Monday, November 30, 2009

KIATU AME BINGWA MBIO ZA PUNDA ZANZIBAR

Wiki iliyopita wakaazi wa wa Mkoa wa mjini magharibi hasa wale wa wilaya ya mjini walishuhudia burudani mwanana ya mbio za punda iliyofanyika katika mji huo.Mbio hizo zilizoanzia viwanja vya kibanda maiti na kumalizikia katika uwanja wa Mao tse tung, ziliwashirikisha punda 60.

Mbio hizo zilizoandaliwa na kituo cha radio cha Coconut FM zilikua ni kivutio kwa watu waliofika na kushuhudia uhondo huo,kwani ni miaka miwili sasa mashindano hayo hayajaonekana tangu yalipofanyika kwa mara ya mwisho mwaka2007.

Mshindi wa kwanza wa mbio hizo aliejuilikana kwa jina la Kiatu Ame amejinyakulia zawadi mwanana ya shilini milioni moja (1,000,000) baada ya kutumia dakika 35:06 kwa kilomita sita,huku nafasi ya pili ikishikiliwa na kijana Makame Khamis aliyetumia dakika 36:00 na kunyakua shilingi laki saba (700,000).

Nafasi ya tatu ya mashindano hayo ilichukuliwa na Mwinyi Said na kuzawadiwa shilingi laki tano (500,000) wakati Abdullah Khamis alijipongeza kwa kitita cha shilingi laki mbili (200,000) kwa kutokea wa nne

Mgeni wa heshima katika mashindano hayo alikua ni Mstahiki mea wa mji wa Zanzibar Mahboub Juma. Soma Zaidi ...

ZANZIBAR WACHEKA TANGANYIKA WALIA CHALLENGE

Mashindano ya Challenge yanaondelea kutimua vumbi huko Nairobi Kenya, Zanzibar wameanza vyema mashindano hayo kwa kuibugiza Burundi mabao 4-0 na kujiweka kwenye matumaini ya kuendelea na mshindano hayo huku Tanganyika ikianza vibaya mashindano hayo licha kuwa na wachezaji wao wanaochza soka ya kulipwa ulaya kwa kukamizwa mabao 2-0 na Uganda, nao Rwanda wakailaza Somalia kwa 1-0.
Kesho katika uwanja wa Mimius patakua hapatoshi wakati Zanzibar watakapokutana na Tanganyika huku Tanganyika wakitafuta matumaini ya kuweza kusonga mbele na Zanzibar wao pia wakitaka kujiongezea alama.

Leo hii kutakua na mechi kati ya Ethiopia wakiminyana na majirani zao Jibouti.
Soma Zaidi ...

Sunday, November 29, 2009

ITAI NJE BBA REVOLUTION

Hatimae wamebaki washiriki watano katika jumba la Big Brother baada ya Itai almaaruf (Ma man) kutolewa nje ya jumba hilo,washiriki wote waliobakia watahitaji kupigiwa kura ili kupata mtu mmoja wa kutoka jumapili ijayo, na kura zinazoweza kumbakisha mtu kwenye jumba hilo ni zile zinazopigwa kutoka katika nchi ya msiriki husika, kwa hio mshiriki atakae pata kura nyingi kutoka nchini kwake atakua amebakia, na atakaepata kura kidogo kutoka nchini kwake basi itakuwa wenyewe ndio wamemtoa.

Soma Zaidi ...

MATOKEO YA MECHI ZA LEO

Arsenal walishindwa kufurukuta walipokua nyumbani kwao leo hii walipochuana na Chelasea na kukandwamizwa magoli 3-0 goli la mwanzo la Chelsea lilifungwa na Drogba la pili liliingia kimyani baada ya mlizi wa Arsenal Thomas Vermaelen kutaka kuokoa mpira wa cross iliopikwa na Ashley cole na hatimae kuujaza nyavuni na goli la tatu liliwekwa tena kimyani na kinara Drogba.

