Sunday, February 28, 2010

BENDERA ZA TANGANYIKA KWENDA TANZANIA

Hii ilikua kuanzia mwaka 1900 - 1919
Hii ilikua kuanzia mwaka 1919 - 1961
Hii ilikua kuanzia mwaka 1961 - 1964
Na hii i kuanzia mwaka 1964

Soma Zaidi ...

ZAIDI YA RAIA 300 WAFARIKI BAADA YA TETEMEKO LA ARDHI NCHINI CHILE

Maafisa wa serikali nchini Chile wanasema kwamba kiasi cha watu 300 wamefariki kufuatia tetemeko la ardhi la 8.8 kwenye kipimo cha Ritcher lililopiga kwenye mwambao wa nchi hiyo mapema jana asubuhi.

Idadi ya watu waliofariki inatarajiwa kuongezeka. Rais wa Chile Michelle Bachelet amesema mkasa huo ni janga la kitaifa. Uharibifu mkubwa umeripotiwa katika mji wa Concepcion kilomita 100 kutoka eneo lilikoanzia tetemeko hilo ikiwa pia ni kilomita 300 kutoka mji mkuu Santiago.

Tetemeko hilo la ardhi limesababisha Tsunami katika bahari ya Pacific huku nchi kadhaa katika eneo hilo zikiwa katika hali ya tahadhari kukabiliana na kishindo cha Tsunami.Kituo kinachohusika na utoaji onyo la kutokea kwa Tsunami,kimethibitisha kwamba mawimbi ya Tsunami yamepiga kwa muda mfupi eneo la Hawaii.Aidha maeneo ya Polynesia, Ufaransa, kisiwa cha Chadham mashariki mwa NewZealand na miji ya pwani ya Chile pia yameshuhudia mawimbi hayo.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Guido Westerwelle ametuma rambirambi zake kwa waathiriwa na amesema kundi la waokoaji limetumwa nchini Chile. Rais wa Marekani Barack Obama ametuma rambirambi zake kwa raia wa Chile waliopoteza jamma zao na ametoa onyo kwa wakaazi ufuoni ikiwemo Hawaii wawe chonjo.

Jumuiya ya Ulaya imeahidi kutoa euro millioni tatu kwa ajili ya kusimamia msaada wa dharura.

Rais Bachelet amesema zaidi ya makaazi milioni mbili yamaeathiriwa na laki tano yameharibiwa vibaya.
Soma Zaidi ...

Saturday, February 27, 2010

CHEKA KIDOGO - KILIMO CHA MTAKULA ZANZIBAR

Wakati wa aboud Jumbe, alitoa maagizo kwa wananchi kuwa kuna mradi wa MTAKULA, maana yake ni kuwa kila familia au nyumba lazima wawe na shamba la migomba 300.

Katika kijiji kimoja pale Pemba (Mtambile kuna jamaa mmoja alikuwa hashughuliki na suala hilo la kupanda migomba.

Akiamka anakwenda katika charahani yake anashona na jua likitua anarejea kwake.

Sheha wa pale alikuwa ni mtu mkorofi na alikuwa haipendi ngozi nyeupe, basi akamtomeza mkuu wa wilaya kuwa kuna mtu hataki kulima na kufuata maagizo ya Mtakula. Ukapangwa mkakati wa mkuu wa wilaya kuja kufanya ukaguzi wa migomba mtambile, lakini lengo lilikuwa nikutaka kutia hatiani jamaa huyo.

Bhati katika baraza la pale kijijini, mmoja wa wajumbe wake (balozi) ni ngozi nyeupe na yeye, na akamjulisha jamaa kuwa unakuja kukaguliwa fanya bidii upate migomba 300.

Fundi charahani huyo hakuwa na wasi wasi na alimjibu balozi kuwa hamuna wasi wasi wacheni muje tu, Balozi alishangaa kusikia hivyo kwa vile fundi huyu anajulikana hajashikapo jembe zaidi ya charahani yake.

Mkuu wa wilaya Ali Mussa akaja Mtambile na kaanza kufanya ukaguzi kwa baadhi ya watu kisha wakamwendea fundi.

Huyu fundi alikuwa akikaa karibu na kitua cha polisi, lakini akishona karibu na kiunga cha famili Mtambile mjini na ni nyuma tu ya hapo anaposhona.

Sheha: Fundi mhe. mkuu wa wilaya anataka kuona migomba yako 300

Fundi: sawa twendeni hapo nyuma.

Walipofika:

Fundi: Ingieni humu katika shina la kijakazi hesabuni mia 300 kama haijatosha nitawapeleka sehemu nyengine pale chini.

Mkuu wa Wilaya: Umetakiwa ulime migomba 300 ya ndizi mbali mbali siyo aina moja.

Fundi: Maagizo yaliyotolewa yamesema migomba 300 tu na siyo migomba maalum.

Balozi pale alipo anataka kupasuka mbavu kwa kuchekea ndani kwa ndani, na yule mkuu wa wilaya alihamaki akapanda gari akarudi Mkoani.

Shina moja la migomba hiyo ilikuwa ni zaidi ya elfu wakati huo na alikuwa nayo matatu pale. Soma Zaidi ...

MECHI ZA LEO

Mechi inayotarajiwa kua nzuri na ya kuvutia ni kati ya Chelsea watakapo wakaribisha Man City katika uwanja wao wa nyumbani huku mechi hio ikiwa na wasi wasi kwa timu zote mbili kwani timu zote mbili zitawakosa baadhi ya wachezaji wake muhimu.

Chelsea watamkosa mlinda mlango wao nambri moja petr Cech ambae anasumbuliwa na misuli ambapo wantarajiwa kumchezesha mlinda mlango wao nambari mbili Hilario.

Mlinzi wa kushoto wa Chelsea na timu ya taifa Uingereza Ashley Cole ambae pia ni mgonjwa wa ancle kwa muda mrefu nae nafasi yake itachezwa na Malouda, lakini kama hii haitoshi Chelsea pia wana tatizo la viungo wao wawili Deco, Essien pamoja na mlinzi wao wa kulia Bosingwa ambao wote wanasumbuliwa na magoti.

Lakini pia kwa upande wa wageni City nako hali sio nzuri kwani wanataria kuwakosa wachezaji wao kadhaa muhimu kama vile mshambuliaji machachari Emmanuel Adebayor ambae anatumikia adhabu ya kutocheza mechi tatu.

Mlinzi Kolo Toure anaendelea kukaa juu kutokana na tatizo la goti, Santa Cruz nae pia atakosa mechi ya leo kwa kua na tatizo hilo hilo la goti huku kiungo Patric Vieira nae akikosa mechi ya leo kutokana na kutumikia adhabu yake ya kutocheza mechi tatu.

Lakini Man City wataweza kufaidika katika mechi ya leo kwani wataweza kumchezesha mshambuliaji wao Carlos Tevez ambae amesharejea kutoka Argentina ambako alikwenda kwa sababu ya mambo ya kifamilia.


Premier League
13:45 Chelsea v Manchester City
16:00 Birmingham City v Wigan Athletic
16:00 Bolton Wanderers v Wolverhampton Wanderers
16:00 Burnley v Portsmouth
16:30 Stoke City v Arsenal

La Liga
18:00 Getafe CF v Real Zaragoza
20:00 CD Tenerife v Real Madrid
22:00 FC Barcelona v Málaga CF

Bundesliga
15:30 VfL Bochumvs1. FC Nürnberg
15:30 Hertha BSCvsHoffenheim
15:30 FSV Mainz 05vsWerder Bremen
15:30 VfB StuttgartvsEintracht Frankfurt
15:30 Borussia MönchengladbachvsSC Freiburg
18:30 Bayer Leverkusenvs1. FC Köln Soma Zaidi ...

THE REASON WHY I DON'T VISIT RICH PEOPLE

Question: 'What would you like to drink ... fruit juice, soda, tea, milo, chocolate, or coffee?'
Answer: 'Tea please'
Question: Ceylon tea, herbal tea, bush tea, honey bush tea, ice tea or green tea?'
Answer: ' Ceylon tea please'
Question: 'How would you like it? Black or white?'
Answer: 'White please'
Question: 'Milk, whitener, or condensed milk?'
Answer: 'Milk please'
Question: 'Goat milk, camel milk or cow milk?'
Answer: 'Cow milk please.'
Question: 'Milk from Freezeland or Afrikaner cow?'
Answer : 'Afrikaner cow please.'
Question: 'Warm or cold?'
Answer: 'Warm please.'
Question: 'Full cream, low fat or fat free?'
Answer: 'Umm ... I'll rather take it black please.'
Question: 'Would you like it with sweetener, sugar or honey?'
Answer: 'With sugar please.'
Question: 'Beet sugar or cane sugar?'
Answer: 'Cane sugar please.'
Question: 'White, brown or yellow sugar?'
Answer: 'Just forget about the tea. I'll have a glass of water instead please.'
Question: 'Mineral or still water ? '
Answer: 'Mineral water please.'
Question: 'Flavoured or non-flavoured ?'
Answer: 'Hey, futseki mann! Just get me water from the river... I don't wanna know which river, and stop asking me too many questions. ALA !! Soma Zaidi ...

Friday, February 26, 2010

FUMBA LEO HII

Mafundi wakijadiliana ili kupata ufumbuzi juu ya nini cha kufanya Ni miongoni mwa insulators zilizo vunjika

Majukwaa kwa ajili ya ufungaji wa insulators na vifaa vyengine
Mafundi wakiwa katika kituo cha Fumba wanaonekana bado wapo katika harakati za kuurudisha umeme Kisiwazi Unguja na wanatarajia kufunga kazi mnamo sasa sita usiku kwa saa za Afrika Mashariki, lakini kuna baadhi ya Insulators zimevunjika na hii inaweza ikasabisha ucheleweshaji wa uwashwaji umeme.

Soma Zaidi ...

BARUA YA PAPII KOCHA KWENDA KWA JK

MF/NA: 836’04 Johnson Nguza (Papii Kocha)

Gereza Kuu Ukonga
S.L.P 9091
Dar es Salaam

Mh. Rais Jamuhuri ya Muungano Tanzania

YAH: MAOMBI YA KUPEWA MSAADA (MSAMAHA) WA KUFUTIWA ADHABU YA KIFUNGO NILIYOPEWA NA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU.

Husika na somo hilo hapo juu. Mimi ni mfungwa katika Gereza Kuu Ukonga.
Kwa heshima na taadhima na kwa kutambua utu na huruma yako ya ki MUNGU ulionayo dhidi ya binadamu wenzako pamoja na mamlaka uliyokabidhiwa na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Naanguka na kushika miguu yako mitukufu mheshimiwa rais.
Na kuomba msaada (msamaha) kwako muheshimiwa rais
Kwa njia hii ya maandishi kusudi niweze kuondolewa adhabu ya kifungo cha maisha gerezani, niliyohukumiwa na mahakama tajwa hapo juu.

Mh. Rais mimi nimefungwa nikiwa bado kijana mwenye umri mdogo. Mpaka sasa natambua wazi hatma pamoja na dhamana ya maisha yangu ipo katika mikono yako mitukufu Mh. Rais.
Naomba huruma yako mheshimiwa Rais maana mimi ni mtoto wako ninayehitaji huruma yako wewe mzazi.

Natumaini kauli yako ya mwisho ndiyo itakayoleta pumzi ya uhai nafsini mwangu
Nakutakia kazi njema, afya njema na maisha marefu.
Mungu akubariki

Wako mtiifu
NO:836’04
JOHNSON NGUZA (PAPII KOCHA) Soma Zaidi ...

TUDUMISHE MILA


Assalam aleykum

Enzi tulipokuwa wadogo, ilikuwa wali unapambiwa kwa mkungu, unafanya gamba (matandu) ya brown, mpunga mpya unanukia

Vile vile vijana walikuwa wanakung'utia maji ili yaonekane makaa yashamaliza kazi

Wapi, utamaduni umepotea! watu wote wanapiga rice cooker, wali si wali, bonndo si bondo, ni balaa tu.

Mchuzi pia ukipikwa kwa vyungu waweza ukajiramba, lakini wapi, watu wote tumejaa maluminium miili mwetu

Jee tunakwenda mbele au twarudi nyuma? Iko haja ya kudumisha mila.


***Mpitanjia Soma Zaidi ...

GHADAFI AITISHA VITA VYA JIHADI DHIDI YA USWIZI

Kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi amewataka Waislamu kuanza vita vya Jihad dhidi ya Uswizi.
Kanali Gaddafi anadai kwamba nchi hiyo imeanzisha kampeini ya kuharibu misikiti baada ya kura ya maoni nchini humo mwezi Novemba, kuidhinisha kupigwa marufuku kwa ujenzi wa minara katika misikiti ya Uswizi


Kanali Gaddafi pia ametaka waislam kote duniani kususia bidhaa za Uswizi. Kiongozi huyo wa Libya ameyasema hayo mjini Benghazi wakati wa kuadhinisha siku ya kuzaliwa kwa Mtume Mohamed.

