bora.

Shamuhuna alisema kwamba akichaguliwa kuwa rais wa Zanzibar atahakikisha analeta mabadiliko makubwa ya kisiasa na kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.

“Mimi naunga mkono maoni ya chama cha mapinduzi katika suala la serikali ya umoja wa kitaifa….mimi kura yangu ya ndio tu katika kura ya maoni July 31” alissisitiza Shamhuna.
Soma Zaidi ...

TIMU YA UFARANSA YAGOMEA MAZOEZI

Timu ya Ufaransa imegomea mazoezi, ikiwa ni kupinga hatua ya kurejeshwa nyumba kwa mshambuliaji nyota wa timu hiyo Nicolas Anelka.

Anelka alitimuliwa kutoka katika timu hiyo baada ya kumtolea lugha chafu kocha wake wakati wa mapumziko kwenye mechi kati yao na Mexico ambapo walifungwa mabao 2-0.

Mgomo huo umesababisha mkurugenzi wa timu hiyo ya Ufaransa Jean-Louis Valentin kujiuzulu.Ufaransa inawajibika kushinda mechi yao ya mwisho dhidi ya Afrika Kusini, na wakati huo ikitegemea, matokeo katika mechi kati ya Uruguay na Mexico, ili kufuzu kwa raundi ya pili.

Taarifa za kutokea kwa kadhia hiyo ziliripotiwa katika vyombo vya habari vya Ufaransa ambapo Rais wa nchi hiyo Nicolas Sarkozy amekosoa tabia ya Anelka pindi itakua ni kweli.

Wakati huo huo, Brazil jana ilikuwa timu ya pili kufuzu kwa duru ijayo baada ya kuifunga Ivory Coast mabao 3-1.

Muda mfupi ujayo Ureno itapambana na Korea Kaskazini, kabla ya Chile kucheza na Uswis na baadaye Uhispania itajaribu kufufua matumaini yake mbele ya Honduras Soma Zaidi ...

UNAIKUMBUKA HII?

Enzi hizo noti hii unapata mikate minne safi kabisa
Soma Zaidi ...

Friday, June 18, 2010

KUINGIA NYUMBANI

Katika mila nyingi za Waislamu utaona kumewekwa mbele "aibu" kuliko "halali" na "haramu" na hili ni moja katika mambo yanayotuletea matatizo.

Inataka tuwafundishe watoto wetu wa kike na wa kiume umuhimu wa kutofanya ya haramu na kutilia mkazo hapo badala ya kuvutia upande wa kutotenda ya aibu khasa iwapo hilo linaloonekana kuwa ni la aibu linapingana na maamrisho ya dini yetu.

Kwa mfano, ukimfundisha mtoto mpaka akaelewa kuwa kuzini ni madhambi na akainukia na kukhofu kutenda hilo, ni afadhali (kwa mara zisizohisabika) kuliko kumwambia kuwa ni "aibu." Kuna wasichana wengi ambao hudhibiti bikra zao mpaka wakishaolewa na baada ya hapo huwa mengine tena na sababu yake kubwa ni kukhofia ya aibu kuliko kutenda ya haramu.

Wanawake wengi Duniani, khasa katika nchi wanamoishi Waislamu wengi, wanadhulumiwa na kuteswa kwa namna za kiajabu kabisa. Moja ni hiyo ya kushona tupu zao; na kuna akhasi ya hayo. Katika nchi fulani wasichana hunyakuliwa usiku na kupekekwa kwa "manyakanga" ili kufyekwa tupu zao ili wasiwe na hamu yoyote ya kuingiliwa maishani mwao. Sasa kama huo si uqatili na uovu wa hali ya mwisho kabisa, basi ni kitu gani hicho?

Na yote haya yanatokana na huko kuona aibu iliyopelekea watoto wa kike kuzikwa wangali wahai, na siku ya Qiyama waliotenda hayo watakuja kuhojiwa kama tulivyoelezwa katika Qur-an Tukufu. Tuwafundishe zaidi watoto wetu wa kiume na wa kike kukhusu ya halali na haramu kuliko ya aibu kimila.

Kusherehekea hadharani kuwa mwanao wa kike amebikiriwa na mumewe ni kutangaza yasiyofaa kuelezwa licha kutangazwa ulimwenguni ili kila mmoja ayajue.

Kila la kheri,
Ibrahim Soma Zaidi ...

HATIMAE LAKERS WATETEA UBINGWA WAO "NBA"

Timu ya LA Lakers leo hii wamenyakua ubingwa wa NBA Basket ball baada ya kuwafunga Boston Celtics kwa jumla ya alama 83 kwa 79.


Mechi ya leo ilikua ni ya vuta nikuvute kwani tofauti na mechi sita zilizopita, hakukua na tofauti kubwa ya alama baina ya timu zote mbili.

Lakers leo hii wamejidhihirishia mbele ya Celtics kwamba wao ni mabingwa wa kikapu, kwani hadi robo ya tatu inamalizika Celtics walikua wanaongoza, lakini waliporudi uwanjani kumaliza robo ya nne hali ilianza kubadilika na hatimae kuibuka kidedea.

Ubingwa wa leo kwa Lakers utakua ni wa mara 16 nyuma ya Celtics ambao wamechukua kwa mara 17.

Mchezaji nyota wa NBA Kobe Bryant "The Black Mamba" kwa upande wake amefanikiwa kuchukua kombe hilo kwa mara ya 5 na hivyo kutangazwa kua MVP "most valuable player"

Katika mechi ya leo Kobe Bryant aliipatia timu yake ya Lakers jumla ya alama 23, ambapo wakati zilipokua zimebaki sekunde 90 mpira kumalizika Kobe aliiwezesha timu yake kuongoza kwenye kipindi cha pili kwa kuweza kupata alama kupitia "free throws".

LA Lakers watakua na furaha isio na kifani kwa kile kitendo cha kua nyuma kwa vipindi vya robo tatu kutokana na Celtics kua na Ulinzi wa hali ya juu lakini hatimae kuibuka kidedea katika robo ya mwisho.

Alipohojiwa baada ya mchezo Kobe alisema " tunapaswa kushinda na bahati sio inayonifanya mimi nifurahi, kinachonifanya mimi nifurahi ni Ushindi".
Kwa ushindi huu wa leo napenda kuwapa pole wapenzi wote wa Boston Celtics akiwemo Rafiki yangu Mwana a.k.a Chichi Heart akiwa maeneo ya Washington U.S.A.

Soma Zaidi ...

Thursday, June 17, 2010

ABIDAL AKISOMA QURAN NDANI YA NDEGE YA WACHEZAJI WA UFARANSA

Soma Zaidi ...