Matokeo mengine ya mechi za leo ni kama ifuatavyo:

Arsenal 0 - 3 Chelsea
Everton 0 - 2 Liverpool
Wolverhampton Wanderers 0 - 1 Birmingham City

Football La Liga
FC Barcelona 1 - 0 Real Madrid
Real Zaragoza 0 - 1 Osasuna
UD Almería 1 - 4 Athletic Bilbao
Real Valladolid 3 - 3 CD Tenerife
Getafe CF 5 - 1 Xerez CD
Racing Santander 0 - 1 Deportivo La Coruña
Sevilla FC 2 - 2 Málaga CF

Football Bundesliga Match
Hannover 96 0 - 3 Bayern München
Bayer Leverkusen 4 - 0 VfB Stuttgart

Football Serie A Match
Atalanta 1 - 2 AS Roma
Parma 1 - 1 Napoli
Lazio 0 - 0 Bologna
Internazionale 1 - 0 Fiorentina
Cagliari 2 - 0 Juventus
Bari 2 - 1 Siena
Chievo 1 - 0 Palermo

Football Ligue 1 Match
Le Mans 1 - 1 Saint-Etienne
AS Nancy 0 - 3 Girondins Bordeaux Soma Zaidi ...

TIGER WOODS ATAFUTWA NA POLISI BAADA YA KUPATA AJALI

Bingwa namba moja wa golf duniani Tiger Woods anasakwa na Polisi wa mji wa Florida kwa ajili ya kufanya nae mahojiano kufuatia ajali ya gari aliopata siku ya ijumaa usiku Mnamo saa 2:25 am.Woods alipata ajali hio mara baada ya kushindwa kulimiliki gari lake alilokua akiendesha aina ya Cadillac 2009 na kwenda kugonga fire hydrant na baadae kugonga mti.

Katika ajali hio woods alipasuka mdomo na kutokwa na damu nyingi kitendo ambacho kilisababisha yeye kupoteza fahamu na kulazwa hospitali. lakini aliruhusiwa baada ya kupatiwa matibabu.
Mkuu wa polisi wa Windermere Chief Daniel Saylor,mke wa Woods bibi Elinaliiambia polisi kua alifika katika eneo la ajali na kumkuta mumewe amekwama ndani ya gari na hakuweza kumtoa kwa mlango wa mbele na ndipo alimtoa kwa kuvunja kioo cha nyuma ya gari kwa kutumia gongo la kuchezea golf.

Polisi walitarajia kuzungumza na Woods jana jumamosi lakini walimkosa walipofika nyumbani kwake, na katika mahojiano yaliofanywa na baba mkwe wa Woods ambae ni mtangazaji wa redio bwana Thomas Nordegren aliviambia vyombo vya habari kua hakua tayari kuzungumza kuhusu ajali

"sijazungumza nae ni siku sasa.....bwana thomas alisema kuhusu mwanawe Elin,kabla hajakata simu "sitaki kuzungumzia hili. Mama mkwe wa Woods pia alikataa kuzungumza kuhusu ajali hio.

Roger Federer ambae amekua rafiki mkubwa wa Woods katika miaka ya karibuni pia alisema kua hakuzungumza nae tangu alipotolewa nusu fainali ya ATP London " sijazungumza nae, lakini nasikia kama hayuko mahututi.
Soma Zaidi ...

Saturday, November 28, 2009

HII NDIO INAYOUA WATU CONGO

Dhahabu hii kutoka mashariki ya Congo eneo la Kaniola pamoja na maeneo mengine ndio yanayounda mlolongo wa matatizo ndani ya Congo. Biashara hii ya maadini ndio ilioleta vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha watu wengi kuikimbia nchi yao.Nchi ambayo ilitegemewa kuwa ni miongoni mwa nchi matajiri duniani.Inakisiwa kua Congo iliuza maadini mbali mbali ikiwemo Dhahabu kwa kiasi cha dola za kimarekani milioni hamsini ($50m) mwaka jana.Katika biashara hii ya dhahabu ambayo wafanyakazi wake wakuu ni watoto,inawafaidisha wana wazungu pamoja na wakuu wa nchi huku ikiacha wananchi wake wakikosa huduma muhimu za kijamii. Soma Zaidi ...

WAINGIA IKULU BILA YA KUALIKWA

Wanandoa wawili Michele Salahi na mumewe Tareq walihudhuria chakula la jioni ndani ya Ikulu ya Marekani (White House) bila ya kualikwa, wanandoa hao walipata kupokelewa na rais Obama katika chumba cha mapokezi.Katika Ghafla hio ambayo ilihidhuriwa na wakuu mbali mbali akiwemo waziri mkuu wa india Manmohan Singh ambae alikua ndie mgeni rasmin katika ghafla hio

Bibi salahi alipata kupiga picha na wakuu mbali mbali waliohudhuria ghafla hio akiwemo makamo wa rais wa Marekani pamoja na kupenana mkono na Obama.