Mwezi Novemba mwaka uliopita, wapiga kura nchini Uswisi waliidhinisha sheria ya kupiga marufuku ujenzi wa minara nchini humo, kupitia kura ya maoni. Uamuzi huo wenye utata unazusha hofu juu ya uwezekano wa kuzuka uhusiano mbaya kati ya Uswisi na jamii ya Kiislamu.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Uswisi, Lars Knuchel alikataa kuzungumzia wito huo uliotolewa na Gadhafi wa kuanzishwa vita vitakatifu dhidi ya nchi hiyo.

Kumekuwa na mzozo wa kidiplomasia kati ya Libya na Uswizi tangu mwana wa Kanali Gaddafi pamoja na mkewe kukamatwa nchini humo kwa tuhuma za kumdhulumu mjakazi.

Wiki iliyopita, Libya iliwapiga marufuku raia wa muungano wa Ulaya kupata vibali vya kuzuru nchi hiyo. Hiyo ilifuatia hatua ya Uswizi kutoa orodha iliyowawekea vikwazo raia 188 wa Libya, ikiwa ni pamoja na Kanali huyo na watu wa jamii yake. Soma Zaidi ...

HATIMAE TAREHE 01/03/2010 UMEME WAWASHWA ZANZIBAR


BAADA YA GIZA NA UKOSEFU WA MAJI ZANZIBAR SABABU KUU UMEME HATIMAE TAREHE 01/3/2010 UMEME WAWASHWA
Kwa habari za kuaminika kutoka kwa wataalamu wa umeme huko fumba kisiwani zanzibar hatimae umeme wanategemewa kuwashwa rasmi hapo 01/3/2010 mmoja katika mafundi hao alisema kwa sasa kila kitu kimekamilika hakuna sababu yeyote hadi sasa labda litokezee tatizo jengine mara tu baada ya kuwasha.

Pia mwandishi wetu alikutana na waziri wa nishati muheshimiwa Mansour Yussuf Himid na kumuhoji juu ya suala zima kuhusiana na umeme na maji kuwa wanachi wa zanzibar takribani miezi mitatu sasa wanapata shida sana maji tabu .
Wakati mwengine wananchi wananunua maji tena maji yenyewe ya udanganyifu mana huuziwa maji ya chunvi bila wao kujua pia vifo vinavyo sababishwa na mageneretar na joto usiku hakuna kulala waziri huyo yote hayo alikiri na kusema nikweli ila tunatarajia kuurudisha umeme haraka iwezekanavyo ili kuepusha matatizo yalipo nchini , mwezi ujao 01/3/2010 pia mimi nawataka Wanzanzibari na wananchi mbali mbali waishio zanzibar kua na subra na uvumilivu.
Soma Zaidi ...

Thursday, February 25, 2010

URAIA WA NCHI MBILI: TUKIZUBAA TUMELIWA !!

Binafsi sina tatizo kabisa na kuruhusu Watanzania kuweza kuwa na uraia wa zaidi ya nchi moja (sielewi kwanini lazima uwe wa nchi mbili tu!) lakini kama unavyosema lazima tuweke wazi exceptions kwa sababu.. nakumbuka Fujimori kilipomuungulia kule Peru akakimbia nchi ya asili ya wazazi wake (Japani!) akidai uraia wa kule. Leo hii tunaona jinsi Wahaiti wenye uraia wa Marekani kilipoungua kule Haiti walivyokimbia kuonesha passport zao kuwa wao ni raia wa Marekani. Tumeliona hili hata kule Lebanon wakati mgongano kati ya Israel na Hezbollah. Tanzania itakuwa hivyo hivyo (tayari in some cases with some people in the Asian communities).

Tusipoweka mambo vizuri.. watawala wetu watakuwa ni raia wa nchi nyingine huku wakifanya mambo bila ya kujali maslahi ya nchi yetu hii kwani wanajua tukitaka kuwatia pingu wanaonesha passport zao au zile za watoto wao na kutimka kwenda "kwao"!

so.. tunaporuhusu uwezekano wa mtu kuwa na uraia wa nchi zaidi ya moja ni lazima wakati huo huo tuainishe vizuri kabisa mipaka ya jambo hilo. Sasa kama wakati huu ambapo hatuna sheria hiyo na tunajua kuwa mtu akiwa na uraia wa nchi nyingine anakuwa ameuakana uraia wetu inakuwaje katika akili timamu tunampendekeza kutuwakilisha kwenye nchi nyingine wakati siyo raia wetu!?

Kuna watu ambao walikuwa karibu sana na serikali yetu kwa miaka mingi baada ya mambo kutulia kwenye nchi zao wakafunga virago na kurudi "kwao" a.k.a Wanyarwanda tuliowadhania ni Waangaza!

Mimi sipingi uraia wa nchi mbili at all.. napinga kanuni zinazopendekezwa. Hatuwezi kubadilisha nature ya uraia wetu kwa sababu ya rangi, nasaba, hali ya kiuchumi, kufuata mtindo n.k.. we have to articulate proper arguments why we have to change.. siyo nchi zote duniani zinaruhusu uraia wa nchi mbili hata zile za kiafrika au za kimagharibi. Sielewi kwanini tuonekane tunafuata zile za nchi fulani na zile za nchi nyingine tuone hazifai.

Chanzo: Mwanakijiji Soma Zaidi ...

SARKOZY KUWASILI RWANDA

Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa anawasili leo nchini Rwanda katika ziara yenye nia ya kurejesha uhusiano mwema kati mataifa hayo mawili, ambao uliharibika kutokana na mauaji ya halaiki nchini humo ya mwaka 1994.


Sarkozy anakuwa rais wa kwanza wa Ufaransa kuizuru Rwanda tokea mauaji hayo, ambapo zaidi ya watutsi laki nane na wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa katika kipindi cha siku mia moja cha mauaji hayo.

Uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili ulivunjika mwaka 2006, baada ya jaji mmoja wa mahakama ya Ufaransa, kumtuhumu Rais Kagame kuwa alipokuwa kiongozi wa waasi alichangia mauaji hayo kwa kushiriki kwake katika kutunguliwa kwa ndege aliyekuwemo Rais wa wakati huo Juvenal Habyarimana.

Rais Sarkozy anawasili Rwanda akitokea Mali alikofanya ziara ya kushtukiza, na kukutana na mateka wa kifaransa Pierre Camatte aliyeachiwa huru na wapiganaji wa tawi la al Qaida la Afrika Kaskazini.Kabla ya hapo aliizuru Gabon Soma Zaidi ...

Wednesday, February 24, 2010

U SHEIKH UKO WA AINA NYINGI

Ninavyojua mimi kuna vitu vitatu amavyo vinapelekea mtu kuitwa "Sheikh" na kama nitakua sijakosea, hii ndio kanuni haswa ya neno hili "Sheikh"

1. Mtu mzima aliyefikia makamo ya uzee.

2.Mtu mwenye fani (kazi) kama vile ufundi, udaktari, n.k.

3.Mtu mwenye elimu ya juu katika mambo ya dini ya Kiislamu.

Mambo hayo matatu mtu akiwa na moja kati ya hayo basi watu wanaweza kumpa au kumwita jina la "Sheikh", sasa hebu msikilize kwa makini huyu anaeitwa "Sheikh Yahya" ikisha utaniambia kaitwa

"Sheikh" kutokana na jambo lipi moja wapo?

Soma Zaidi ...

MIGOMO YA NDEGE BARANI ULAYA

Waongozaji safari za ndege nchini Ufaransa wameanza mgomo wao wa siku nne, kupinga wazo la kuunganisha mamlaka za kimataifa zinazosimamia safari za ndege. Ubelgiji, Ufaransa,

Ujerumani, Luxembourg, Uholanzi na Uswisi wana mpango wa kuunganisha mamlaka zao za safari za ndege ili kuimarisha usalama na pia kupunguza gharama.

Hata hivyo kuna uwezekano wa kufanyika mgomo wa wahudumu wa Shirika la ndege la Uingereza British Airways, hapo kesho wakitaka nyongeza ya mishahara.

Kiasi cha wafanyakazi milioni tatu nchini Ugiriki wanatarajiwa kushiriki katika mgomo wa kitaifa hii leo. Vyama vya wafanyakazi vinataka mapendekezo ya hatua kali za kurekebisha uchumi kutupiliwa mbali. Mapendekezo hayo ni pamoja na hatua ya kusimamisha nyongeza za mishahara pamoja na kuongezwa kwa kodi.

Mgomo huo wa sekta za umma utasababisha kufungwa kwa shule, hospitali na afisi za serikali pamoja na kutatiza shughuli za usafiri. Mgomo huo unakuja wakati Maafisa wa Umoja wa Ulaya wanakutana mjini Athens kuangalia vipi watapunguza upungufu mkubwa uliopo katika bajeti ya serikali ya Ugiriki. Soma Zaidi ...

UJUMBE KUTOKA ZANZIBAR - SMS

(((( ))))
((( @) (@ )))
(((; <._.> ; )))
( ——-, )
1.Angalia nilivyobabuka uso kwa joto na mapele ya mbu yamenijaa.
Upara ushaota kwa madumu ya maji. Lakini tunawambia kisiwa hakiuzwi anaetaka akae kama hawezi ahame…
Mapinduzi daimaa…Umeme mpaka mwakani, atakaekufa na afe,
CCM Oyee!

2.Dua za kisasa
Asalam-alaykum!
Dua ni zawadi moja kutunukiwa huna budi kuipokea
Napendelea furaha yako iongezeke kama BEI YA PETROLI. Mashaka yakupotee kama UMEME WA ZANZIBAR. Umaarufu wako uzidi kama SHIDA YA MAJI.Mungu akupe subira kama unavyo subiri UMEME. Hekima zako zizagae kama kelele za MAJENRETA kwenye kisima chetu cha Zanzibar..AMIN.


Soma Zaidi ...

PONGEZI KWA SPIKA WA BARAZA LA WAWAKILISHI

Spika BLW Zanzibar Mh. Pandu Ameir Kificho

MUWAZA inakutunukia pongezi zake za dhati kwa matamshi yako ya kizalendo ya kutetea uhuru, uwezo na nguvu za BLW kwa kutamka kwamba “Hakuna Mtu au Utawala wowote unaoweza kubadilisha maamuzi ya BLW”.

MUWAZA imefarijika na inatoa pongezi kwa msimamo madhubuti huo ambao umeweka wazi Mamlaka ya BLW na kuondosha tafsiri za migongano zilizotolewa hapo kabla baada ya Mkutano wa NEC wa karibu huko Dodoma.

Kauli hiyo ilio wazi na isio na wasi wasi wowote ya Mh. Spika wa BLW imesaidia kutolewa kwa kauli sahihi ya Rais wa Muungano wa Tanzania Mh. Rais Jakaya Mrisho Kikwete huko Uturuki na kufuatiliwa na kauli sahihi za ndugu zetu Waziri wa Mambo ya Kimataifa wa Tanzania Mh. Bernard Membe pamoja na kusahihishwa kwa kauli sahihi ya Katibu Muenezi wa CCM Mh. John Chiligati. MUWAZA imefurahishwa kusikia kauli sahihi na zilizorekibishwa na ndugu zetu hawa wa Bara kwa kuunga mkono maamuzi ya BLW na kuitakia Zanzibar mema.

MUWAZA inamshukuru Spika wa BLW Mh. Pandu Ameir Kificho kuwa ni chachu ya kuondosha wingu la suitafahum baina ya ndugu zetu wa Tanzania Bara na Zanzibar

MUWAZA vile vile inaomba kutumia nafasi kwa kupitia kwa Mh. Pandu Ameir Kificho kuwapongeza Wawakilishi wote wa Baraza la Wawakilishi kwa kuonyesha moyo wa maridhiano, kutetea mustakbal wa Zanzibar kwa pamoja bila ya kujali mirengo ya kisiasa, kusimama kidete kwa sauti moja katika dhamana yao ya kuondosha uhasama baina Wazanzibari na kuchimba misingi ya mashirikiano kwa maslah ya Zanzibar na kuzika uadui ulio wafarakanisha Wazanzibari kwa muda mrefu

MUWAZA vile vile kwa kupitia Spika wa BLW inawapongeza Wawakilishi wote kwa kusimamia utekelezaji wa:

Kusimamisha BENDERA ya Zanzibar,
Kuanzisha NEMBO ya Zanzibar,
Kuanzisha WIMBO WA TAIFA,
Kutetea MAFUTA ya Zanzibar
Kulilinda na kulitukuza BLW
Kulinda, kuitetea, kuihifadhi na kuitengeneza KATIBA ya Zanzibar
MUWAZA kwa kupitia Mh. Spika wa BLW inatuma pongezi zake za dhati kwa Mwanashria Mkuu Mh. Iddi Pandu Hassan pamoja na timu yake ya Wanasheria kwa kutunga kwa haraka Sheria ya Kura ya Maoni Zanzibar, sheria ambayo itaifungulia Zanzibar milango ya kheri siku za usoni.