U.A.E DIRHAM BIASHARA INALIPA


Katika hili bango linaonesha kwamba pesa ya U.A.E unaweza kuinunua kwa bei ya chini kabisa ya sh 400 na kuiuza hapo hapo kwa bei ya chuu kabisa ya sh 3700, hii biashara ni babu kubwa.

Soma Zaidi ...

KOMBE LA DUNIA "LIMEKULA KWA WALALA HOI"

Taarifa toka BBC kufuatia uchunguzi ikiwa raia wa kawaida wanafaidika na mashindano ya kombe la dunia inaonesha kuwa waliofaidi hadi sasa ni shirikisho la mpira duniani (FIFA),pamoja na mabwanyenye.

1.Raia mmoja, Angela Ncube, mchuuzi wa barabarani amesema kuwa ukiritimba mkali wa biashara umedidimiza ndoto za wengi akiwemo wamiliki wa nyumba na wafanyabiashara. Ncube amesema kuwa alilazimishwa kuhama kutoka karibu na uwanja wa mpira huko Johannesburg alipojaribu kuuza pipi na bidhaa ndogo ndogo kwa mamilioni wanaoingia uwanjani.

2.Taarifa ya FIFA inasema haijawakwaza wachuuzi wenye biashara ndogo ila imewapa fursa wenye biashara za wastani waweze kunufaika ili kujenga nafasi za ajira, taarifa ambayo ni vigumu kukubalika ikiwa utachunguza hali halisi ya maisha ya wananchi wa kawaida.

3.Polisi na walinzi wamezingira viwanja vinavyotumiwa kwa mashindano haya, wakichunguza mihadarati inayoweza kusababisha ghasia. Wananyang'anywa chakula au kinywaji kisichotoka kwa makampuni yaliyosajiliwa na FIFA au mamlaka nyingine.

4.Umasikini wa kupindukia pamoja na ukosefu wa ajira unaokadiriwa kufikia asilimia 25 umesababisha mamia ya watu kumiminika mitaani wakijaribu kuuza bidhaa ili kukidhi maisha. Wengi wao wamekuwa wakiuza bendera, jezi na kofia zinazohusiana na Kombe la Dunia kwa raia wenzao lakini wamezuiliwa kuwasogelea wageni.

5.Ndani ya viwanja, bidhaa kama pombe ya wadhamini maalum Budweiser inaruhusiwa lakini pombe maarufu nchini humo inayotengenezwa na kiwanda cha pili kwa ukubwa duniani SAB Miller hairuhusiwi. Kampuni hiyo imefanikiwa kuuza bidhaa zake katika maeneo ya wazi ambako mkono wa FIFA haufiki.

6.Watalii wachache. Upungufu wa fedha. Afrika ya Kusini ilitarajia mamilioni ya watalii lakini ukweli wa mambo ni kwamba imepokea watu 370,000 au pungufu. Wengi wamehofia maisha yao, gharama kubwa na uhalifu. Wamiliki wa hoteli, migahawa na biashara zinazotegemea utalii imewabidi wapunguze matumaini ya kipato kikubwa walichotarajia.

7.Waimbaji wa nchi hiyo ambao ni maarufu kote duniani, walitarajia vibarua lakini wasanii kama Black Eyed Peas na Shakira ndiyo waliobahatika kwenye sherehe rasmi.

Kundi la wamiliki wa nyumba na mawakala wa biashara ya nyumba waliodhani watapandisha bei za kupanga nyumba wakati wa Kombe la Dunia wamejikuta katika majonzi makubwa na nyota ya jaha imekuwa janga. Soma Zaidi ...

AGOMBEA URAIS ZANZIBAR SASA WAPIGWA MKWARA

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, kimesema marufuku kwa wanachama wake watakaojitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi ya urais kusindikizwa kwa mbwembwe za maandamano na wafuasi wao.

Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho, Saleh Ramadhan Ferouz, alipokuwa akizungumza na Nipashe kuhusu matayarisho ya zoezi la utowaji wa fomu linarotarajiwa kuanza wiki ijayo.

Alisema matayarisho yote yamekamilika na fomu zitaanza kutolewa Jumatatu ijayo kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa.

Aidha alisema wagombea wote watakao jitokeza watatakiwa kutoa taarifa siku moja kabla ya kuchukua fomu ili waweze kuingizwa katika ratiba badala ya kwenda ghafla.

“Wagombea wote watakao jitokeza kuwania urais wa Zanzibar hawaruhusiwi kusindikizwa kwa maandamano wakati wa kuchukua fomu na kurejesha” alieleza.

Alisema wagombea wote wanatakiwa kwenda kimya kimya wakati wa kuchukua fomu na kurejesha na wale watakaosindikizwa kwa mbwembwe za maandamano watakuwa wanakwenda kinyume na maadili ya chama kwa sababu wakati wa kampeni haujafika.

***Nipashe Soma Zaidi ...

WABUNGE 3 WAACHIWA KWA DHAMANA KENYA

Wabunge wawili nchini Kenya na Waziri mmoja msaidizi waliokuwa wameshtakiwa kwa uchochezi nchini humo wameachiliwa kwa dhamana.

Waziri msaidizi wa barabara Wilfred Machage na Mbunge wa Mlima Elgon Fred Kaondi waliachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki mmoja, ilhali mbunge mwenzao wa Cherangany Joshua Kutuny akaachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki mbili pesa taslimu.

Mwanaharakati mwingine aliyeshtakiwa pamoja na wabunge hao, Christine Nyagitha pia aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki moja. Wote wanne walifikishwa leo asubuhi mbele ya Jaji wa Mahakama kuu, na walikanusha mashtaka dhidi yao.

Mahakama hiyo pia iliwaagiza wanasiasa hao wawe wanafika katika afisi za idara ya upelelezi, CID kila siku asubuhi saa tatu. Wabunge hao walishtakiwa kwa makosa ya kutoa vitisho vya kuwatimua watu kutoka katika ardhi zao, iwapo mswada wa katiba mpya utapitishwa. Kesi yao itasikizwa tena Juni 21 mwaka huu. Soma Zaidi ...

Wednesday, June 16, 2010

LAKERS WAIBUKA KIDEDEA "GAME 6" THE FINALS

Mechi ya 6 kati ya mechi 7 za fainali ya NBA kati ya Los Angeles Lakers na Boston Celtics imemalizika kwa Lekers kuibuka kidedea kwa kujipatia alama 89 dhidi ya 67 za Celtics.

Mechi ya leo ilikua ni vuta nikuvute kwenye robo ya kwanza lakini baada ya kuanza kwa robo ya pili timu ya Celtics walionekana kuzidiwa na kushindwa kufurukuta mbele ya wapinzani wao.