Wadadisi wa mambo wamesema kua kitendo cha wanandoa hao kutinga ndani ya White House kinyemela ni aibu sana kwa wanausalama wa ikulu hio, walinzi waliokua katika ghafla hio walikiri kufanya kosa kwa kuwaachia wanandoa hao kupita kiulaini.

Imesemwa kua hakukua na kitendo cha hatari ndani ya ikulu kufuatia kitendo hicho, uchunguzi zaidi unaendelea na bibi Salahi na mumewe Tariq wanaweza kushtakiwa ikiwa watabainika kutenda kosa
Soma Zaidi ...

Thursday, November 26, 2009

48 WAFARIKI DUNIA KUTOKANA NA MVUA SAUDI ARABIA

Watu 48 wamefariki na wengine 900 wameokolewa baada ya mvua kubwa kunyesha huko SAudi Arabia. Msemaji katika wizara ya mambo ya ndani ya Saudi Arabia amesema hakuna katika majeruhi ambae ni miongoni mwa mahujaji waliohudhuria katika ibada ya hija.

Hija inajumuisha siiku nne ambayo ilianza siku ya jumatano na kuhudhuriwa na waumini milioni tatu kutoka kila sehemu duniani.

Mvua kwa sasa zimesimama lakini kuna matarajio ya mvua zaidi kunyesha,vyombo vya habari vimeripoti kua vifo vilitokea Jiddah, Rabigh na Makka.

Leo hii mahujaji wanafanya kitendo muhimu zaidi katika hija nacho ni kusimama katika mlima wa 'Arafa mpka jua kuzama.

Ibada ya hija mwaka huu inafanyika huku dunia ikiwa katika mgogoro mkubwa wa kiuchumi pamoja na mripuko wa homa ya mafua ya nguruwe (H1N1 virus)
Soma Zaidi ...

Wednesday, November 25, 2009

MATOKEO YA CHAMPIONS LEAGUE

Manchester United wafungwa nyumbani 1-0 na Besiktas ya Uturuki.

Girondins Bordeaux 2 - 0 Juventus
Bayern München 1 - 0 Maccabi Haifa
AC Milan 1 - 1 Olympique Marseille
Real Madrid 1 - 0 FC Zürich
FC Porto 0 - 1 Chelsea
APOEL Nicosia 1 - 1 Atlético Madrid
CSKA Moskva 2 - 1 VfL Wolfsburg Soma Zaidi ...

MAZIKO YA AINA YAKE BONGO

Soma Zaidi ...

KITUO CHA POLISI MALINDI ZANZIBAR


Mzee kiss naomba uwawekee hii picha ya kituo chetu cha Polisi wa usalama barabarani Malindi Kituo hichi kina kawaida ya kulia honi kila sikua mara tatu asubuhi saa moja na nusu, ni wakati wa kwenda makazini, mchana saa tisa na nusu, ni wakati wa kutoka makazini, na saa kumi na mbili na nusu jioni, hii inatumika sawa na wakati wa kusali sala ya magharibi na ikiwa ni wakati wa mwezi wa Ramadhani watu hutumia kama ni wakati wa kuftari.

Ali abdallah, Darajani Zanzibar

Soma Zaidi ...

PICHA YAMDHALILISHA MICHELLE OBAMA

Kampuni ya Google imeomba msamaha kutoka kwa Michelle Obama, mkewe rais wa Marekani kutokana na picha inayomdhalilisha na ambayo imechapishwa kwenye mtandao.
Picha yenyewe imechorwa kwa mfano wa mnyama na inajitokeza pindi mtu anapotafuta kwenye mtandao picha zozote za Michelle Obama.

Google imeomba radhi na kukiri kwamba picha hiyo ambayo tayari imezua hoja kali inachochea hisia za ubaguzi wa rangi.

Kampuni hiyo imetoa tahadhari kwa wale wanaotembelea mtandao na kutafuta picha za Michelle Obama ingawa ilisema haiwezi kuiondoa hiyo picha.

Ikulu ya Marekani, White House, imekataa kutamka lolote kuhusu tukio hilo. Soma Zaidi ...