MUWAZA haitakuwa mwizi wa fadhila kwa kusahau chanzo cha michango ya maraidhiano kwa hivyo papo inachukuwa fursa hii adhiim kuwapongeza tena Rais wa Zanzibar Dk. Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Shariff Hamad kwa ushujaa na ujasiri wao kuiletea maridhiano ya Zanzibar.

Kwa niaba ya MUWAZA
Dr. Yussuf S. Salim Mwenyekiti wa Muda wa MUWAZA

Febuari 24, 2010 Gawanyo Kitaifa
Soma Zaidi ...

Tuesday, February 23, 2010

TUSOME UJUMBE PALE PALE TUNAPO UPOKEA

Mgonjwa mmoja mahututi alikuwa hawezi kuongea na kuwekewa oxygen akawa anaombewa na mchungaji akiwa anaombewa, yule mgonjwa akachukua kalamu na karatasi.

Akaandika na akampa yule Mchungaji, ambaye badala ya kuisoma ile karatasi, akaitia kwenye
mfuko wa joho na kuendelea na maombi hadi yule mgonjwa, AKAKATA ROHO.

Mchungaji hakuisoma ile karatasi akijua kua ni wosia wa marehemua, akasubiri baada ya mazishi kwenye kikao cha ndugu akasema:-

"KUNA KITU NILIPEWA NA MAREHEMU SIKU NILIYOKUA NAMUOMBEA"

Akampa mmoja wa wanandugu akisome, haya ndiyo yaliyokuwa yameandikwa na yule mgonjwa:

"UMEKANYAGA WAYA WA OXYGEN, NAKOSA HEWA"

JE KAMA NI NDUGU YAKO ALIEFARIKI UTAFANYA NINI ? AU UTASHAURI NINI ?
Soma Zaidi ...

FIKIRIA KABLA YA KUTUMA KITU CHOCHOTE KWENYE FACEBOOK

Soma Zaidi ...

SABABU YA MAUAJI YA WATU 17 MUSOMA


Mauaji ya kikatili ya watu 17 wa familia tatu yaliyotokea mwanzoni mwa wiki iliyopita katika Kata ya Buhare, nje kidogo ya Mji wa Musoma mkoani Mara, yameibua mambo mengine mazito yaliyofichika.

Uchunguzi wa umebaini kwamba, katika tukio hilo majeruhi watatu waliopelekwa katika hospitali ya Mkoa wa Mara, siku mbili baadaye mmoja alifariki dunia na kuacha ndugu wawili wakiendelea kuuguza majeraha

Ilibainika kwamba, chanzo cha mauaji hayo ya watu wa ukoo mmoja ni kutaka kulipiza kisasi cha muda wa miaka minne iliyopita kutokana na ukoo huo kudaiwa kuuwa watu fulani kwa tuhuma za wizi wa ng’ombe.

Uchunguzi huo unakwenda mbele zaidi kuwa, watu hao walitenda ukatili huo kwa kukusudia kutokana na ahadi ya nyuma waliyoitoa kuwa ndugu zao waliouawa mwaka 2005, hivyo ilikuwa ni lazima walipe kisasi.

Ilibainika kwamba, pamoja na kuwa na nguvu kubwa lakini nyumba za wanaukoo huo ziko mbalimbali hivyo kurahisha zoezi la mauaji kwani ingekuwa ngumu mno kukusanyika ili kukabiliana na maadui zao.

Ilifahamika pia kwamba, lengo la wauaji hao ilikuwa ni kumaliza ukoo mzima ili kupoteza ushahidi.

Akisimulia mkasa mzima, mtoto mdogo aliyenusurika aliyejitambulisha kwa jina la Kurwa Kawawa alisema kuwa alisikia milio ya mapanga na kelele za ndugu zake wakiomba msamaha kwa wauaji hivyo akaingia kwenye damu ambapo wauaji walidhani kuwa amefariki kumbe alikuwa hai.

Mwingine ambaye hakuweza kutaja jina lake kufuatia hofu kubwa aliyokuwa nayo, alisema alisikia wauaji wakimlazimisha kaka yake kutoa pesa ambapo aliingia uvunguni na ndipo alipoweza kuwashuhudia jamaa hao wakiwakata ndugu zake kwa mapanga na baadae walimvamia ng’ombe na kumcharanga mapanga.

Ilifichuka kwamba, wauaji hao walikuwa ni watu wenye hasira kufuatia kuwepo kwa madai kuwa waliouawa ni ukoo wenye tabia ya wizi wa mifugo, huku chuki ikitawala zaidi.

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Mstaafu Enos Mfuru ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa aliliagiza Jeshi la Polisi kufanya kila linalowezekana kuwakamata wote waliohusika.

Katika tukio hilo watu kumi wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za mauji hayo.

Soma Zaidi ...

WATANO WA FAMILIA MOJA WAFARIKI KWA AJALI YA GARI PWANI

Ajali za barabarani zimeendelea kutisha katika mkoa wa Pwani baada ya watu watano wa familia moja kufariki dunia papo hapo na wawili kujeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha magari mawili waliyokuwa wakisafiria kugongana katika eneo la Ruvu - Nafco wilayani Bagamoyo.

Ofisa Upelelezi mkoani Pwani, Nsato Marijani aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa tukio hilo liilitokea katika barabara ya Dar es Salam - Morogoro na ilihusisha magari mawili ambayo yaligongana uso kwa uso na kusababisha vifo hivyo pamoja na majeruhi.

Alisema gari lenye namba za usajili T 707 EEF aina ya Fuso lililokuwa likiendeshwa na Abdul Hassan (30) mkazi wa Tabata jijini Dar es Salaam kwenda mkoani Morogoro liligongana na gari ndogo aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba za usajili T 529 AED lililokuwa likiendeshwa na mtu aliyetambulika kwa jina moja la Mohamed.

Marijani alisema baada ya ajali hiyo, watu watano waliokuwa wamepanda gari dogo lililokuwa likitokea Morogoro, akiwemo dereva walifariki dunia na maiti zote zimehifadhiwa katika Hospatali Teule ya Tumbi wilayani Kibaha.

Aliwataja waliofariki kuwa ni mtoto wa miaka minne ambaye hakutambulika jina, Mwasiti Hamisi (23), Mwalami Salumu (21), Fatuma Salum (23) na dereva wa gari hilo aliyetambulika kwa jina moja la Mohamed wote wakazi wa Dar es Salaam.

Aliwataja waliojeruhiwa kuwa ni Mohamed Salum (30) na Yasira Mohamed (2) wote wakazi wa Dar es Salaam ambao wamelazwa katika Hosptali ya Tumbi kwa matibabu.
Soma Zaidi ...

THE HAGUE (DEN HAAG) YA KENYA

Soma Zaidi ...

BOFULO


Soma Zaidi ...

Monday, February 22, 2010

UINGEREZA KUWABANA WANAFUNZI WA KIGENI

Sheria kali zilizoanzishwa nchini Uingereza kuhusu wanafunzi kutoka nje ya ulaya wanaokuja nchini humo kwa masomo zitawafanya wanafunzi wengi kutoka barani Afrika kutoweza kusomea Uingereza.

Idara ya uhamiaji Uingereza - UK Border Agency, imesema watu wengi wametumia vibaya na kukiuka sheria za uombaji wa viza hasa za wanafunzi.

Serikali ya Uingereza imeongezea vikwazo kupiga vita ukiukaji wa sheria hizi. Ukiukaji wa sheria umekuwa ukifanyika kufuatia kukomeshwa kwa uchunguzi uliokuwa ukifanywa kuhakikisha kwamba wanafunzi wanarudi nchini mwao baada ya kumaliza masomo yao na mda waliopewa na idara ya uhamiaji Uingereza kumalizika.

Ingawaje wanafunzi wanachunguzwa kabla ya kupewa viza, hawajakuwa wakichunguza hivi karibuni kuhakikisha kwamba wamerudi nchini mwao.Imekuwa vigumu kujua idadi ya wale wanaorudi na wale wanaoishi Uingerza kinyume cha sheria. Idara ya uhamiaji inasema kwamba itakuwa vigumu sana kuvunja sheria za uhamiaji siku zijazo. Mnamo mwaka 2011, Idara hio itakuwa na technolojia ya kipekee duniani kuwachunguza watu wakiingia na kutoka Uingereza.

Idara hii imeanzisha vikwazo mbalimbali ambavyo wanafunzi wengi kutoka nchi za kigeni wanasema ni vikali mno. Mwaka uliopita mwezi Machi, Idara ya uhamiaji ilibadilisha taratibu ambazo wanafunzi kutoka nchi zingine hutumia kuomba viza za kuja Uingereza na kuanzisha mfumo ujulikanao kama Tier 4 Points based system.

Katika mfumo huu, vyuo vyote vya elimu ya juu ni lazima vijiandikishe katika idara ya uhamiaji. Vikitimiza mahitaji yote, vitapewa leseni ya kuwaleta wanafunzi kutoka nchi mbalimbali hapa Uingereza. Wanafunzi nao wanahitajiwa kuwa na pointi arubaini ndio watapewa viza. Wanafunzi watashinda pointi thelathini wakipewa barua ya kuomba viza kutoka chuo ambacho kimesajiliwa. Watashinda pointi kumi kama watakuwa na karo yote na pesa za matumizi za mwaka mmoja.

Wakitaka kuongezea mda wa viza zao wakiwa Uingereza, watahitajiwa kuonyesha kwamba wamekuwa na kiasi cha pauni 800 kila mwezi, kama chuo chao kiko mjini London na pauni 600 kila mwezi kama chuo chao kiko nje ya mji wa London.

Kabla ya kuongezewa mda wao kama wanafunzi, wale wanaoishi mjini London watahitajika kuonyesha kwamba kiasi cha £ 1600 kimekuwepo kwenye akaunti yao ya benki kwa mda wa siku 28. Wale wanaoishi nje ya mji wa London, watatakiwa kuonyesha wamekuwa na kiasi cha £ 1200 kwenye akaunti yao ya benki kwa mda wa siku 28.

Wanafunzi watakaopewa fursa kufanya kozi za muda mfupi wataruhusiwa kufanya kazi kwa masaa kumi kila wiki lakini kama wanasomea shahada, wataruhusiwa kufanya kazi masaa 20.

Wanaopinga hatua hii wanasema vikwazo hivi havijafanikiwa. Dr. Zakir Hussein, mkuu wa chuo cha London Trinity , anasema hivi vikwazo vimefanya wanafunzi wengi kuja Uingereza wakiwa hawawezi kuzungumza Kiingereza, wengi wao wakitoka bara la Asia.

Idara ya uhamiaji Uingereza imesimamisha kwa muda uombaji wa viza kutoka kaskazini mwa India, Nepal na Bangladeshi. Walichukua hatua hii kufuatia kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi walioomba viza eneo hilo kutoka 2,000 mwaka 2008 hadi 13,500 mwaka uliopita. Mabadiliko haya yatawaathiri vibaya wenye vyuo ambavyo havitoi shahada.

Jeremy Oppenheim ambaye ni mkuu wa mfumo wa Tier 4 Point based amesema kwamba kuanzia mwezi Machi mwaka huu, idara ya uhamiaji itawapa viza wanafunzi watakaopata nafasi kwenye vyuo ambavyo vitatoa shahada na zaidi . Mfumo huu utamaliza mafunzo yote ambayo wanafunzi hawatapewa shahada.

David Game, mkuu wa muungano wa vyuo wa David Game group of colleges, amesema kama serikali ya Uingereza itafuata sera hii kwa makini, basi utakuwa mwisho wa vyuo kama vyake. Kama idara ya uhamiaji itachukua hatua hiyo, David anasema yeye ataacha nchi yake na kuanzisha vyuo vya elimu ya juu nchi zingine.


Soma Zaidi ...

MAMA NA MTOTO WAKE WAULIWA PEMBA

Mtu mmoja Mwajuma Sahare Amour (25) na kitoto chake kichanga cha miezi (6) wameuwawa kikatili juzi usiku baada ya mama huyo kukakwa katwa na visu katika sehemu tisa katika mwili wake.