Ushindi wa leo kwa Lakers umewapa matumaini ya kuweza kuchukua ubingwa iwapo kama wataweza kushinda katika mechi ya saba ambayo pia wana matumaini nayo kwani mechi hio itachezwa katika uwanja wao wa nyumbani.

Kwa upande wake nyota wa timu ya lakers Kobe Bryant ikiwa kama watafanikiwa kunyakua taji hili la NBA basi itakua ni kwa mara ya tatu nje ya Shaquille O'neal na pia itakua ni kwa mara ya tano akiwa na timu hio ya LA Lakers.

Katika mechi ya leo Kobe Briant kama kawaida yake aliongoza kwa kupata alama nyingi kuliko mchezaji yoyote ambapo alipata alama 26 huku akifuatiwa na mchezaji wa Celtics Ray Allen ambae alipata alama 19.

Mechi sita za fainali za NBA "The Finals" hadi sasa zimekwisha chezwa ambapo matoke hadi sasa ni sare (3-3),na mechi ya saba na ya mwisho ya fainali hizi ambayo ndiyo itakayo amaua ni nani bingwa wa NBA 2010 inatarajiwa kuunguruma siku ya Alkhamis ya tarehe 17 mnamo saa 21:00 kwa Marekani ambapo itakua ni alfajiri ya kuamkia Ijumaa mnamo saa 03:00 (CET).
.
Soma Zaidi ...

Tuesday, June 15, 2010

Hali ya wasiwasi yawakabili Wakenya huku Onyancha akifikishwa mahakamani

Phillip Onyancha mwenye umri wa miaka 32, amefikishwa mahakamani hii leo kwa mauaji ya Anthony Njirua Muiruri. Polisi wanasema walimkamata jamaa huyo kwa kumteka nyara kijana huyo Muiruri, kwa kumfuatilia kupitia simu yake ya mkononi ambayo alikuwa akiitumia kuwashinikiza wazazi wake wamlipe fedha kabla kumuachilia.

Polisi pia wanasema Onyancha amekiri alimuua kijana huyo pamoja na watu wengine 18.

Akiwa mahakamani hii leo, Onyancha hakujibu mashitaka yanayomkabili kwa sababu hakuwa na wakili.

Habari za kutisha kuhusu jamaa huyo ambaye amejitokeza hadharani kukiri kwamba amekuwa akitekeleza mauaji ya kikatili, na kisha kunywa damu za watu hao, zinazidi kuzusha hofu kote nchini Kenya.

Sasa visa vya kupotea watu vimeanza kuhusishwa moja kwa moja na ukatili huo unaohofiwa umetekelezwa na wafuasi wa makundi yenye itikadi kali wanaotaka kumaliza kiu chao kwa kunywa damu ya wanadamu.
. Soma Zaidi ...

Polisi yaahidi $6,250 kwa atakayetoa habari za mripuko, Kenya

Polisi nchini Kenya imeahidi kutoa zawadi kwa mtu atakayetoa habari kuhusu shambulio la grinedi katika mkutano wa hadhara wa kisiasa iliyowauwa watu 6.

Kamishna wa Polisi, Mathew Iteere, amesema kwamba anatarajia kwamba kima cha Dola 6, 250 kitaharakisha uchunguzi kuhusu shambulio la Jumapili katika mkutano wa kuipinga rasimu ya katiba.

Waliohudhuria mkutano huo wa hadhara wanaipinga rasimu hiyo ya katiba kwa sababu itahalalisha kutoa mimba katika hali hatari ya ujauzito na itatambua mahakama za Kadhi. Kura kuhusu rasimu hiyo itapigwa Agosti nne.

Bw. Iteere pia alisema polisi ilimkamata naibu waziri wa serikali pamoja na wabunge wawili kwa kutoa hotuba za uchochezi walipokuwa wanafanya kampeni dhidi ya rasimu hiyo ya katiba. Mashirika yasiyo ya kiserikali yanasema hotuba za uchochezi zilichangia ghasia za baada ya uchaguzi mwaka wa 2007 na 2008 ambapo kiasi ya watu 1000 waliuawa.
.
Soma Zaidi ...

Monday, June 14, 2010

VUVUZELA ZAWAKERA WENGI 'SAUZI'

Kamati ya Maandalizi ya Ndani ya Fainali za Kombe la Dunia zilizoanza kutimua vumbi Juni 11 nchini hapa, imesema inafikiria uwezekano wa kupiga marufuku upulizaji wa Vuvuzela ndani ya viwanja kunakofanywa na mashabiki wa soka.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Danny Jordaan, hatua hiyo inaweza kuchukuliwa na kamati yake kutokana na malalamiko yanayotolewa na watangazaji na baadhi ya mashabiki wa nje ya Afrika Kusini.

Vuvuzela mfano wa filimbi ndefu kama tarumbeta, zimekuwa zikitumiwa na mashabiki wengi hasa wenyeji wa timu ya Bafana Bafana ambao hupuliza mfululizo kuanzia mwanzo hadi mwisho wa mechi kiasi cha kuwa kero.

Vuvuzela zilishawahi kupigiwa kelele hata kabla ya kuanza kwa fainali hizo, lakini Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), likajadili suala hilo na kutupilia mbali malalamiko hayo kwa hoja kuwa kelele hizo zingeongeza mvuto wa fainali hizo.

Akizungumza na Kipindi cha Michezo cha BBC juzi, Jordan alisema kama malalamiko hayo yatazidi, kamati yake itachukua hatua ya kupiga marufuku.

Mbali ya watangazaji na baadhi ya mashabiki kulalamikia kelele hizo, pia hata nahodha wa timu ya taifa ya Ufaransa, Patrice Evra, amelalamikia kero ya kelele za Vuvuzela ambazo kutokana na wingi wake, kelele zake zinafanana na mzizimo wa nyuki kwenye mzinga.

Kauli ya Evra imekuja baada mechi yao ya ufunguzi iliyopigwa Juni 11 dhidi ya Uruguay ambayo iliisha kwa sare ya bila kufunguna ikitanguliwa na mechi kati ya wenyeji Afrika Kusini na Mexico ambazo zilitoka sare ya bao 1-1.

Wanaopinga upigaji wa Vuvuzela, hawaishii kero ya uwanjani tu, bali kitendo cha mashabiki kupuliza vifaa hivyo hata usiku wa manane kiasi ambacho kinawafanya wakose hata usingizi.

“Ndani ya uwanja kunakuwa na mvumo wa ajabu, kiasi cha kukosa utulivu wakati wote wa mechi, heri mashabiki hao wangekuwa wakiimba nyimbo za kawaida kwa mdomo.” Soma Zaidi ...

CHAMA KINACHOTAKA KUJITENGA CHASHINDA UCHAGUZI BELGIUM

Chama kinachopigania kujitenga nchini Ubelgiji kimeshinda uchaguzi mkuu nchini humo.