ZANZIBAR KWENDA KENYA KWA CHALLENGE

Wachezaji wa timu ya taifa ya Zanzibar wakiwa bandarini Dar-es-salaam leo asubuhi wakielekea nchini Kenya tayari kwa mashindano ya Challenge ambayo yatafanyika kwa muda wa wiki mbili.Safari hio imejumuisha watu 26 wakiwemo wachezaji 19 pamoja na viongozi 7.

Wachezaji ni pamoja na Abdi kassi,Mwadini Ali, Aggrey Morris, Suleiman Kassim, Abdallah Seif, Nassor Masoud, Sadik Habib, Ahmed Malik, Abdulhalim Humud, Abdulrahman Othman, Khamis Mcha, Haji Ramadhani, na Waziri Rajab.

Wengine ni Mohamed Salum, Rashid Faki, Nadir Haroub, Abdughany Gulam, na Mohamed Abdallah.


Viongozi ni pamoja na Hemed Suleiman Moroco (kocha msaidizi), Abdulfath Abbasi (kamati ya ufundi), Khamis Ali Mzee (mkuu wa msafara), Abdallah Saidi (daktari), and Haji Ameir (makamo wa rais ZFA).

Aidha jana ilianyika sherehe ya kuwaaga wachezaji hao ambapo katibu mkuu wizara ya habari utamaduni na michezo Omar Dadi Shajak aliwataka wachezaji hao ku jitahidi katika mashindano hayo ili kurudi na ushindi.


"Najua mtasafiri kutoka Dar-es-salaam hadi Nairobi kwa basi lakini hii isikuvunjeni moyo.


Ndugu Dadi alisema kua ni furaha kusafiri kwa basi kwani hata timu kubwa kama Manchester United pia wanatumia usafiri kama huo huko Ulaya,


"Serikali imetumia shilingi milioni kumi (10m.) kwa maandalizi ya timu, mnakwenda kuiwakilisha Zainzibar hivo ushindi wenu utatufanya sisi sote tujivunie"alisema katibu huyo kabla hajakabidhi bendera kwa nahodha wa timu hio.


Timu nyengine zitakazo shiriki mashindano hayo ni pamoja na Tanzania Mainland, hosts Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Ethiopia, Eritrea, Djibouti and Sudan.

Soma Zaidi ...

Tuesday, November 24, 2009

MATOKE YA CHAMPIONS LEAGUE

Liverpool wayaaga mashindano licha ya kushinda 1-0 dhidi ya Debrecen

Fiorentina 1 - 0 O lympique Lyon
FC Barcelona 2 - 0 Internazionale
Rangers 0 - 2 VfB Stuttgart
Unirea Urziceni 1 - 0 Sevilla FC
Arsenal 2 - 0 Standard Liège
AZ Alkmaar 0 - 0 Olympiacos
Rubin Kazan 0 - 0 Dynamo Kyiv Soma Zaidi ...

ATUPWA JELA MAISHA BAADA YA KUMSABABISHIA KIFO BIBI KIZEE KWA WOGA

CHARLOTTE, N.C. Kijana mmoja nchini Marekani atamalizia maisha yake yaliobaki gerezani baada ya kugundulika kua mkosa kwa lile lililoelezwa kua ni kumtia woga bibi mmoja mwenye umri wa miaka 75 anaeishi North Carolina na kumsababishia kifo.

Vyombo vya habari vilieleza kua mahakama haikumtia haitiani kijana huyo mwenye umri wa miaka 21 Larry Whitfield kwa kosa la kumuua bibi Marry Parnells mwaka jana.Lakini waligundua kua ni mkosa kwa kumsababishia kifo bibi huyo baada ya kumteka na hii kupelekea moja kwa moja kufungwa kifungo cha maisha.

Waendesha mashtaka walieleza kua kijana huyo alikua akitafuta sehemu ya kujificha baada ya jaribio lake la kuteka benki huko Gastonia Septemba 2008 kutofanikiwa na ndipo alipovunja na kuingia ndani ya nyumba ya bibi Parnells.Wahusika walisema kua whitfield hakumgusa bibi huyo lakini alipata mshtuko wa moyo na kufa, na wala whitfield hakuomba msaada. Soma Zaidi ...