Mama huyo alipata mkasa huo baada ya mwanamme mmoja anaedaiwa kuwa alikuwa ni Mpenzi wake aliyetambulika kwa jina la Fadhili Yussuf (25) mkaazi wa Ndooni – Fundo mkoa wa kaskazini Pemba kumkata marehemu huyo katika sehemu ya tumbo ambapo alama sita zote zilikuwa katika tumbo leke na sehemu nyengine za mapajani na mkononi.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka kwa Sheha wa Shehia ya Fundo, Khamis Abeid zinasema kuwa mkasa huo ulitokea siku ya tarehe juzi majira ya saa 5.30 mchana, kijijini hapo baada ya wapenzi hao ambao walikuwa wakiishi kama mke na mume baada ya kutokea ugomvi wa kugombania mtoto

Marehemu ni Mwajume ni mzaliwa wa Kisiwa cha Fundo hapo hapo kisiwani Pemba na mtuhumiwa wa mauaji hayo Yussuf ni mzaliwa mkoa mmoja kutoka Tanzania bara.

Katika mkasa huo pamoja na kumkata mpenzi wake kwa kisu na kumsababishia Mwajuma kutokwa na damu nyingi mwilini mwake na hatimae kupoteza maisha pia aliamuwa kukinyonga kichanga hicho ambaco nacho kilipoteza maisha hapo hapo.

Kamanda wa polisi mkoa wa kaskazini Pemba Yahya Bugi hajapatikana kuthibitisha vifo hivyo vya mama na mtoto baada ya simu yake ya kiganjani kuita bila ya kupokewa.

Baada ya tukio hilo ambalo ni kubwa kufanyika kisiwani Pemba, Mtuhumiwa huyo Fadhil Yussuf, alinusurika kufa baada ya wananchi wenye hasira kutaka kumuuwa nay eye baada ya kutoka nje alipata kipigo kikubwa kutoka kwa majirani wa nyumba hiyo iliyotokea mauaji hayo ambayo yalianzia na ugomvi.

Mtuhumiwa huyo alilazimika kukimbizwa haraka katika hospitali ya Wete baada ya watu wenye hasira kumvamia na kumpiga ambapo hivi sasa amelazwa na kupatiwa matibabu huku akikabiliwa na kesi ya kuuwa kwa makusudi iwapo atatoka hospitalini hapo.

Hili ni tukio la kwanza kutokea katika Kisiwa cha Pemba la kuuliwa mama na mtoto wake pamoja kutokana na magomvi ingawaje mauwaji ya kuwania mpenzi yameshatokea mara kadhaa ksiwani hapo.
Soma Zaidi ...

TIMU YA TAIFA YA WANAWAKE YA SAUDI ARABIA


Soma Zaidi ...

KAZI IPO

Soma Zaidi ...

MARUBANI WA LUTHANSA WAGOMA

Shirika la ndege la kitaifa la Ujerumani, Lufthansa, limelazimika kusitisha safari zake baada ya marubani wake wote 4,000 kuanza mgomo wa siku nne kuhusu mishahara na usalama wa kazi zao.

Shirika hilo limesimamisha zaidi ya safari 3,000 za ndege zao. Msemaji wa shirika hilo Klaus Walther amesema mgomo huo utailetea kampuni hasara ya zaidi ya dola milioni 136.

Mgomo huo sasa unamanisha kutakuwa na msongamano wa abiria huku safari nyingi za ndege Barani Ulaya, zikicheleweshwa.

Chama cha marubani hao, Cockpit, kimesema kinataka wanachama wake kupewa nyongenza ya mshahara ya asilimia 6.3.

Pia kinataka Lufthansa kuwahakikishia marubani wake kuwa hawatapoteza kazi wakati ambapo kampuni hiyo itaanza kutumia makampuni mengine ya ndege kutoa baadhi ya huduma zake.

Vilevile chama hicho kinataka kupewa nafasi ya kuchangia zaidi katika maamuzi yanayofanywa na kampuni hiyo. Hadi sasa pande hizo mbili hazijaafikiana kufanya mazungumzo, lakini Klaus Walther anasema Lufthansa iko tayari kufanya hivyo.

Lufthansa inatarajiwa kufutilia mbali safari 800 za ndege kila siku, au theluthi mbili za ratiba yake. Waziri wa Usafiri wa Ujerumani Peter Ramsauer ameonya kuwa mgomo huo utaathiri kwa kiasi kikubwa uchumi wa Ujerumani na amejitolea kuwa mpatanishi wa mzozo huo wa malipo. Soma Zaidi ...

Sunday, February 21, 2010

WAZIRI MKUU WA UHOLANZI BALKENENDE AWASILISHA BARUA YA KUJIUZULU

Waziri Mkuu wa Uholanzi, Jan Peter Balkenende amewasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa Malkia Beatrix wa nchi hiyo. Serikali ya muungano ya nchi hiyo imevunjika baada ya vyama viwili vikubwa kushindwa kukubaliana iwapo wawaongezee muda wanajeshi wake waliopo nchini Afghanistan.

Jumuiya ya Kujihami-NATO ilitoa ombi kwa Uholanzi la kuwaongezea muda wanajeshi wake walioko nchini Afghanistan hadi mwezi Agosti mwaka ujao.

Balkenende jana alitangaza kuwa serikali hiyo ya muungano iliyokaa madarakani kwa miaka mitatu imevunjika, baada ya mazungumzo ya muda wa saa 16 ya kuikoa serikali kumalizika bila ya mapatano yeyote. Kwa sasa Uholanzi ina wanajeshi 2,000 nchini Afghanistan chini ya vikosi vya kimataifa vya ISAF vinavyoongozwa na NATO. Soma Zaidi ...

Saturday, February 20, 2010

MNARA WA MSIKITI WAANGUKA NA KUUA WATU MOROCCO

Wafanyakazi wa huduma za uokoaji katika mji wa Meknes nchini Morocco wamekuwa wakiendelea na utafutaji wa manusura kufuatia kuanguka kwa mnara wakati wa swala ya Ijumaa.
Kwa uchache watu thelathini na sita waliuwawa na wengine zaidi ya sabini walijeruhiwa .

Inaarifiwa kuwa watu wengine zaidi wamefukiwa chini ya kifusi cha mnara huo.

Baadhi ya waokoaji wamekuwa wakijaribu kuwafikia manusura wakitumia mikono yao kwa sababu mashini kubwa na nzito haziwezi kupita kwenye barabara finyu za mji huo wa kale.

Maafisa walisema siku kadhaa za mvua kali ziliathiri mnara huo uliojengwa karne kadhaa zilizopita katika mji wa kihistoria wa Meknes.
Soma Zaidi ...

WALIONUSURIKA MAUAJI MUSOMA WASIMULIA

Baadhi ya majeruhi katika tukio la mauaji ya kinyama ya watu 17 katikati ya wiki hii katika Manispaa ya Musoma, mkoani Mara wamesema wauaji walikuwa wamejiandaa na inaonekana walikuwa wanawafahamu kila mmoja.

Aidha wamesema wauaji waliamini hata wao wamekufa.

Moris Mgaya (40), aliyepoteza mke na watoto wake watano katika mauaji hayo, alisema wauaji walikuwa wanamfahamu vizuri.

Akizungumza kwa shida kitandani katika moja ya wodi za Hospitali ya Mkoa wa Mara mjini hapa, Mgaya alisema wauaji walikuwa wakimjua vizuri kwa kuwa walimtaja kwa majina yake likiwemo lile lisilojulikana na wengi la Susi (kunguni) wakati wakifanya mauaji hayo nyumbani kwake.

Katika tukio hilo mke na watoto wa Mgaya waliuawa kwa kucharangwa mapanga huku yeye mwenyewe akiachwa na majeraha makali, kutoka kiunoni hadi miguuni.

Mgaya alisimulia kuwa wauaji hao ambao alishindwa kuwatambua kutokana na kuvalia makoti makubwa na kutumia tochi waliyoitumia kuwamulika, walimtaka atoe pesa na aliposema hana walimtaja kwa jila lake la Susi na kumwambia kuwa watamuua endapo hatatoa pesa hizo. Alisema kuwa wauaji hao walichukua fedha taslimu Sh. 200,000 alizokuwa amezihifadhi sandukuni na zingine Sh. 50,000 alizoweka katika suruali yake aliyokuwa ameitundika katika kamba kabla ya kulala.

Akizungumzia kuhusu taarifa za mkewe na mtoto wake waliokuwa katika chumba kimoja, Mgaya alisema kuwa hadi sasa bado hajaambiwa kama mkewe na mtoto wake walifariki dunia katika tukio hilo la mauaji lililohusisha jumla ya nyumba tatu za wana ndugu wa ukoo mmoja.

"Hadi sasa sijaambiwa kama mke na mtoto wangu walifariki dunia katika tukio hilo, bado wamenificha ingawa mimi nahisi kuwa walishakufa," alisema Mgaya huku akifuta machozi kwa kutumia kitambaa alichokuwa amekishika mkononi.

Naye majeruhi mwingine, Maximilian Robert (20), ambaye amelazwa wodi moja na Mgaya, alisema kuwa alikatwa mapanga katika nyumba nyingine ambayo alikuwa amelala yeye, bibi yake na mtoto mwingine mdogo.

Robert alisimulia kuwa bibi yake alikatwa mapanga na kuuawa, na kwamba yeye alinusurika baada ya wauaji kumkata mapanga begani na mkononi na kisha kumwacha wakidhani kuwa alikuwa ameshafariki.

Jumla ya watu 17 waliuawa katika tukio hilo lililotokea usiku wa kuamkia Jumatatu, mbapo familia zilizokumbwa na tukio hilo na idadi ya watu waliouawa ikiwa katika mabano ni ya Mzee Kinguye (8), Moris Mgaya (6), na familia ya mzee Mgaya Nyarukende (3).

Akizungumza katika Hospitali ya Mkoa wa Mara jana, Mganga Mkuu Mfawidhi wa hospitali hiyo, Benadecto Mwijarubi, alisema kuwa majeruhi hao ukiondoa Maria Kawawa, hali zao zinaendelea vizuri.

Mwandishi wa habari hizo alipomtembelea Maria, alishindwa kuongea naye baada ya kumkuta akiwa bado katika maumivu makali kitandani mwake huku akiwa amefungwa bandeji kichwani na sehemu nyingine za mwili pamoja na kufungwa bandeji (pop) katika mkono wake wa kushoto.

Jeshi la Polisi mkoani hapa limesema kuwa tayari linawashikilia watuhumiwa sita kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo, huku Waziri wa Mambo ya Ndani, Laurence Masha, aliyefanya ziara ya mkoani hapa juzi kwa ajili ya kufuatilia tukio hilo akisisitiza kuwa wote walioshiriki katika mauaji hayo lazima wakamatwe na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Waziri Masha aliyasema hayo juzi alipowatembelea wafiwa na baadaye majeruhi katika Hospitali ya Mkoa wa Mara mjini hapa.

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Mstaafu Enos Mfuru, amekuwa akiwahimiza wananchi kutoa taarifa zitakazowezesha kukamatwa kwa watuhumiwa kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Robert Boaz, tangu kutokea kwa mauaji hayo amekuwa akisisitiza kuwa Jeshi la Polisi limejipanga katika maeneo yote ya mkoa huo kufanya msako wa kuwatia mbaroni watu waliohusika na tukio hilo ambalo limeandika historia mkoani humo.
Soma Zaidi ...

SERIKALI YA MUUNANO YA UHOLANZI YAVUNJIKA

Serikali ya muungano ya Uholanzi imevunjika baada ya vyama viwili vikubwa kushindwa kukubaliana endapo wawaondoe wanajeshi wake nchini Afghanistan au la mwaka huu kama ilivyopangwa.

Baada ya mazungumzo yaliyofanyika majira ya usiku mjini The Hague pamoja na baraza la mawaziri, Waziri Mkuu wa Uholanzi Jan Peter Balkenende ametangaza kuwa serikali ya nchi hiyo imeshindwa.

Baraza la mawaziri limekuwa likijadili ombi lililotolewa na Jumuiya ya Kujihami-NATO kwa Uholanzi kuwaongezea muda wanajeshi wake walioko nchini Afghanistan hadi mwezi Agosti mwaka ujao wa 2011.

Chini ya serikali ya sasa, wanajeshi 2,000 wa Uholanzi walioko katika vikosi vya NATO vinavyoongozwa na ISAF nchini Afghanistan wanatakiwa kuondoka katika jimbo la Uruzgan mwaka huu.
Soma Zaidi ...

TIGER WOODS AMUANGUKIA MKEWE

Mcheza gofu mashuhuri duniani Tiger Woods katika mkutano wa waandishi wa habari amemuomba radhi rasmi mkewe kwa kumuendea kinyume.

Mcheza gofu huyo anayeshikilia nafasi ya kwanza kwa ubora duniani, alikuwa akizungumza hadharani kwa mara ya kwanza tangu kashfa iliyokuwa imegubika maisha yake ya faragha kuibuka mwezi wa Novemba mwaka jana.