Ushindi huo wa Chama hicho cha jamii ya waflemish cha N-VA katika uchaguzi uliofanyika mapema, kimeibua hofu kwamba huenda hali ya wasiwasi iliyotawala Ubelgiji, kwa miezi kadhaa itaendelea.

N-VA ambacho ni chama kinachopigania kujitenga kwa watu wanaozungumza lugha ya kiholanzi, kilipata ushindi mkubwa katika mkoa wa Kaskazini wa Flanders , ilhali chama cha Kisoshalisti kimepata ushindi katika mkoa wa Kusini wa Wallonia, eneo la wanaozungumza Kifaransa. Tofauti katika kugawana mamlaka baina ya mikoa hiyo miwili ndio ilikuwa sababu kuu ya kuanguka kwa serikali iliyopita ya mseto kabla ya muda wake kumalizika.

Vyama hivyo viwili vina misimamo tofauti ya kisera, lakini vinatarajiwa kuanza mazungumzo ya kuunda serikali ya muungano.
. Soma Zaidi ...

JE UMESHAISIKIA HII?


Soma Zaidi ...

LA LAKERS WALALA TENA FAINALI NBA

Mchezo wa fainali ya kumtafuta bingwa wa mpira wa kikapu nchini Marekani kati ya Boston Celtics na LA Lakers umechezwa leo ambapo LA Lakers walishindwa kufurukuta dhidi ya Boston Celtics ambao waliutumia vyema uwanja wao wa nyumbani kwa kuwashinda Lakers kwa vikapu 92 kwa 86.

Mechi iliyochezwa leo ni ya tano kati ya mechi saba za fainali zitakazochezwa,ambapo mechi hio ilionekana ikiwa ni ya upande mmoja zaidi wakati Celtics walionekana kuudhibiti Mchezo na kuutawala katika vipindi vyote vinne.

Ushindi wa leo wa Celtics ni wa pili mfululizo huku ukiwa unafanya jumla ya ushindi wa mechi tatu za Celtics dhidi ya mbili kwa Lakers
Nyota wa kikapu wa timu ya Lakers Kobe Bryant aliweza kuipatia timu yake jumla ya alama 38, ambapo nyota wa upande wa Celtics Paul Pierce aliipatia timu yake jumla ya alama 27.
Alipohojiwa baada ya mechi hio Nyota Pul Pierce alisema " ilikua ni mechi yetu kubwa kwa mwaka huu, na kwa sasa tuko katika nafasi nzuri ambapo tuna michezo miwili huko Los Angeles na tunahitaji kushinda mmoja".
Celtics sasa inakua ni timu ya mwanzo kushinda mechi mbili mfululizo katika mechi zaba za fainali za NBA, na ikiwa kama Lakers hawataweza kushinda mechi mbili zilizobaki katika uwanja wao wa nyumbani basi Celtics watakua ni mabingwa.

Mechi ya sita ya fainali hio itachezwa siku ya Jumanne tarehe 15 mnamo majira ya saa 03:00 (CET) huko Los Angeles

.
Soma Zaidi ...

Sunday, June 13, 2010

MASHAMBULIO YA MAGURUNETI MJINI BUJUMBURA

Watu sabaa wamejeruhiwa, maguruneti yaliporipuliwa jana usiku mjini Bujumbura na vituo kadhaa vya chama tawala kutiwa moto mikoani.
Msemaji wa polisi Pierre Chanel Ntarabaganyi anasema mashambulio hayo "yamelengwa kuuwa na yameandaliwa wakati mmoja".
Ni kitendo cha kutaka kufuja uchaguzi wa rais-amesisitiza msemaji huyo wa polisi.Afisa mmoja wa ngazi ya juu wa vikosi vya usalama,ambae hakutaka jina lake litajwe anautuhumu upande wa upinzani kuwa nyuma ya mashambulio hayo.
Msemaji wa Muungano wa kidemokrasi kwa ajili ya demokrasia,Léonard Nyangoma amesema upande wa upinzani hauhusiki hata kidogo na mashambulio hayo.Visa hivi vinatokea katika wakati ambapo hali ni tete nchini Burundi.
Upande wa upinzani unakosoa matokeo ya uchaguzi wa May 24 uliokipatia ushindi mkubwa chama tawala cha CDNN-FDD.Kampeni za uchaguzi wa rais zimeanza rasmi jana.Na uchaguzi utaitishwa June 28 mwaka huu.
.
Soma Zaidi ...

Friday, June 11, 2010

ALIYEZIDIWA FURAHA NA KUMKUMBATIA KAKA

Nagery Ally Kondo (21) mwanafunzi katika shule ya Green Acres na mkazi wa Sekenke, Kinondoni jijini Dar Es Salaam, aliyeingia kiwanjani wakati mechi kati ya Tanzania na Brazili ikiendelea siku ya Jumatatu, Juni 7, 2010 ameachiwa huru na Jeshi la Polisi na kesi imeachwa mikononi mwa ofisi za shirikisho la soka Tanzania (TFF).

Kijana huyo alifika katika studio za redio Clouds FM na kuhojiwa katika kipindi cha Power Breakfast jana, Juni 10, 2010 na Dina Marios anaandika hivi katika blogu yake "...wakati wanaenda uwanja wa taifa yeye na wenzake walikata tiketi ya Tsh 30,000 lakini kutokana na kutokuwa na watu Maaskari waliwaruhusu kukaa jukwaa la Tsh 80,000....mpira ulipokolea Washikaji zake walimuona jamaa anavua mkanda, saa, viatu akawaomba wamshikie simu na kuwaambia mie naenda hivyo kumkumbatia Kaka.


Wenzie walijua utani mara jamaa akaanza kukimbia akielekea uanjani na kwenda kumkumbatia Kaka. Na anasema wakati anaenda alikuwa anajua lazima yatampata makubwa lakini alishaamua potelea mbali Mzuka wa soka ushampanda liwalo na liwe.

Anasema hakupanga chochote toka anatoka nyumbani mzuka ulimpanda wakati anangalia soka hapo uanjani na akajikuta anatamani kwenda kumkumbatia Kaka na ndicho alichofanya." - Dina Marios.

Watu kadhaa wametoa hisia mchanganyiko kuhusiana na tukio hili. Baadhi wamesema kuwa kwa kuwa alikuwa na nia njema na kwa kuwa kitendo kama hiki hutokea kwingineko duniani, basi adhabu yake isiwe ya kutisha. Wapo waliohoji umakini wa askari katiak kazi yao kuhusiana na hili.