Monday, November 23, 2009

KARUME ALIPOPOKEA MAANDAMANO JANA

Karume akipokea maandamano ya wanachama wa CCM wa mikoa mitano ya Zanzibar jana jumapili katika viwanja vya kibanda maiti wilaya ya mjini mkoa wa mjini magharib Soma Zaidi ...

MAHUJAJI WANNE WAFARIKI KWA MAFUA YA NGURUWE

Mahujaji wanne waliokuwa nchini Saudi Arabia kuungana na mamilioni ya mahujaji toka nchi mbali mbali duniani kwaajili ya hija kubwa, wamefariki dunia kutokana na mafua ya nguruwe.

Mwanaume mmoja toka India, mwanamke mmoja toka Morocco na mwanaume mwingine toka Sudan wote wenye umri zaidi ya miaka 75 pamoja na msichana mwenye umri wa miaka 17 toka Nigeria wamefariki dunia kutokana na ugonjwa wa homa ya mafua ya nguruwe walioambukizwa wakati wa hija.

"Wote walikuwa na matatizo mbali mbali ya kiafya kabla ya kukumbwa na mafua ya nguruwe, msichana wa Kinigeria alikuwa na matatizo ya kifua", alisema msemaji wa wizara ya afya ya Saudia, Khaled al-Marghlani.

"Pia hakuna hata mmoja wao aliyepiga sindano ya chanjo ya ugonjwa wa mafua ya nguruwe", aliongeza msemaji huyo wa wizara ya afya.

Takribani waislamu milioni 2.5 wanatarajiwa kuhudhuria hija ya mwaka huu, ukiwa ni mkusanyiko mkubwa kuliko wote wa watu tangia ugonjwa wa mafua ya nguruwe ulipogunduliwa nchini Mexico mwezi aprili mwaka huu.

Watu 20 wamegundulika kuambukizwa mafua ya nguruwe tangia hija zilipoanza katika miji ya Makka na Madina na 12 kati yao walipatiwa matibabu na kutolewa hospitali wakati watu wanne bado wamelazwa hospitali.

Wataalamu wa masuala ya afya wamesema kuwa maambukizi ya ugonjwa huo yamekuwa katika kiwango kidogo sana kuliko ilivyohofiwa kutokana na tahadhari zilizochukuliwa.

Wataalamu wa afya 20,000 wamepelekwa kwenye miji ya Makka, Madina na Jeddah kuwa tayari tayari kupokea watu watakaoambukizwa ugonjwa huo huku hospitali zimewekwa mamia ya vitanda vya ziada.

Mawe yatakayotumika kuipiga alama ya shetani wakati wa hija, nayo yamewekwa madawa kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo.

Watu wenye magonjwa sugu, wazee sana, watoto na wanawake wenye mimba wametakiwa kuahirisha safari zao za hija mwaka huu.

Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO, watu 6750 wamefariki duniani kutokana na ugonjwa wa mafua ya nguruwe tangia ulipogunduliwa nchini Mexico na Marekani mwezi aprili mwaka huu.

Waislamu hutakiwa kuhudhuria ibada ya hija mara moja katika maisha yao iwapo watakuwa na uwezo wa kufanya hivyo.

Sikukuu ya Idi itasherehekewa ijumaa wiki hii huku baadhi ya nchi zingine zikisherehekea jumamosi.

Soma Zaidi ...

Mhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh!!!!


Soma Zaidi ...

Sunday, November 22, 2009

EMMA ANUSURIKA KWA MARA NYENGINE TENA BIG BROTHER

Mambo yamezidi kupamba moto ndani ya jumba la Big Brother, hivi sasa wamebaki washiriki 6 ndani ya jumba hilo baada ya mshiriki kutoka Nigeria Geraldine kufukuzwa kutoka kwenye jumba hilo kwa kupata kura chache huku Emma kunusurika kufukuzwa kwa mara nyengine tena baada ya kupata kura nyingi kumshinda Geraldine, kabla ya Geraldine kutolewa mjengoni IK alimtaka Itai kumtaja ni nani alie mnusuru na alimbadilisha na nani na ndipo aliposema kwamba amejinusuru yeye mwenyewe na amejibadilisha na Geraldine, na alipotakiwa kutoa sababu za kumuweka juu Geraldine alishindwa kufanya hivyo.

Kaa tayari kujua ni nani na nani atakua juu kwa kufukuzwa siku ya jumapili ijayo

Soma Zaidi ...