Woods Mmarekani mwenye umri wa miaka 34 alikuwa akihutubia kundi dogo la marafiki, wacheza gofu wenzake na jamaa wa karibu mjini Florida.

Mcheza gofu huyo aliyewahi kushinda mataji makubwa mara 14 alisema hakuwa mwaminifu, alikuwa na uhusiano na wanawake wengine na alitembea nje ya ndoa. Alikiri kitendo hicho ni cha fedheha na hakikubaliki.

Aliendelea kukiri, kwa vitendo vyake amemuumiza mkewe, wanawe, mama yake, familia ya mkewe, mfuko wake na watoto wote duniani waliokuwa wakimpenda.

Woods alisema kuna uwezekano wa kurejea kucheza tena gofu mwaka huu, lakini akasema bado hajapanga tarehe na akaongeza atarejea tena kupata nasaha na ushari siku ya Jumamosi.

Alisema ni vigumu kukiri lakini anahitaji msaada.

Tiger Woods alifafanua kwamba kwa siku 45 tangu mwishoni mwa mwezi wa Desemba hadi mapema mwa mwezi wa Februari, alikuwa akipatia matibabu ya kitaalamu ya kumuweka sawa na dhoruba hiyo ya maisha aliyokumbana nayo.

Alisema anasafari ndefu katika hilo lakini amekamilisha hatua ya awali ya safari hiyo kwa njia sahihi.
Soma Zaidi ...

Friday, February 19, 2010

CONGO YAFUNGA MAKANISA NA VILABU VYA POMBE MJINI KINSHASHA

Makanisa manane pamoja na vilabu vya kuuza pombe kadhaa vimefungwa mjini Kinshasa (DRC) kwa kuhusika na kelele za usiku na mchana.

Hatua hiyo iliyochukuliwa na serikali imelalamikiwa na wafuasi wengi wa makanisa hayo ambao wamehisi kwamba viongozi walitakiwa kupiga marufuku kelele na sio kufunga makanisa.

Kumejitokeza jijini Kinshasa miaka ya hivi karibuni mfumuko wa makanisa ya kujitegemea ambayo yanajiita makanisa ya muamko ama " wake up churches." Taarifa kamili na mwandishi wetu Saleh Mwanamilongo. Soma Zaidi ...

JESHI LATWAA MADARAKA NIGER

Jeshi nchini Niger limethibitisha kuwa limetwaa madaraka na limetangaza kuivunja serikali ya nchi hiyo. Pia Rais Mamadou Tandja pamoja na baraza lake la mawaziri wanashikiliwa.

Msemaji wa wanajeshi waliotwaa madaraka, Kanali Goukoye Abdul Karimou, alijitokeza katika televisheni ya nchi hiyo kutangaza mapinduzi hayo.

Kufuatia mapinduzi hayo ya kijeshi huko Niger, Umoja wa Afrika umelaani hatua hiyo, ambapo Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Afrika, Jea Ping, amesema kuwa wanaifuatilia kwa karibu hali nchini humo.

Mapinduzi hayo yamefanyika huku kukiwa na hali tete ya kisiasa, baada ya Rais Mamadou Tandja kuongezewa muda wa kukaa madarakani .

August mwaka jana, Rais Tadja alilivunja bunge pamoja na mahakama ya katiba, ili kushinikiza mabadiliko ya katiba yatakayomruhusu kuweza kuwania tena urais hata baada ya kumaliza vipindi viwili vya miaka mitano mitano.

Na taarifa za hivi punde zinasema kuwa wanajeshi waliyotwaa madaraka wamemtangaza kiongozi wao kuwa ni Salou Djibo. Soma Zaidi ...

Thursday, February 18, 2010

ANNAN AWAASA KIBAKI NA RAILA

Kundi la viongozi mashuhuri wa Muungano wa Afrika limeelezea wasiwasi wake kuhusu mzozo wa kisiasa unaoendelea nchini Kenya, na kusema kuwa huenda ukaathiri utekelezwaji wa mkataba wa kitaifa wa serikali ya muungano.

Katika taarifa yao, kundi hilo linalo-ongozwa na aliyekuwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa na mpatanishi mkuu katika mzozo nchini Kenya, Kofi Annan, limewataka rais Mwai Kibaki na waziri mkuu Raila Odinga wafanye mashauriano ili kuutatua mzozo huo.

Mvutano wa hivi punde kati ya Rais Kibaki na waziri mkuu Raila Odinga ulianza siku ya jumaapili, wakati Bw Kibaki alipobatilisha uamuzi wa awali wa Bw Odinga wa kuwasimamisha kazi mawaziri wawili waliohusishwa na kashfa za ufisadi.

Kufuatia hatua hiyo, Bw Odinga alitoa wito kwa Bw Annan kuja kuutatua mzozo huo.

Lakini taarifa ya jopo hilo la watu mashuhuri imemnukuu Bw Annan akitoa wito kwa waakilishi wa pande mbili walioshiriki katika kubuni mwafaka wa serikali ya muungano kutilia mkazo kutekeleza ajenda za mwafaka huo.

Jopo hilo limeelezea wasi wasi kwamba huenda mzozo uliopo ukatatiza juhudi za kupambana na ufisadi katika serikali ya Kenya.

Awali Rais Kibaki alisema hakuna mzozo wowote katika serikali
Soma Zaidi ...

SAUDI SENTENCED FOR SIX WIVES

JEDDAH: A court in Al-Masarha in Jizan region has sentenced a 56-year old Saudi employee of the Commission for the Promotion of Virtue and Prevention of Vice (the Hai'a) to 120 lashes for being married to six wives at the same time, 20 lashes per wife.

He has been ordered to memorize two chapters of the Holy Qur'an. The court also banned him from traveling abroad for five years and delivering sermons or leading prayers in mosques. The accused had claimed he did not know it was against Islamic law to have more than four wives at the same time. He told the judge that he had no education beyond elementary school.

He faced the possibility of being stoned to death, a sentence applied in Islam against married men and women for adultery. Under Sharia rules, a man may marry up to four wives. However, the judge in the case, Sheikh Salman bin Yahya Al-Wadaani, said there was insufficient evidence to apply the Had Al-Zina (the sentence for adultery), according to Al-Watan daily.

The man was charged originally in June 2008 after he was reported for having three Saudi and three Yemeni wives. It also emerged during investigations that two of his Yemeni wives were resident illegally in the Kingdom.

The judge said there would be a separate case against him for marrying foreign women without official consent. No Saudi man or woman wishing to marry a foreigner may do so without approval from the Ministry of Interior. Soma Zaidi ...

ZANZIBAR NJEMA

Soma Zaidi ...

MUAFAKA - ZANZIBAR

Naikumbuka hadithi ya mzee Haji. Alikuwa mzee wakujipenda sana, akivaa nadhifu kabisa, Kanzu, kofia, koti na makbadhi ilikuwa kawaida yake, Akipenda sana kula hasa pilau na biriyani. Shughuli yake kubwa ilikuwa kutegeya nje ya sehemu za kukodisha masufuria, sahani, majamvi n.k.

Liondokapo rikwama na mizigo hiyo basi yeye hujifanya mmoja wa washindikizaji wa mzigo. Wanapofika penye shughuli hujifanya bizi katika matayarisho. Atatandika majamvi na kujifanya kama mmoja ya wahusika, almuradi aondoke hapo kashiba, hii ilikuwa kawaida yake ya kila siku.

Siku mmoja likaondoka rikwama limejaza majamvi. Mzee Haji akaliandama, bizi kusukuma. Kilima cha kwerekwe kapandisha na nyimbo za hamasa kuimba, Safari iliishiya Fuoni, mzee Haji
taabani kwa uchofu.

Majamvi yakashushwa. Mzee Haji akashiriki kikamilifu hata kutandika akijuwa ya kuwa biriyani iko njiani. Mara yakaletwa magunia ya karafuu, Mzee Haji kashangaa. Viiipi hapa? Zikaanza kutandazwa karafuu majamvini, mzee Haji kakosa subra, matusi jujuu. Analaumu-kwa nini asiambiwe mapema.

Maridhiano Zanzibar ilikuwa bashraf tu. Nyimbo hasa wameiimba Dodoma. Serikali shirikishi baada ya uchaguzi, kura za maoni baada ya uchaguzi, sasa sijui baina ya uchaguzi na kura za maoni itakuwepo serikali ipi? na hasa lakujiuliza ni hiyo kura ya maoni ni lini? Labda September 2015. Laa-haulla! Sijui CUF itakula biriyani au tuta anika karafuu.
Mwenye Enzi Mungu atusaidie.
Soma Zaidi ...

GIZA ZANZIBAR LASABABISHA NDEGE YA NAHODHA KUKWAMA KUTUA

Ndege ya Serikali ikiwa imembeba Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha, imeshindwa kutua katika Uwanja wa Kimataifa wa Zanzibar kutokana na giza baada ya jenereta ya kufua umeme wa dharura kuharibika.

Waziri Kiongozi alikuwa akitokea mkoani Dodoma kuhudhuria kikao cha Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM akiwa amefuatana na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Zanzibar, Shawana Buheit Hassan ambaye pia ni mjumbe wa NEC.

Taarifa zilizopatikana zimeeleza kwamba ndege hiyo iliondoka juzi saa 12:00 jioni mjini Dodoma na ilitarajia kutua saa 1:00 usiku katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege Zanzibar.

Hata hivyo, kutokana na uwanja huo kuwa gizani, ndege hiyo ilizunguka mara kadhaa katika anga ya Zanzibar na baadaye kwenda kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Meneja wa Mamlaka ya Usalama wa Usafiri wa Anga Zanzibar, Said Sumri, alithibitisha kuwa ndege hiyo ilishindwa kutua Zanzibar ikiwa na wajumbe wa NEC.

Hata hivyo, Sumari hakutaka kuingia kwa undani zaidi juu ya suala hilo kwa madai kwamba si msemaji.

Lakini vyanzo vya habari katika tukio hilo vilieleza kwamba ndege hiyo ililazimika kuzunguka katika anga ya Zanzibar na baadaye kurejea Dar es Salaam na kutua katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

“Tulilazimika kulala Dar es Salaam baada ya ndege yetu kushindwa kutua kutokana na tatizo la giza kufuatia jenereta ya uwanja kuharibika,” chanzo kimoja cha habari kilikaririwa kikisema.

Hata hivyo, abiria wote waliokuwemo katika ndege hiyo baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam, walilazimika kujihudumia gharama za hoteli na kulazimika kusafiri Zanzibar siku iliyofuata na kuwasili Zanzibar saa 4:00 asubuhi jana.

Baadhi ya viongozi waliokuwemo ndani ya ndege hiyo ni wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Salmin Awadh Salmin (Magomeni), Ali Suleiman Ali (Kwahani), Thuwaiba Kisasi (Viti Maalum), Zainab Shomari (NEC), Issa Ahmed Othman (NEC) na wasaidizi kadhaa wa Waziri Kiongozi.

Lakini Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege Zanzibar, Malik Mohammed Hanif, alisema ndege hiyo ilishindwa kutua Zanzibar kwa vile uwanja wa ndege upo katika matengenezo.

Alisema tangu kuanza matengenezo katika uwanja huo, umekuwa ukifungwa kuanzia saa 1:00 usiku ili kuweka mazingira ya utulivu wakati mafundi wakitekeleza majukumu yao.

“Ndege ilishindwa kutua kutokana na matengenezo yanayoendelea katika uwanja huo na sio kweli kama jenereta liliharibika ghafla," alisema Mkurugenzi huyo.

Zanzibar haina huduma za umeme tangu Desemba 10, mwaka jana na kuathiri sekta za kiuchumi na kijamii, baada ya waya unaopokea umeme kutoka Tanzania Bara kulipuka katika kituo cha Fumba Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Kutokana na tatizo hilo, taasisi mbalimbali zimekuwa zikitumia umeme wa dharura wa majenereta, ikiwemo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar ambao hivi sasa upo katika matengenezo makubwa yanayofanywa na Kampuni ya Sogea Satom ya nchini Ufaransa.

Uwanja huo wa ndege unatarajiwa kuongezwa urefu kutoka mita 2,662 hadi 3,022 na mradi huo unatarajiwa kukamilika Agosti, mwaka huu. Soma Zaidi ...

Wednesday, February 17, 2010

BABA NA MWANA

Nawaz akiwa kwenye vazi la Darzi na kiuwa na hivi ndivyo alivyotoka siku ya kisomo chake,
Soma Zaidi ...

ZIMBABWE HAITISHWI NA VIKWAZO ZAIDI

Chama tawala cha rais Robert Mugabe wa Zimbabwe; ZANU-PF, kimepuuzilia mbali kurefushwa muda wa vikwazo vilivowekwa na nchi za Umoja wa Ulaya, kikidai ni njama ya ushirikiano na chama tanzu kliomo katika serikali ya muungano ya nchi hiyo.