Vile vile wapo waliasa kuwa endapo kijana huyu angekuwa ameficha silaha na kumdhuru yeyote kiwanjani, ingechafua kabisa nchi ya Tanzania na hili laweza kutokea kwani mtu anaweza kuficha silaha popote na kuitumia haraka.


Soma Zaidi ...

MAHAKAMA NCHINI FINLAND YAMUHUKUMU KIFUNGO CHA MAISHA MCHUNGAJI WA RWANDA

Mahakama nchini Finnland imemhukumu kifungo cha maisha gerezani mchungaji Francois Bazaramba wa Rwanda.
Mahakama hiyo ya wilaya imemtia hatiani mchungaji Bazaramba kwa kushiriki katika mauaji ya kimbari yaliyotokea katika nchi yake aliyozaliwa mwaka 1994.

Katika hukumu yake, mahakama hiyo imesema hatua ya mchungaji huyo wa zamani inaonesha dhamira yake ya kuliteketeza kabila la Watutsi ama sehemu ya kabila hilo.

Televisheni za Finnland zimeripoti kwamba Bazaramba anapanga kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

Polisi nchini Finnland walimkamata mchungaji huyo April mwaka 2007 kwa tuhuma za kushiriki katika mauaji hayo ambayo watu laki nane waliuawa.
Soma Zaidi ...

MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA KUANZA LEO AFRIKA KUSINI

Nchini Afrika kusini hii leo Ijumaa tarehe 11.06.10 yanafunguliwa rasmi kwa mara ya kwanza katika ardhi ya bara la Afrika mashindano ya fainali za kombe la dunia la kandanda.


Firimbi ya kuanzisha mashindano hayo itakapolia jioni hii wenyeji wa mashindano hayo Afrika Kusini watapambana na Mexico katika mchezo wa kwanza. Hali hii ya kufurahia mashindano haya makubwa ilikuwa na shaka wakati wote wa maandalizi, iwapo Afrika Kusini ilikuwa tayari kwa ajili ya changamoto ya mashindano makubwa kama haya.

Afrika kusini ilianza rasmi sherehe hizi za kombe la dunia jana Alhamis kwa shamrashamra za burudani ya muziki iliyosheheni wanamuziki nyota kutoka sehemu mbali mbali duniani, ikiwa ni pamoja na Shakira, na kundi linaloungurumisha muziki wa Afropop kutoka nchini Afrika Kusini wakifunga tamasha hilo kwa wimbo rasmi wa fainali hizo, Waka Waka.

Kitongoji cha Soweto, eneo ambalo litafanyika mchezo wa ufungizi wa fainali hizi, lilikuwa katika hali ya sherehe kubwa jana kwa tamasha la muziki. Shakira mzaliwa wa Colombia, mwimbaji wa muziki wa rap K'naan mzaliwa wa Somalia na mwimbaji wa muziki wa soul, Alicia Keys, walitia fora.


Afrika Kusini inafurahia muziki, Afrika kusini ni poa, amesema hayo rais wa Afrika kusini Jacob Zuma alipowahutubia mashabiki 34,000 waliohudhuria burudani hiyo katika mkesha wa ufunguzi wa mashindano ya fainali za kombe la dunia.

Waziri wa utalii wa Afrika kusini Marthinus van Schalkwyk alikuwa na haya ya kusema, "Zitakuwa fainali adimu za kombe la dunia la FIFA mwezi huu wa Juni na Julai. Lakini pia itakuwa juu ya kupata uzoefu wa kipekee kuhusu Afrika."

Bafana Bafana timu ya taifa ya Afrika Kusini inapambana na Mexico katika pambano la ufunguzi katika uwanja wa Soccer City katika kitongoji cha Soweto wakati Ufaransa ikiwa na miadi na Uruguay baada ya pambano hilo la ufunguzi.

Rais Jacob Zuma ana matumaini ya kumkabidhi kombe nahodha wa Afrika Kusini Aaron Mokoena hapo Julai 11, lakini wengi wa mashabiki wa Afrika Kusini wanaamini kuvuka duru ya kwanza litakuwa jambo jema kabisa.

Didier Drogba amerejea katika mazoezi kiasi siku chache baada ya kufanyiwa upasuaji katika mkono wake uliovunjika na huenda akafikiriwa kushiriki katika mchezo wa kwanza wa Ivory Coast dhidi ya Ureno.

Mabingwa wa Ulaya Hispania wameondoka jana Alhamis kuelekea nchini Afrika Kusini wakiwa hawataki kujitutumua kuwa wanapigiwa upatu kushinda kombe hilo la dunia.

Ujerumani ikiwa ni moja ya timu zinazofikiriwa kuwa huenda zikanyakua kombe hilo pamoja na Hispania na Brazil iko tayari kwa fainali hizo anasema kocha wa timu hiyo Joachim Löw.

Sisi kama Wajerumani tumo miongoni mwa wale wanaopigiwa upatu kulinyakua kombe hili, bila shaka. Na tunataka kulinyakua.

Masuala ya kifamilia pia yanahusika katika fainali hizi za kombe la dunia 2010 wakati Slovakia na Marekani zina makocha ambao katika timu zao kuna watoto wao. Mataifa matatu yana ndugu wanaocheza katika timu hizo na ndugu wawili watapambana katika timu tofauti. Kocha Vladimir Weiss katika kikosi chake yumo mwanawe anayekwenda kwa jina la Vladimir Weiss pia ambaye huchezea klabu ya Manchester City.

Kikosi cha Marekani, US Boys kikiongozwa na kocha Bob Bradley kinamjumuisha pia mtoto wa kocha huyo Michael Bradley anayecheza soka katika kilabu cha Borussia Moenchengladbach nchini Ujerumani.

Prince Boateng.......................Jarome Boateng

Lakini kazi itakuwa kwa ndugu wawili wa baba mmoja lakini mama mbali mbali Jerome Boateng wa Ujerumani na Kevin Prince Boateng atakayekuwa akitetea nchi alikozaliwa baba yake Ghana. Wote ni wa baba mmoja lakini mama tofauti wa Kijerumani.

Kevin Prince atakayechezea Ghana mjomba wake ni Helmut Rahn, ambaye alifunga goli la ushindi kwa Ujerumani katika fainali ya kombe la dunia mwaka 1954. Mbali na historia ya mashindano haya kufanyika katika bara la Afrika, kuna historia nyingi zitakazoandikwa katika fainali hizi 2010 nchini Afrika Kusini
Soma Zaidi ...

Thursday, June 10, 2010

BAJEI YA SMZ HAKUNA KODI MPYA


Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imewasilisha bajeti yake ya mwaka wa fedha wa 2010/11 bila kupandisha kodi kwa lengo la kuwapunguzia ukali wa maisha wananchi wake.

Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi katika kikao cha Baraza la Wawakilishi jana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Fedha na Uchumi), Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini, alisema serikali imechukua hatua hizo ili kupunguza mfumuko wa bei katika soko la ndani.

Dk. Mwadini alisema bajeti ya mwaka huu imeathiriwa na nakisi kwa Sh. milioni 6,000, lakini alisema pengo hilo litazibwa na mikopo ya ndani kupitia hati fungate.

Alisema kuwa serikali inatarajia kutumia Sh. bilioni 444.637 katika mwaka wa fedha 2010/11 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na utekelezaji mpango wa maendeleo.

Alisema kati ya fedha hizo, Sh. bilioni 193.433 zitatumika kwa kazi za kawaida wakati Sh. bilioni 251.204 zitatumika kwa utekelezaji wa mpango wa maendeleo na Sh. bilioni 82.459 kwa malipo ya mishahara ya watumishi wake.

Waziri Mwadini alisema pato la taifa limeongezeka hadi kufikia Sh. milioni 878.403 kutoka Sh. milioni 748.057 mwaka 2008 sawa na ongezeko la asilimia 17.4.

Alilieleza Baraza la Wawakilishi kwamba uchumi wa Zanzibar umekuwa umeongezeka kwa asilimia 6.7 kutoka asilimia 5.3 kutokana na mageuzi katika sekta ya kilimo pamoja na kuongezeka kwa idadi ya watalii.

Alisema pato la mtu wa kawaida pia limeongezeka kutoka Dola za Marekani milioni 557 hadi 728.364 mwaka 2008 sawa na ongezeko la asilimia 4.3 na kuwataka wananchi kuendelea kudumisha hali ya amani na utulivu wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu.

Hata hivyo, alisema mfumuko wa bei katika soko la ndani la Zanzibar umeongezeka kutoka asilimia 5.1 mwaka 2000 hadi asilimia 9.7 mwaka huu, lakini alisema mwaka 2008 mfumuko wa bei ulikuwa mkubwa baada ya kufikia asilimia 20.6 na kuathiri wananchi wake.

Waziri Mwadini alisema kwamba tayari Serikali imeshaanza kupitia upya muundo wa watumishi wa umma ili iweze kuboresha maslahi yao kwa lengo la kuwapunguzia ukali wa maisha.

“Maslahi ya wafanyakazi yatashughulikiwa vizuri zaidi baada ya kukamilika mapitio ya muundo wa watumishi wa umma,” alisema Waziri huyo.

Watumishi wa umma wamekuwa wakilipwa mshahara wa Sh.100,000 viwango ambavyo vimekuwa vikilalamikiwa na wafanyakazi pamoja na vyama vya wafanyakazi Zanzibar.

Alisema katika mwaka ujao wa fedha, Serikali inatarajia kukusanya Sh. milioni 171,687 kutoka vyanzo vya mapato ya ndani sawa na asilimia 17.9 ya pato la taifa.

Hata hivyo, alisema kwamba katika bajeti hiyo Sh. bilioni 266.950 zinatarajiwa kutoka kwa wafadhili kupitia misaada ya kibajeti kwa ajili ya utekelezaji programu na miradi ya maendeleo katika mwaka wa fedha ujao.

Waziri Mwadini alisema kutokana na wahisani kupunguza misaada ya kibajeti katika mwaka huu wa fedha, bajeti ya Zanzibar itaathiriwa na upungufu wa Sh. bilioni 18, lakini serikali imeshaanza kuchukua hatua mbali mbali kuziba pengo hilo kupitia mikopo.

Aidha alisema kwamba serikali inatarajia kuanzisha Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo ili kuharakisha maendeleo katika majimbo 50 ya Zanzibar.

Alisema kwamba serikali inatarajia kuwasilisha muswaada wa sheria wa kuanzisha mfuko huo mwaka huu kama ilivyo kwa serikali ya Muungano ambayo imeshaanza kutoa fedha za maendeleo ya jimbo kwa wabunge wa Tanzania Bara na Zanzibar.
***Nipashe
Soma Zaidi ...

VYAMA VYA UPINZANI VYAIBUKA NA USHINDI NCHINI UHOLANZI

Matokeo ya uchaguzi wa bunge nchini Uholanzi hayakutoa ushindi kamili kwa chama chochote lakini yanaonyesha kuwa wapigakura nchini humo wameamua kubadilisha serikali.

Chama cha Christian Democratic Action cha waziri mkuu anayeondoka madarakani Jan Peter Balkenende kimepata pigo katika uchaguzi huo, kikipoteza nusu ya viti vyake bungeni. Kutokana na hali hiyo, Balkenende ametangaza kujiuzulu kama kiongozi wa chama hicho, na kuacha kiti chake bungeni.

Chama cha mrengo wa kati kulia cha Kiliberali na kile cha mrengo wa shoto kati cha Labour vimefungana kwa kupata viti 31 kila kimoja kutoka viti 150, wakati chama kinachopinga wahamiaji kimekuwa cha tatu kwa kupata viti 22.

Chama cha Christian Democratic kimeshika nafasi ya nne. Chama cha Kiliberali kilitarajiwa kushinda kutokana na uchunguzi wa maoni ya wapiga kura kabla ya uchaguzi. Soma Zaidi ...

Wednesday, June 9, 2010

MAHOJIANO:IDHAA YA KISWAHILI BBC NA BALOZI MWANAIDI SINARE MAAJAR


Mahojiano kati ya Zuhura Yunus wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC na Balozi Mwanaidi Sinare Maajar. Balozi Maajar yuko mbioni kuelekea Washington atakakokuwa balozi mpya wa Tanzania baada ya kufanya kazi hiyo nchini Uingereza kwa takriban miaka minne. Anazungumzia changamoto na mafanikio yake. ANGALIA HAPA
Soma Zaidi ...

Monday, June 7, 2010

SEIF AWAONYA WANAOPINGA MARIDHIANO YA KISIASA ZANZIBAR

Katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF Seif Sharif Hamad amesema anashangazwa kuona baadhi ya wazanzibari wanakula njama za kuwatenganisha wananchi baada ya kufikiwa maridhiano ya kisiasa.

Akizungumza katika sherehe fupi ya kurejesha fomu ya kugombea nafasi ya urais wa Zanzibar kupitia CUF amesema watu hao wanajaribu kuyabeza mafanikio ya maridhiano na kusema lengo lao ni kutaka Wazanzibari wahasimiane ili kulinda maslahi yao binafsi.