TANGAZO:

ASSLAAM ALAIKUM,
UONGOZI WA BUSTANI YA WASWAHILI UNAPENDA KUWAALIK A WATU WOTE KATIKA WEBSITE YAO, KWA AJILI YA KUCHANGIA MAONI, KUTAFUTA MARAFIKI, KUBADILISHANA MAWAZO KWA PICHA, VIDEO, MIZIKI, NA MENGINE MENGI WEBSITE YENYEWE NI HII:
KARIBUNI SANA
Soma Zaidi ...

MATOKEO YA MECHI ZA JANA



PREMIER LEAGUE
Manchester United 3 - 0 Everton
Birmingham City 1 - 0 Fulham
Burnley 1 - 1 Aston Villa
Chelsea 4 - 0 Wolverhampton Wanderers
Hull City 3 - 3 West Ham United
Sunderland 1 - 0 Arsenal
Liverpool 2 - 2 Manchester City


LA LIGA
Athletic Bilbao 1 - 1 FC Barcelona
Real Madrid 1 - 0 Racing Santander
Deportivo La Coruña 2 - 1 Atlético Madrid
CD Tenerife 1 - 2 Sevilla FC

SERIE A
Fiorentina 2 - 3 Parma
Bologna 1 - 3 Internazionale


BUNDESLIGA
Borussia Dortmund 0 - 0 FSV Mainz 05
VfB Stuttgart 1 - 1 Hertha BSC
VfL Wolfsburg 2 - 3 1.FC Nürnberg
Eintracht Frankfurt 1 - 2 Borussia Mönchengladbach
1. FC Köln 0 - 4 Hoffenheim
SC Freiburg 0 - 6 Werder Bremen
Schalke 04 2 - 0 Hannover 96
DUTCH EREDIVISIE
FC Twente 1 - 0 Vitesse
RKC Waalwijk 3 - 1 FC Groningen
NAC Breda 3 - 3 NEC
Roda JC 2 - 4 AZ Alkmaar
Soma Zaidi ...

Saturday, November 21, 2009

AFUNGA NDOA NA BINTI YAKE KWA AJILI YA MAKARATASI



Mzee Jelili Adesanya mwenye umri wa miaka 54, mzaliwa wa Nigeria mwenye pasipoti ya Uingereza anafanyiwa uchunguzi baada ya kugundulika kuwa amefunga ndoa na binti yake wa kumzaa.

Mzee Jelili ambaye yupo nchini Uingereza tangia mwaka 1976 anatuhumiwa kufunga ndoa na binti yake Karimotu Adenike na kuishi naye kwa kuzuga kama mke wake ili aweze kupata "makaratasi" ya Uingereza.

Magazeti ya Uingereza yalitoa habari hii yakiambatanisha na picha ya harusi ya Jelili na binti yake wakiwa wameshikana mikono kama maharusi wa kweli.

Taarifa zilizotolewa na karibia magazeti yote ya Uingereza zilisema kwamba Jelili alifunga ndoa ya bomani na binti yake nchini Nigeria tarehe 29 mwezi mei mwaka 2007 na baada ya hapo aliomba viza ya miaka miwili ya ndoa kumwezesha "Mke wake" (binti yake) aishi Uingereza. Alipewa viza hiyo mwezi oktoba mwaka huo huo.

Baba na mwanae walikuwa wamepanga kuwa baada ya miaka miwili, binti yake atapata sheria za Uingereza za kumruhusu kuishi milele Uingereza na hivyo ataivunja ndoa yake na baba yake na kisha atafunga ndoa tena lakini safari hiyo itakuwa na mumewe wa kweli anayeishi Nigeria ambaye amezaa naye watoto wanne.

Mpango huo umeingia chachu baada ya mdaku mmoja asiyejulikana wa nchini Nigeria kuripoti ubalozini, wizarani mpaka kwa mawaziri kuwa mzee huyo amefunga ndoa na binti yake.

Taarifa zilisema kwamba wizara ya mambo ya ndani ya Uingereza ilitaarifiwa suala hilo na mdaku huyo miaka miwili iliyopita lakini haikuchukua uamuzi wowote.

Mdaku huyo awali alituma barua ubalozi wa Uingereza nchini Nigeria akiwataarifu suala hilo akiambatanisha majina yao, anuani zao, namba za pasipoti zao mpaka picha ya harusi yao.