Msemaji wa ZANU-PF, Rugare Gumbo, amesema hawana wasiwasi na kurefushwa muda wa vikwazo hivyo, na kwamba wataendelea na jitihada zao za ukombozi. Alisema ni dhahiri shahiri watajikomboa wenyewe.

Bwana Gumbo alikilaumu chama cha Movement for Democratic Change, MDC, kinchoongozwa na waziri mkuu, Morgan Tsvangirai, kwa kuunga mkono vikwazo hivyo dhidi ya rais Mugabe na marafiki wake wengine wa kisiasa mia moja.

Mwezi Septemba mwaka jana, Umoja wa Ulaya ulituma wajumbe wake nchini Zimbabwe na katika tathmini yao hawakuridhishwa na mwelekeo wa mabadiliko. Shirika la kutetea haki za kibinaadam la Human rights Watch lilipendekeza kuongezwa muda wa vikwazo kutokana na visa vya kukiukwa haki za binadamu, vikiwemo mauaji ya wakereketwa wa chama cha upinzani.
Soma Zaidi ...

ASKARI KANZU NA WENGINE WANNE KUTUPWA JELA MIAKA 25

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Ruvuma, imewahukumu kifungo cha miaka 25 jela watu watano akiwemo aliyekuwa akari kanzu a jeshi la polisi Kituo cha Mbamba Bay, Koplo Dustan Mweta (25) kwa kosa la kuvunja na kuiba briefcase iliyokuwa na camera yenye thamani ya dola 1,350 za Marekani Euro 800, simu za mikononi tano na Sh. 1,510,000 vyote kwa pamoja vikiwa na thamani ya Sh. 5,040,000 mali ya Emanuel Masanche mmiliki wa Nyasa View Hotel Mbamba Bay.

Waliohukumiwa kifungo hicho ambapo kila mmoja atatumikia miaka mitano ni mhudumu wa Hoteli ya Nyasa View, Susana Kapinga (25), John Yona (30), mkazi wa Mbamba Bay, Gallus Mchimbi (36), mkazi wa Mbinga mjini, Joseph Mbunda na Koplo Mweta.Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mfawidhi a Mahakama ya Mkoa, Baptist Mhelela, alisema Mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na mashahidi wanne.

Hakimu Mhelela alisema kila mshtakiwa atatumikia kifungo cha miaka mitano jela kutokana na ushahidi ambao umeonyesha kuwa ulikuwa na mazingira ya wizi uliotokea kwenye Hoteli hiyo.

Alisema wahtakiwa wamepewa adhabu hiyo ili liwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia mbaya kama hiyo na haa ikizingatiwa kuwa askari polisi imeonekana alihusika kupanga njama za kuvunja na kuiba.

Awali, ilidaiwa na mwanasheria wa Serikali kuwa Desemba 25, mwaka juzi, katika mji mdogo wa Mbamba Bay kwenye Hoteli ya Kitalii ya Nyaa View ambayo ipo kando kando ya ziwa Nyasa, washtakiwa wote watano walipanga njama na kuvunja na kuiba briefcase ambayo ilikuwa imehifadhiwa kwenye moja ya vyumba vya Hoteli hiyo na kuiba vitu na fedha hizo.

Hata hivyo, washtakiwa kwa mara ya kwanza walikana mashitaka hayo na kwamba kesi iliendelea kusikilizwa hadi ilipofikia hukumu hiyo.
Soma Zaidi ...

NEC INA AJENDA MBAYA KWA ZANZIBAR - MZANZIBARI ZINDUKA

Kila kunapo kucha hali ya Zanzibar inabadilika kutokana na joto la uchaguzi hapo mwezi oct. Vile vile kuna wengine wana furaha kutokana na maridhiano ya kisiasa yaliofikiwa visiwani humo kwamba yanaashiria njozi njema.

Lakini kuna upande mwengine, hali imeshaaza kuwa ya wasi wasi wakifikiria yale masahibu yanayowakuta kila baada ya miaka mitano.

Mara nyingi kwa nchi zenye demokrasia ya kweli,wananchi wake huwa wanapendelea kipindi kama hichi. Utaona wanaopigania uongozi wakielezea mipango yao au sera zao kwa wananchi juu ya maendeleo na huduma nyengine za kijamii. Kwa upande wa Zanzibar hali sio shuari kwani huu ni wakati wa majonzi na adhabu kubwa kwa wanajamii.

Hatuna budi kuwapongeza wale wote ambao wanachukua juhudi za mak-sudi kutaka kuviepusha visiwa hivi na balaa inayoandaliwaa huko mbele na Tume ya uchaguzi (ZEC).

Ni ukweli usioweza kupingika kwa mtu yeyote, kwamba upepo wa mabadiliko umevuma Zanzibar, na tayari watu wanajiandaa kuona Zanzibar mpya, kwani wako hoi bin Taaban kimaisha na vurugu zisizo msingi za kila siku kwa maslahi ya makaburu wachache wasiotakia mema visiwa hivi.

Ingawaje kama nilivyoeleza katika nakala zilizopita kwamba wako wachache wasio ridhishwa na hali ya matokeo mazuri ya maridhiano yalio jitokeza kati Maalim SEIF na MH. Abeid Aman. Watu hawa wanahaha kuona hali inatibuka na wao wanaendelea kuzifurahisha nyoyo zao na ndoto zisizokuwa na kikomo za madaraka na ving’ora.

Ili uchaguzi uwe huru na haki basi hauna budi kusimamiwa na chombo maalum na sio ZEC. Kwani tume inayoongozwa na Usalama wa Taifa, ndio chanzo cha fujo katika chaguzi zote zilizofanyika huko nyuma. Sasa iweje leo hii, wasimamie kura za maoni na uchaguzi wa visiwa hivi na wao ndio chanzo cha matatizo?

Nawatahadharisha wale viranja wote wanaoshabikia uonevu na uporwaji wa haki ya wazanzibar, kwamba kila kitu kina mwanzo na mwisho wake na mara hii wasitegemee kwamba itakuwa rahisi kama hivyo walivyozoea. Najua mazoea yana tabu lakini mpaka tabia ziwe zinalingana. Na tayari mwendo wa tume hauridhishi kabisa , kwani hawafanyi kazi kama tume huru na bali wanaongozwa na idara ya usalama wa Taifa sasa niambieni hapo jamani haki itatendeka ?

Tunakuomba Rais Kikwete hili uliangalie kwa mapana kwani bila kulifanyikia kazi historia katika uongozi wako itakumbwa na doa jeusi kama alivyofanya Benjamin Mkapa katika uongozi wake.

Licha ya ubadhirifu wa fedha na kashifa ya rushwa katika uongozi wake pia damu ya wazanzibar ilimdondokea yeye akiwa Amir Jeshi Mkuu kwa amri yake. Kikwete tunajua wewe ni muungwana hatutegemei kwamba utatufikisha huko.

Tulio wengi Zanzibar hatuna imani na tume hii. Ni ajabu na vichekesho kuona kwamba hapo zamani Wazanzibar wakiibiwa kwa kura na kubadilishwa matokeo, kama hivyo haitoshi mara hii hata kuundikishwa basi wanakoseshwa haki yao sasa hii tume tuielewe vipi?

Huyu anaenyimwa hakli ni mzanzibar halisi, nawauliza ZEC muna agenda gani kwaWazanzibar? Musijenge zana kuwa hali itakuwa shuari kama mutakataa matakwa yawalio wengi, jitayarisheni kwa kuwamaliza Wazanzibar kwa mtutu wa bunduki kama mulivyofanya huko nyuma.

Mungu libariki Taifa la zanzibar -Amini Soma Zaidi ...

WAFANYAKAZI WA SHIRIKA LA RELI WADAI MISHAHARA YAO

Wafanya kazi wa shirika la Reli Tanzania (TRL) walikusanyika katika makao makuu ya shirika hilo jijini Dar-es-salaam leo hii kwa ajili ya kudai mishahara yao Soma Zaidi ...

Tuesday, February 16, 2010

BANGO LINALOONESHA HISTORIA YA MSIKITI MKONGWE WA KIZIMKAZI DIMBANI


Soma Zaidi ...

MSETO WAWATESA WAPINZANI ZANZIBAR

Chama cha Wakulima Zanzibar (AFP) kimesema wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wale wa Chama cha Wananchi (CUF), walifanya makosa kupitisha hoja binafsi ya kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa, inayovitenga vyama vigine vya siasa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo-Zanzibar) jana, Mwenyekiti wa AFP, Soud Said Soud alisema chama chake kinaunga mkono kuwepo kwa serikali hiyo kwa sababu ndiyo ufumbuzi wa matatizo ya kisiasa ya Zanzibar.

Hata hivyo alisema muundo wake uliopitishwa na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi haufai, na serikali lazima isitishe utekelezaji wake hadi hapo marekebisho yatakapofanyika ikiwemo kuvipa nafasi vyama vingine kushiriki kuunda serikali hiyo.

Hata hivyo, alisema kwamba viongozi Zanzibar wasiwe wepesi wa kusahau historia ya kisiasa ya Zanzibar kwa sababu mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 yalifanyika baada ya Chama cha Afro Shirazi Party kuchoshwa na vitendo vilivyokuwa vikifanywa na vyama vya ZNP na ZPP, kutoshirikishwa katika serikali ya umoja wa kitaifa.

Alisema tayari chama hicho kimewasilisha barua maalumu serikalini kuitaarifu kuwa kina nia ya kufungua kesi mahakamani, kama ushauri wao hautozingatiwa ndani ya siku 20.


Soma Zaidi ...

AJALI MBAYA YA TRENI ILIYOTOKEA JANA BELGIUM

Soma Zaidi ...

Monday, February 15, 2010

JAMBAZI AUAWA BAADA YA KUPIGWA RUNGU NA MMASAI

Mtu mmoja aliuawa baada ya kupigwa rungu la kichwa na mmasai wakati majambazi walipovamia hoteli moja ya kitalii iliopo Uroa Zanzibar.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa kusini Unguja Augustino Ollomi tukio hilo lilitokea katika hoteli ya kitalii ya Samaki Lodge ambapo watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi kuvamia hoteli hio mara tu baada ya hoteli hio kufungwa, na wageni wote kuingia vyumbani mwao kwa kulala.

Majambazi hao walivunja mlango mkubwa wa hoteli hio na kumvamia mmiliki wa hoteli hio aliyejuilikana kwa jina Fabian ambae ni raia wa Itali.

Mmiliki huyo wa hoteli alipambana na majambazi hao kabla ya kupata msaada kutoka kwa polisi ambao waliokua wakifanya doria katika maeneo hayo.

Kamanda Ollomi alimtaja aliyefaki katika tukio hilo kua ni Hassan Mohammed Abdallah mwenye umri wa miaka 44 ambae alifariki baada ya kupigwa rungu la kichwa na mlinzi wa kimasai wakati jambazi huyo alipotaka kumnyang'anya silaha askari koplo ambae alitajwa kwa ina la Mohammed.

Katika tukio hilo pia askari wawili pamoja na jambazi mmoja walijeruhiwa, askari waliojeruhiwa ni pamoja na koplo Mohammed Salum ambae amejeruhiwa sehemu za kichwa na shingo pamoja na kamanda wa polisi wilaya ya kati ASP Juma Said ambae alijeruhiwa mkononi baada ya kuchinjwa kwa kiwembe na mmoja wa majambazi hao.

Polisi walifanikiwa kumkamata Abdallah Juma Faki mwenye umeri wa miaka 45 mkaazi wa Mwembe Makumbi ambae alijeruhiwa baada ya kupigwa na wananchi wenye hasira na kulazwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja. Soma Zaidi ...

MAFUNZO YAANZA VIBAYA KLABU BINGWA

Mabigwa wa soka kutoka Zanzibar timu ya Mafunzo jana walianza vibaya mashindano ya Klabu bingwa Afrika kwa kufungwa na timu ya Gunners kutoka Zimbabwe mabao mawili kwa moja. Soma Zaidi ...

KIBAKI ABATILISHA UAMUZI WA RAILA

Hali tete ya serikali ya muungano ya Kenya imeendelea kudhihirika huku Rais Mwai Kibaki akibatilisha uamuzi wa awali wa waziri mkuu Raila Odinga wa kuwasimamisha kazi mawaziri wawili kuhusiana na uchunguzi wa kashfa za ufisadi.

Awali Waziri mkuu Raila Odinga alitangaza kuwasimamisha kazi waziri wa kilimo William Ruto na waziri wa elimu Prof Sam Ongeri, akisema alifanya hivyo baada ya ripoti mbili za uchunguzi wa mashirika mawili tofauti kuonyesha kwamba mawaziri hao wanastahili kuchunguzwa zaidi.