Hamad amesema mataifa ya nchi wahisani yamepongeza hatua iliyofikiwa na Zanzibar ya kufungua ukurasa mpya wa melewano ambapo nchi hizo zimeahidi kutoa misaada yao na kuwaonya wanaojaribu kuhujumu maridhiano hayo …

Aidha katibu mkuu huyo amewataka wananchi kuendelea kuunga mkono maridhiano ya kisiasa kwa kushiriki kwa wingi katika kura ya maoni inayotarajiwa kufanyika Julai 31 mwaka huu kwa kukubali mfumo mpya wa serikali ya mapinduzi Zanzibar.

Katibu mkuu wa CUF Hamad anakuwa mwanachama pekee wa CUF kutaka kuteuliwa na chama chake kugombea nafasi ya urais wa Zanzibar.

Mwaka 1995 wanachama wa CUF Mataka Amour Mataka na Suleiman Khamis walijitokeza kuchuana na kiongozi huyo, lakini baadae walijiondoa katika mkutano wa baraza kuu la chama hicho. Soma Zaidi ...

6 WAFA 29 WAJERUHIWA KWENYE AJALI ZANZIBAR

Watu 6 wamefariki dunia na wengine 29 kujeruhiwa baada ya gari ya abiria waliyokuwa wakisafiria kuangukiwa na gari la kubebea maji katika ajali iliyotokea jana huko eneo la Koani, Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.

Gari aina ya Tata ililokuwa na namba T 807 AHC ililokuwa limebeba maji ilishindwa kupanda mlima na kuanza kurudi nyuma kwa kasi na kuiangukia gari ya abiria yenye namba za usajili Z 609 AB inayofanya safari zake kati ya Machui na mjini Zanzibar

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Makarani Ahmed, aliviambia vyombo vya habari kuwa, ajali hiyo ilitokea baada ya gari ya kubeba maji kufeli kupanda mlima na kuiangukia daladala iliyokuwa na abiria hao.

Akifafanua tukio hilo alisema kuwa kati ya majeruhi hao, 10 ni wanawake, 4 ni wanaume na 11 ni watoto na kusema wengi wao wamekatika miguu na mikono.

Waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni dereva wa daladala hiyo, Salum Ali Issa (38), Salum Ali Ame (40), Yussuf Abdallah Yussuf (79), Abdallah Maulid Abdallah (6), Shaida Amour Abdallah (27) na Asha Abdallah Saleh (30).

Hata hivyo kamanda huyo alisema dereva wa gari ililosababisha ajali alitoweka mara baada ya ajali hiyo kutokea na juhudi za kumsaka dereva huyo zinaendelea.

Ajali hii ilidaiwa na wakazi wa visiwani humo kuwa ni ajali mbaya ya kwanza kutokea toka mwaka huu uanze na wengi kusikitishwa na tukio hilo.

Makarani alisema majeruhi wa ajali hiyo wote wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja ya Zanzibar. Soma Zaidi ...

WASHUKIWA WA UGAIDI WAKAMATWA NEWYORK

Polisi jijini New York nchini Marekani wamewakamata wanaume wawili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa John F. Kennedy, ikiwa ni sehemu ya upelelezi, ambapo vyombo vya habari vimearifu kuwa wanahusishwa na mtandao wa al Qaida.

Gazeti moja nchini Marekani limearifu kuwa watu hao walikuwa wanapanga kwenda Somalia kujiunga na kundi la waislam wenye msimamo mkali. Watu hao walikuwa wapande ndege tofauti kuelekea Misri.

Inaarifiwa kuwa nyumba za watuhumiwa hao pia zilifanyiwa upekuzi na maafisa wa idara ya upelelezi ya Marekani FBI. Watu hao leo wanatarajiwa kupandishwa kizimbani katika mahakama ya New Jersey, kukabiliana na makosa ya kujihusisha na vitendo vya ugaidi.

Kukamatwa kwao kunafuatia jaribio lililoshindwa la kutaka kuripua eneo maarufu la Times Square kwa bomu lililotegwa kwenye gari mwezi uliopita. Soma Zaidi ...

TICKET ZA MECHI YA LEO


Soma Zaidi ...

Saturday, June 5, 2010

ENZI HIZOOOOOOO!!!!!!!!!


Hapa rais Jafar el Nimeiri wa Sudan akisalimiana na Omar
Zimbwe huku mohamed chuma (shoto) na nahodha
Abdulrahmani wakishuhudia. nyuma yao ni Kitwana Manara 'popat'
na Abdallah King Kibaden Mputa. hapa staazi walicheza vifua wazi
na Sudan baada ya kukosekana jezi. mwalimu Nyerere aliyehudhuria
mechi hii na mgeni wake hakuonekana tena mpirani toka siku hiyo....
Soma Zaidi ...

Friday, June 4, 2010

WAHAMIAJI HARAMU 21 WATIWA MBARONI KISIWANI TUMBATU

Jumla ya wahamiaji haramu 21 wamekamatwa baada ya kuingia nchini kinyume cha sheria na Idara ya uhamiaji Zanzibar kwa kushirikiana na Kikosi cha Kuzuwia Magendo KMKM katika Maeneo ya Tumbatu Unguja.

Katika taarifa yake Afisa Uhusiano wa Idara hiyo Muhsin Abdalla Muhsin amekiri kukamatwa kwa watu hao wakiwa ni raia wa Kenya ,Somali na Ethiopia ambao wameingia nchini kinyume cha sheria.

Amesema wamepata taarifa ya kukamatwa kwa watu hao siku ya Jumamosi na kikosi cha KMKM kwa msaada wa wananchi kutoa taarifa ya uwepo kwa watu hao .

Hata hivyo watuhumiwa hao wamefikishwa mahakamani kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.
Aidha amewataka wananchi kutoa taarifa zaidi ambapo wanagundua kuwepo kwa wageni ambao wanawatilia mashaka ili hatua za kiusalama ziweze kuchukuliwa. Soma Zaidi ...

UMEME PEMBA WAZIDNULIWA RASMIN


Rais wa Zanzibar Ambae ni mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi akibonyeza kitufye kuashiria uzinduzi rasmin wa umeme wa gridi ya taifa uliopita chini ya bahari kutoka Tanga hadi Pemba, uzinduzi ambao ulifanyika katika uwanja wa Gombani huko Pemba jana.
Soma Zaidi ...

WATURUKI WAOMBOLEZA WALIOPOTEZA MAISHA

Maelfu ya waombolezaji walikusanyika jana katika mazishi ya wanaharakati wa Kituruki waliouwawa wakati wa uvamizi wa majeshi ya Israel dhidi ya mlolongo wa meli za misaada. Rais Abdullah Gul amelihutubia taifa hilo lililokasirishwa kutokana na tukio hilo, kuwa uhusiano na Israel hauwezi tena kuwa wa kawaida.

Majeneza ya wengi wa wale waliouwawa yakifunikwa bendera za Uturuki na Palestina yalipelekwa katika msikiti wa mjini Istanbul wa Fatih kwa kuombewa dua, kabla ya kupelekwa katika maeneo wanakotoka kwa mazishi.