Kashfa hizo zinahusu mahindi yanayosemekana kuuziwa wafanyabiashara kwa njia ya ufisadi badala ya kuwauzia wananchi, na nyingine ni kuhusu ubadhirifu wa mamilioni ya pesa zilizokusudiwa kugharamia elimu ya bure.

Taarifa kutoka Ikulu imeeleza kwamba Rais Mwai Kibaki amebatilisha uamuzi huo kwa kuzingatia kipengee cha mkataba wa serikali ya muungano, kinachohitaji kuwepo mashauriano na kiongozi wa chama kabla ya waziri yeyote kufutwa kazi.

''Kuondolewa kwa Waziri yeyote aliyeteuliwa na chama cha siasa katika serikali ya muungano utafanywa pale tu na baada ya mashauriano na makubaliano kimaandishi kwa kiongozi wa chama.'', taarifa hiyo ilisema.

Lakini Bw Odinga ameambia BBC kwamba kulingana na mwafaka wa serikali ya mseto , mashauriano yanahitajika tu katika kuteua au kumwachisha kazi waziri na sio katika kumsimamisha kazi.

Amesema alichokifanya yeye ni kuwaambia mawaziri wahusika kukaa kando ili uchunguzi ufanyike kuhusiana na kashfa hizo na kwamba hajamwachisha kazi waziri yeyote.

Bw Odinga amesema Rais Kibaki amevunja sheria na katiba kwa kubatilisha uamuzi wake.
Soma Zaidi ...

Sunday, February 14, 2010

CHERIE NA ZAM ZAM WAKISISITIZA UPENDO NDANI YA VAZI LA KANGA


Soma Zaidi ...

MKIMBIZI WA KIHOLANZI ATUHUMIWA UGAIDI NCHINI BURUNDI

Mkimbizi mmoja alieomba hifadhi ya ukimbizi nchini Uholanzi, alituhumiwa kuwa ni gaidi kutoka katika kikundi cha Al-Shabab baada ya kurudishwa Burundi na kudai kwamba yeye si mrundi bali ni Msomali.

Mtandao mmoja nchini Burundi ambao unaandika habari zake kwa lugha ya Kifaransa na Kirundi uliandika habari hizo baada ya wakimbizi kutoka Sweeden na Uholanzi kurudishwa burundi.

Habari kamili zinapatikana hapa kwa lugha ya Kifaransa

Soma Zaidi ...

Saturday, February 13, 2010

TANZANIA YAPELEKA MAJESHI YAKE SUDAN

Baadhi ya manajeshi wa jeshi la wananchi JWTZ wakipanda ndege siku ya Alkhmis usiku katika uwanja wa ndege wa Mwalim Julius Nyerere wakielekea Darfur nchini Sudan kwa ajili ya kulinda amani katika mji huo, Tanzania inatarajiwa kupeleka wanajeshi 600 katika mpango huo wa kulinda amani.
Soma Zaidi ...

ISMAIL JUSA AAPISHWA BUNGENI

Mbunge wa kuteuliwa kupitia chama cha wananchi CUF akipokea vitendea kazi baada ya kuapishwa rasmin bungeni mapema jana asubuhi
Soma Zaidi ...

HARUSI YA WANAUME YAVUNJWA MOMBASA

Polisi katika mtaa wa Mtwapa ulioko kaskazini mwa mji wa Mombasa nchini Kenya wamewakamata wanaume wawili waliokuwa wanajiandaa kuoana.

Afisa wa utawala katika eneo hilo George Matundura amesema wanaume hao walikuwa na pete tayari kufunga ndoa katika hoteli moja iliyoko Kikambala katika wilaya jirani ya Kilifi.

Raia pia wameripotiwa kuwakamata wanaume wengine kadha wanaodaiwa kushiriki mapenzi ya jinsia moja na kuwakabidhi kwa Polisi.

Ndoa za watu wa jinsia bora ni marufuku nchini Kenya, lakini sio jambo la kawaida wale wanaofanya hivyo kukamatwa.

Makundi ya Waislamu na Wakristo katika eneo hilo walifanya maandamano wakilaani kile walichokielezea kuwa tabia ya baadhi ya watu isiyokubalika katika eneo hilo la Mtwapa. Soma Zaidi ...

Friday, February 12, 2010

SALAAM ZA IJUMAA - SHAIRI

JUMA'A KAREEM!!

Wapendwa iwe ni ada Istawi Ukumbini
Iwe yetu kawaida Siku hii tupambeni
Au pawekwe kasida Waungwana nambieni
Kina kaka kina dada Fursa itumieni

Kuingia Ijumaa Furaha ziwe moyoni
Haitofaa hadaa Allah tumuogopeni
Sura zisije kunyaa Ukatiwa kaburini
Hakuna lakukufaa Utakuwa hasarani

Mikono juu kwa dua Jalali tumuelekeni
Tupate nyingi shufaa Ibada tuongezeni
Hakuna cha kuzubaa Hili tueke usoni
Machozi husaidia Pindi upo duniani

Watu wakikufukia Chozi litafaa nini
Ni bora kukuzindua Kuliko kukuacheni
Babengwa namalizia Itikieni amini
Tuombeni nyingi dua Ili tulale peponi.

Waislamu sote ukumbini, tutakieni kila la kheri

Maasalaam,

Babengwa Zanzibar Soma Zaidi ...

UINGEREZA NA RWANDA KUBADILISHANA WAFUNGWA

Makubaliano ya kukabidhiana wafungwa kati ya Rwanda na Uingereza yametiwa saini na waziri wa sheria wa Rwanda, Tharcis Karugarama na Balozi wa Uingereza nchini Rwanda, Nicolus Cannon Rwanda .
Makubaliano hayo yataruhusu watu waliohukumiwa na mahakama katika yoyote ya nchi hizo kutumikia kifungo nyumbani.

Rwanda ndiyo nchi ya pili ya kiafrika kutia saini makubaliano hayo na Uingereza, baada ya Uganda kusaini makubaliano kama hayo mwaka jana.

Wachambuzi wanasema Rwanda inataka kuonyesha jamii ya kimataifa kwamba inaweza kupokea watu waliohukumiwa na mahakama ya kimataifa ya Rwanda ambayo inasikiliza kesi za washukiwa wa mauaji ya kimbari ya mwaka 94.

Mahakama hiyo iliyo mjini Arusha, Tanzania, imekuwa ikikataa kuwakabidhi watu iliowahukumu kwa serikali ya Rwanda, ikidai kuwa mfumo wa gereza wa taifa hilo, hauwahakikishii haki wafungwa hao.

Soma Zaidi ...

BABU SEYA SASA KUMALIZIA MAISHA YAKE JELA

Ile nyota iliyoanza kung'ara Desemba 3, mwaka jana wakati Makahama ya Rufaa iliposikiliza sababu 15 za rufaa ya Nguza Viking 'Babu Seya' na wanawe watatu, jana imepotea kabisa baada ya mahakama hiyo kuamuru mwanamuziki huyo na mwanae, Johnson Nguza (Papi Kocha) kuendelea kutumikia kifungo cha maisha.

Mahakama hiyo pia imewaachia huru wanawe wawili, Nguza Mbangu na Francis Nguza ambao pamoja na Baba yao 'Babu Seya' walikuwa wakitumikia kifungo cha maisha jela, baada ya mwaka 2004 kukutwa na hatia ya makosa ya kudhalilisha watoto 10 wa kike wa shule ya msingi wenye umri kati ya miaka 6-10.

Wakili wa warufani hao, Bw. Mabere Marando alisema hukumu hiyo ya jopo la majaji Salum Massati, Mbarouk S. Mbarouk na Nathalia Kimaro inafunga kabisa hatua mbadala wanayoweza kuchukua 'Babu Seya' na 'Papi Kocha' ili kuwa huru tena.

"Kesi ikishasikilizwa na jopo la majaji watatu ni sawa na 'Full Bench' hakuna refrence 'rejea' isipokuwa kama rufaa ingesikilizwa na jaji mmoja, ninasikitika kwa hilo, lakini nashukuru kwa kuwa jamii iko upande wetu, pengine iko siku nao watasamehewa na kuachiwa," alisema Bw. Marando.

Hukumu hiyo ya rufaa ya jinai No. 56 ya mwaka 2009 ilizingatia utetezi uliotolewa na Bw. Marando kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu pamoja na Mahakama Kuu zilikiuka misingi ya sheria na kupuuza ushahidi wa wateja wake katika mashitaka hayo.

Kwa kuzingatia utetezi huo, mahakama hiyo iliwafutia mashitaka 9 warufani wote, likiwemo kosa la kulawiti kwa pamoja, huku ikiwakuta na hatia ya kubaka na kubaka kwa pamoja, warufani wawili, Babu seya na Papi Kocha, hivyo kuamuru waendelee na adhabu ya awali iliyotolewa na mahakama za chini.

Mahakama hiyo ilitaja sababu za kuwaachia huru Nguza Mbangu na Francis nguza kuwa ni kutokuwepo kwa ushahidi wa kutosha juu ya ushiriki wao katika udhalilishaji huo, na kuwa mahakama za chini hazikuzingatia utetezi wao kuwa hawakuwepo eneo la tukio siku iliyotajwa.

Aidha mahakama hiyo iliukataa utetezi wa 'Babu Seya' kuwa mahakama za chini hazikuleta mashahidi walioshuhudia akifanya vitendo hivyo, na kuwa asingeweza kubaka watoto katika nyumba iliyokuwa na watu wengine muda wote ukitumika kama ukumbi wa mazoezi ya bendi yake ya Achigo.

Mahakama ilisema kutokana na ushahidi wa watoto na wa mazingira ya eneo la tukio ni wazi kuwa 'Babu Seya' asingeshindwa kufanya udhalilishaji huo, na kuwa watoto wote 10 waliomtambua wasingeweza kuongopa kwa kuwa hawakuwa na sababu ya kufanya hivyo.

Ushahidi wa 'Papi kocha' kuwa asingeweza kutenda vitendo hivyo kwa kuwa mara nyingi alikuwa safarini kwa ziara za kimuziki pia ulikataliwa na mahakama zote ikiwamo ya rufaa kwa sababu alikuwa akirejea nyumbani mara ziara hizo zinapolizika.

"Mahakama haipingi kuwepo kwa ushahidi wa safari za muziki na kuwa mrufani wa pili alikuwa akienda mazoezini, lakini hiyo hamaanishi kuwa alikuwa harudi na kukaa nyumbani, wakati alipokuwepo nyumbani asingeshindwa kufanya hivyo," ilidai sehemu ya hukumu hiyo.

Kabla ya hukumu hiyo wanamuziki hao na umma wa Watanzania ulikuwa na matumaini mamkubwa ya kuachiwa huru kwa warufani hao kutokana na hoja za utetezi kushindwa kujibiwa na upande wa mashtaka katika usikilizwaji wa rufaa hiyo.

Miongoni mwa hoja hizo ni pamoja na ile ya mrufani wa kwanza 'Babu Seya' kuiomba mahakama kumpima ugonjwa wa zinaa waliokutwa nao baadhi ya watoto, ambayo ingethibitisha iwapo waliingiliwa naye au na mtu mwingine, jambo ambalo halikufayika.

Baada ya hukumu hiyo baadhi ya wanasheria na wananchi hawakusita kuonesha kutoridhishwa kwao, kwa madai kuwa upande wa mashtaka haukuweza kuthibitisha pasipo shaka kuwa warufani ndio hasa walio wadhalilisha watoto hao 10 wa darasa la kwanza shule ya Msingi Mashujaa, Sinza Dar es Salaam.

Aidha wameiomba serikali kuwasaidia vijana walioachiwa, hasa katika suala la elimu ambapo iliwalazimu kuacha shule baada ya kuhukumiwa kifungo cha maisha, kwa kile walichodai walisababishiwa usumbufu na mateso wakati hawakuwa na hatia kama ilivyothibitishwa jana.

Soma Zaidi ...

Thursday, February 11, 2010

WAZIRI SMZ ABURUZWA MAHAKAMANI

Waziri wa Maji, Ujenzi Nishati na Ardhi Mansour Yussuf Himid, amefunguliwa mashitaka katika Mahakama ya Ardhi Zanzibar kwa tuhuma za kuchukua ardhi kinyume na sheria katika kijiji cha Buyu, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Kesi hiyo imefunguliwa na Abdallah Ahmed Abdallah, ambaye anadai shamba lake limevamiwa na waziri huyo kwa malengo ya kujengwa hoteli na nyumba za kulala wageni.

Karani Mkuu katika Mahakama ya Ardhi Zanzibar, Kassim Haji Ali, alisema kesi hiyo tayari imepangwa kuanza kusikilizwa Febuari 18, mwaka huu katika Mahakama ya Ardhi na Naibu Mwenyekiti wa mahakama hiyo, Haroub Shehe Pandu, na kwamba imefunguliwa kwa hati ya ombi la dharura.

Kwa mujibu wa hati ya kiapo ya madai, Abdallah Ahmed Abdallah, shamba linalodaiwa kuvamiwa na Waziri Mansour ni mali yake aliyorithi kutoka kwa bibi yake, Mwanayamu Kombo likiwa na thamani ya Sh. milioni 12.

Abdallah ameiomba mahakama itoe amri ya kuzuia matumizi ya aina yoyote katika eneo hilo hadi mahakama itakapotoa uamuzi pamoja na kulipa gharama zote za kesi hiyo.

“Kitendo cha kufanya uvamizi na kuharibu mazingira ya shamba langu ni cha unyang’anyi na dhuluma juu yangu na kumenitia simanzi na hasara kubwa na hasa kwa kuzingatia umiliki wangu wa ardhi ni halali,” alilisisitiza katika hati yake ya kiapo ya Januari 22, mwaka huu.

Alidai kuwa shamba hilo limevamiwa na Waziri Mansour upande wa Magharibi eneo ambalo lipo pwani ya Bahari ya Hindi katika eneo la Buyu Wilaya ya Magharibi Unguja.

Alieleza kwamba ameamua kesi hiyo isikilizwe kwa ombi la dharura kwa vile tayari mdaiwa amekwishaanza kufyeka eneo hilo na kujenga ghala la kuhifadhia vifaa kwa ajili ya ujenzi wa hoteli na nyumba za kulala.

Aidha ameiomba mahakama isibitishe kuwa eneo hilo limevamiwa na mdaiwa kuwa ni eneo lake na itoe amri ya kumtaka ahame na kuondosha kila kinachowekwa katika eneo hilo na kukabidhi kwa muhusika likiwa tupu.

Mdai anaiomba mahakama kuchukua hatua ya kumtaka mdaiwa alipe gharama za mahakama na kutoa amri nyingine ili kuhakikisha haki inatendeka katika kesi hiyo.

Aidha, mdai huyo aliambatanisha na nyaraka za kuthibitisha umiliki wa eneo hilo zilizotolewa na Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana baada ya kurithi shamba hilo kutoka kwa bibi yake.
Soma Zaidi ...

BABU SEYA NA PAPII KOCHA WARUDISHWA TENA JELA

Mahakama ya rufaa leo imewarudisha tena jela Nguza Viking (Babu seya) pamoja na mwanawe Papii Nguza (papii kocha) na kuwaachia huru Nguza Mbagu na Francis Nguza.

Babu seya pamoja na wanawe watatu walihukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatika na makosa ya ubakaji wa watoto wadogo wenye umri wa miaka 6 hadi 8 mwaka 2003

Katika kesi iliyosikilizwa leo katika mahakama ya rufaa ambayo iliendeshwa kwa muda wa masaa matatu na kutolewa hukumu ilisababisha vilio baada ya mahakimu Nathalia Kimaro, Mbarouk Mbarouk na Salum Massati kuwaamuru Babu Seya na Papii kocha kurudi jena,kwa upande wa utetezi kesi hio ilikua ikisimamiwa na mawakili Mabere Marando and Hamidu Mbwezeleni, Soma Zaidi ...

CHELSEA HOI KWA EVERTON


Premier League
Blackburn Rovers 1 - 0 Hull City
Everton 2 - 1 Chelsea
Arsenal 1 - 0 Liverpool
West Ham United 2 - 0 Birmingham City
Wolverhampton Wanderers 1 - 0 Tottenham Hotspur
Aston Villa 1 - 1 Manchester United
Soma Zaidi ...

MADE IN AFGHANSTAN


Soma Zaidi ...

KIKAO MAALUM CHA UMOJA WA ULAYA KUJADILI MZOZO WA UGIRIKI

Umoja wa Ulaya unazingatia kuisaidia Ugiriki inayokabiliwa na tatizo kubwa la madeni. Hayo alitamka Kansela wa Austria Werner Faymann siku moja kabla ya kufanywa mkutano maalum wa viongozi wa umoja huo leo hii mjini Brussels.

Hapo awali,Waziri Mkuu wa Uhispania José Luis Rodríguez Zapatero alie pia Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya, alihakikisha kuwa Ugiriki itasaidiwa na umoja huo.

Wakati huo huo nchini Ugiriki wafanyakazi kutoka sekta za kuhudumia umma,wameandamana kwa maelfu kupinga mipango ya serikali ya kupunguza matumizi yake. Kuambatana na mipango hiyo, wafanyakazi serikalini hawatopata nyongeza ya mishahara na hakuna wafanyakazi wapya watakaoajiriwa katika sekta za kuhudumia umma.

Kwa kuchukua hatua hizo,serikali ya Ugiriki inajaribu kupunguza nakisi iliyovunja rekodi ikiwa ni asilimia 13 ya bajeti yake. Lengo ni kuwa ifikapo mwaka 2014 nakisi hiyo itafikia asilimia 3 ya bajeti, ambacho ni kiwango kinachoruhusiwa na Umoja wa Ulaya. Soma Zaidi ...

HABARI KATIKA PICHA


Soma Zaidi ...

Wednesday, February 10, 2010

AJUZA WA MIAKA 80 ABAKWA BAGAMOYO

Ajuza wa miaka 80, mkazi wa kitongoji cha Kiwangwa wilayani Bagamoyo amebakwa na kijana mwenye umri wa miaka 35 na kusababishiwa majeraha makali katika sehemu zake za siri.


Tukio hilo lilitokea saa 8:00 usiku wa kuamkia jana na kwamba kijana aliyehusika na tukio hilo (jina linahifadhiwa), lakini ni mkulima wa Kiwangwa wilayani humu.


Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Absalom Mwakyoma alidhibitisha tukio hilo na kusema kuwa bibi kizee huyo alibakwa wakati akiwa amelala nyumbani kwake ambapo mtuhumiwa alitumia mbinu ya kuvunja mlango usiku huo na kuingia katika chumba cha ajuza huyo kisha kumbaka kwa nguvu.


Mwakyoma alisema tukio hilo linasikitisha na kutia aibu vijana kutokana na ukweli kwamba bibi huyo anaishi kwa shida na taabu nyingi.


"Inavyoonekana huyo jamaa, alikuwa anamvizia ajuza kwa muda mrefu na nadhani alikuwa akimfuatilia kwa karibu ili kujua mwenendo mzima,alipobaini analala mwenyewe ndipo alipotumia mbinu ya kumvizia muda huo na kuvunja mlango na hatimaye kumbaka hata imani za kishirikina zinaweza kuwa ni chanzo,"alisema Mwakyoma.


Alisema mlalamikaji anaishi mwenyewe kwenye nyumba hiyo na kwamba tayari mtuhumiwa alikamatwa na anaratajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote mara uchunguzi utakapokamilika, mlalamikaji anaendelea vizuri.


Katika tukio jingine Kamanda huyo wa Polisi Pwani alisema mkazi wa Kongowe wilayani Kibaha,(Jina linahifadhiwa) alikamatwa kwa kosa la kukutwa na meno ya tembo vipande vinne vyenye uzito wa kilogramu 15.1 vya thamani ya Sh 1.1milioni.


Tukio hilo lilitokea saa 8.00 mchana juzi katika eneo la shule ya msingi Kongowe na waliomkamata mtuhumiwa huyo ni maafisa wa maliasili wa kituo cha Kongowe kwa ushirikiano na askari polisi na kwamba mzee huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote. Soma Zaidi ...

IF YOU NOTICE THIS!!!!


Soma Zaidi ...

NGOMA TUKUTANE CHINIIII


Soma Zaidi ...

WAZIRI AKOSA LA KUJIBU BUNGENI

Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Jeremiah Sumari, jana alilishangaza Bunge baada ya kutoa jibu ambalo halikutarajiwa na wabunge.

Naibu waziri huyo alisema kuwa “hajui” mara baada ya kuulizwa swali na Mbunge wa Magogoni, Vuai Abdallah Khamis (CUF), aliyetaka kufahamu kwa nini kodi inayokatwa kwa wafanyakazi wa Zanzibar kwenye Serikali ya Muungano isibaki visiwani Zanzibar.

“Spika, napenda kumjibu mheshimiwa Mbunge kuwa sijui,” jibu hilo la Sumari lilisabaisha wabunge kuangua vicheko huku mwenyewe akiridhika na kurejea kwenye kiti chake, hali iliyosababisha Naibu Waziri mwenzake, Omar Mzee kumsaidia kujibu swali hilo.

Wakati akiuliza swali la nyongeza, mbunge huyo alitaka kujua kwa nini kodi za mishahara ya wafanyakazi wa Jamhuri ya Muungano walioko visiwani humo zisiwanufaishe wananchi wa huko.

Katika swali lake la msingi, mbunge huyo alisema kuwa wafanyakazi wamekuwa wakikatwa kodi kutoka katika mishahara yao ili kuchangia huduma za jamii na mambo mengine kwanini walioko Zanzibar wasikatwe na fedha zibaki huko kwa ajili ya Zanzibar.

Akijibu swali lililomshinda Sumari, Mzee alisema pale ambapo mishahara inakokotolewa ndipo ambapo kodi inakatwa na kuwa mishahara aliyoizungumzia mbunge huyo huwa inakokotolewa Tanzania Bara.

Awali akijibu swali la msingi la Khamis Sumari alisema kodi ya mapato ni kodi ya muungano na hutozwa kwa utaratibu wa zuio kama ilivyoainishwa katika sheria ya kodi ya mapato.

Alisema utaratibu unampa mwajiri kukata kodi mahali ambapo hati ya kutayarisha mshahara wa mfanyakazi huandaliwa.

Alibainisha kuwa hati ya malipo hutayarishwa Bara, kodi ya mapato hukatwa Bara na kuingizwa katika mfuko mkuu wa serikali ya Jamuhuri ya Muungano na kama hati hiyo ya malipo hutayarishwa Zanzibar, kodi ya makato hukatwa Zanzibar na huingizwa katika mfuko Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Soma Zaidi ...

MAJI NI AFYA

Correct timing to take water, will maximize its effectiveness to Human body. Two (02) glass of water - After waking up - Helps activate internal organs

One (01) glasses of water - 30 minutes before meal - Help digestion

One (01) glass of water - Before taking a bath - Helps lower blood pressure

One (01) glass of water - Before sleep - To avoid stroke or heart attack



Soma Zaidi ...

Tuesday, February 9, 2010

TIMU YA TAIFA YA BENIN YAVUNJWA


Shirikisho la mchezo wa soka nchini Benin, limevunja kikosi kizima cha timu ya taifa ya nchi hiyo kufuatia matokeo mabaya katika michuano ya kuwania kombe la mataifa bingwa barani Afrika.

Kocha wa timu hiyo raia wa Ufaransa Michel Dussuyer na maafisa wote wa kiufundi pia wamefutwa kazi. Kwa mujibu maafisa wakuu wa shirikisho hilo, kikosi hicho kimevunjwa kutokana na utovu wa nidhamu na kutowajibika kama wazalendo.

Timu hiyo inayojulikana kama The Squirrels, iliyaaga mashindano hayo nchini Angola, baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu katika kundi lake na alama moja pekee.
Soma Zaidi ...

DR CONRAD MURRAY ABURUZWA MAHAKAMANI

Daktari wa Michael Jackson, Conrad Murray alifikishwa katika mahakama mjini Los Angeles na kushtakiwa kwa kusababisha kifo cha mwanamuziki huyo miezi saba iliyopita.

Murray alikuwa ameajiriwa kumsaidia Michael Jackson kujiandaa kwa tamasha kadhaa mjini London na inaaminiwa kuwa alikuwa mtu wa mwisho kumwona mwanamuziki huyo akiwa hai.

Inadaiwa kuwa daktari Murray aliwaeleza wapepelezi kuwa alimpa Jackson dawa kadhaa ikiwemo ile yenye nguvu nyingi ya Propofol ambayo kwa kawaida hutumika hospitalini pekee.

Inadaiwa baada ya kumpa dawa hiyo Murray aliondoka kwa muda mfupi kutoka chumbani mwa Jackson ili kupokea simu na aliporudi akampata mwanamuziki huyo hapumui.

Afisa wa upelelezi alimpata daktari huyo na hatia ya kumpa Michael Jackson propofol kwa kupita kiasi kilichostahili na hivyo kusababisha kifo chake. Lakini alipofikishwa mahakamani kwa kosa hilo ambalo linaweza kumpa kifungo cha miaka 4 gerezani, Daktari Murray alisisitiza kuwa hakuna na hatia.

Daktari Murray aliachiliwa kwa dhamana ya dola 75,000 akisubiri kusikilizwa kwa kesi yake mwezi april Soma Zaidi ...