Watu wote tisa waliouwawa, ikiwa ni Waturuki wanane , pamoja na Mmarekani mmoja mwenye asili ya Uturuki, walikuwa katika meli ya Mavi Marmara wakati makomandoo wa Israel walipovamia meli yao katika eneo la maji la kimataifa.

Wakati huo huo vyombo vya habari vya Uturuki vimesema kuwa askofu mmoja wa kanisa Katoliki amekutwa amekufa kwa kupigwa visu leo kusini mwa Uturuki na dereva wake amekamatwa kwa madai ya kuhusika na mauaji hayo. Askofu Luigi Padovese , alikutwa amekufa katika nyumba yake ya mapumziko katika mji wa Iskendrun katika jimbo la Hatay katika pwani ya barahani ya Meditteranean nchini Uturuki. Jimbo la Hatay, linaishi jamii ya waumini wa Kikristo ambao wameishi katika eneo hilo tangu enzi za himaya ya Warumi. Soma Zaidi ...

JAJI NA KARANI WAKE WAPIGWA RISASI BRUSSELS

Mtu mmoja ambaye hakuweza kutambuliwa amempiga risasi jaji na karani wake katika chumba cha mahakama katikati ya mji wa Brussels nchini Ubelgiji jana.

Msemaji wa mwendesha mashtaka Jean-Marc Meilleur amesema mtu huyo mwenye silaha alikimbia na bado anatafutwa. Jean-Marc Meilleur anaamini kuwa mtu huyo bado ana silaha na hakuweza kuthibitisha iwapo amejeruhiwa.

Polisi wanaendelea na msako dhidi ya mtu huyo.

Haifahamiki kwa nini mshambuliaji huyo, ambaye amehudhuria kesi mahakamani hapo asubuhi ya jana pamoja na mawakili wawili, karani na jaji , aliwapiga wahanga hao wawili.

Waziri wa sheria Stefaan De Clerck amesema kuwa ni mara ya kwanza kwa jaji kuuwawa katika mahakama nchini Ubelgiji.
. Soma Zaidi ...

Wednesday, June 2, 2010

LUGHA GANI HII?

Soma Zaidi ...

FABIO CAPELLO ATAJA KIKOSI CHAKE

Kifuatacho ni kikosi kitakachoiwakilisha Uingereza katika michuano ya fainali za kombe la dunia itakayofanyika huko Nchini Afrika Kusini:


Goalkeepers:
James, Green, Hart

Defenders:
Ferdinand, Terry, King, Upson, Carragher, Cole, Johnson, Warnock

Midfielders:
Gerrard, Lampard, Wright-Phillips, Milner, Barry, Carrick, Joe Cole, Lennon
Strikers: Rooney, Crouch, Heskey, Defoe

Katika hali ya kushangaza wengi Capello amemuacha kiungo mshambuliaji Theo Walcott ambae alitoa mchango mkubwa katika hatua ya makundi kutafuta kufuzu kuingia fainali za kombe hilo na pia ndio aliekua ni tegemeo la Waingereza wengi.

Wachezaji wengine ambao wameachwa katika kikosi hicho ni pamoja na Dawson, Baines, Johnson, Parker, Huddlestone, Bent Soma Zaidi ...

ISRAEL KUWAACHIA RAIA WA KIGENI WALIOKAMATWA NDANI YA MELI

Israel imesema itawaachia raia wote wa kigeni, ambao walikamatwa na jeshi la nchi hiyo siku mbili zilizopita katika shambulio la umwagaji damu lililofanywa dhidi ya meli iliyobeba misaada kuelekea Gaza.

Israel imechukua uamuzi huo kutokana na matakwa ya viongozi duniani, ambao pia wametaka kufanyika kwa uchunguzi juu ya shambulio hilo la Jumatatu, ambao ulisababisha vifo vya wanaharakati tisa.

Katika mkutano uliofanyika mjini New York Marekani, wanachama wengi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa waliilaani Israel na kuitaka nchi hiyo kuondoa vizuizi ilivyoweka Gaza.

Msafara huo mdogo wa meli, ulikuwa umeandaliwa kwa pamoja na kundi linalowaunga mkono Wapalestina pamoja na Shirika la Haki za Binadamu la Uturuki.

Uturuki imesema watu wanne miongoni mwa watu tisa waliouawa, ni raia wake na kuliita tukio hilo kama ugaidi wa kitaifa.

Wakati huohuo Serikali ya Israel imesema imewaachia kutoka gerezani ilikokuwa ikiwashikilia wanaharakati wapatao 50 wa Uturuki waliokuwa katika meli hiyo iliyobeba msaada na kwamba watarudishwa kwao. Soma Zaidi ...

Tuesday, June 1, 2010

MARUFUKU KWENDA KOMBE LA DUNIA: GHANA

Rais wa Ghana amewapiga marufuku mawaziri wake pamoja na maafisa wengine wa serikali kwenda Afrika kusini kuangalia fainali za kombe la dunia hadi pale watakapokuwa na majukumu ya kiserikali katika fainali hizo.

John Martey Newman, msemaji wa rais John Atta Mills , amesema kuwa amri hiyo ina lengo la kuhakikisha kuwa shughuli za kiserikali hazivurugiki wakati wa fainali hizo, ambazo zinaanza rasmi barani Afrika kwa mara ya kwanza Juni 11.

Kikosi cha timu ya taifa ya Ghana , Black Stars, moja kati ya matumaini makubwa ya bara hilo , ilikuwa ni timu ya kwanza kufanikiwa kupata tikiti ya kushiriki fainali hizo za kombe la dunia mwaka 2010, na itakumbana na Ujerumani, Serbia na Australia katika kundi D. Soma Zaidi ...

ISRAEL YAUA WATANO GAZA

Israel imewauwa wapiganaji watano wa Kipalestina katika ukanda wa Gaza leo, watatu katika mashambulio ya anga baada ya shambulizi la roketi dhidi ya ardhi ya Israel na wawili wengine katika mapambano mengine ya ardhini.

Jeshi la Israel limethibitisha kuwa ndege zake zimeshambulia wapiganaji katika ukanda wa Gaza na kwamba watu wawili wenye silaha wameuwawa baada ya kuvunja amri ya kutokaribia uzio wa mpaka katika eneo la pwani, lakini haikutoa taarifa zaidi.

Msemaji wa kundi la Popular Resistance Committees amesema kuwa wanachama watatu wa kundi hilo wameuwawa katika shambulio la Israel katika eneo la kaskazini mwa Gaza, mmoja akiwa kamanda wa kundi hilo. Soma Zaidi ...