Baada ya kuona hamna hatua yoyote iliyochukuliwa, februari mosi mwaka huu mdaku huyo aliamua kuwatumia email waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza wa wakati huo, Jacqui Smith na mawaziri Vernon Coaker na Phil Woolas lakini mawaziri hao nao hawakuchukua hatua yoyote.

Taarifa zaidi zilisema kwamba Adenike alibadilisha umri wake kwenye pasipoti yake kwa kujiongezea miaka 10 zaidi ili kusiwe na tofauti kubwa ya umri kati yake na baba yake. Adenike hivi sasa ana umri wa kwenye miaka ya 30 na ushee.

Taarifa zaidi zilisema kwamba hata harusi yao iliyofanyika Nigeria ilifanyika kwa kuzuga kwa kukodisha wahudhuriaji wa harusi hiyo ili ionekane kama ya kweli.

Zengwe la ndoa yao limebumbuluka hivi sasa baada ya viza ya miaka miwili aliyopewa Adenike kuisha na akiwa kwenye hatu za mwisho za kuomba sheria ya kuishi Uingereza milele.

Jelili na binti yake wanafanyiwa uchunguzi kuhusiana na tuhuma hizo na maafisa wa uhamiaji wa Uingereza wamesema kuwa ikithibitika kuwa tuhuma hizo ni za kweli basi Jelili na binti yake watapandishwa kizimbani na huenda wakatupwa jela kabla ya kurudishwa Nigeria." />
Soma Zaidi ...

Friday, November 20, 2009

OPRAH WINFREY KUTANGAZA MWISHO WA TALK SHOW YAKE

Oprah Wilfrey anatarajiwa kutangaza leo hii kwamba mwisho wa talk show yake itakua ni 2011 baada ya talk show hio kuwa hewani kwa muda wa miaka 25, msemaji wa Oprah alisema waendeshaji wa show hio watatoa habari zaidi katika show itakachorushwa moja kwa moja leo hii, kua show ya mwisho itakua Septemba 2011.

"Tuna heshima kubwa kwa Oprah na hatuna zaidi ya kumtakia mafanikio na mwisho mwema, tunajua kwamba jambo lolote atakalo lifanya baada ya hili litakua ni lenye mafanikio makubwa, tunatarajia kufanya nae kazi kwa miaka mingi na baade kwa ujumla", iliandika CBS.

Wilfrey alianza utangazaji katia mji wa Nashville, Ten, na Baltimore kabla hajahamia Chicago 1984 kuendesha WLS-TV's morning talk show "A.M. Chicago."

Na katika mwaka 1985 aliibadilisha jina show hio na kuiita Oprah Wilfrey Show
Soma Zaidi ...

Thursday, November 19, 2009

WATU WENGI ZIMBABWE NI MILIONEA LAKINI SIO MATAJIRI

Kununua mkate tu basi lazima uwe milionea
Jamaa akilipa baada ya kula chakula Restaurant
Zimbabwe vipochi havitumiki
Soma Zaidi ...

Wednesday, November 18, 2009

KARUME KATIKA UFUNGUZI WA MADARASA YA KILIMO

Rais Karume pamoja na balozi wa Japan nchini Tanzania Mr Hiroshi Nagakawa, wakikata utepe kwa pamoja jana, katika ufunguzi wa madarasa ya kilimo katika eneo la Tunguu mkoa wa kusini Unguja, ubalozi wa japani ndio uliodhamini ujenzi wa madarasa hayo Soma Zaidi ...

Tuesday, November 17, 2009

MAJUMBA YA MICHENZANI

Majumba ya michenzani ambayo yalijengwa na Rais wa mwanzo wa Zanzibar Mh, Abeid Aman Karume, majumba kama haya yalijengwa sehemu tofauti ndani ya Zanzibar kama vile kikwajuni, kilimani, makunduchi, Gamba, (kama sijakosea jina) hii ni kwa upande wa Unguja na kwa upande wa Pemba ni Chake chake(madungu), Mkoani (mapinduzi), Wete(mtemani) na Micheweni, na pia Rais Mh, karume alijenga nyumba za vijiji ambazo zipo sehemu nyingi pia Unguja na Pemba.

Tukashuhudia tena mambo angalau mfano wa haya kwa Rais wa awamu ya tano Komandoo Dr, Salmin Amour juma ambae alijenga majumba ya Mchina, akajenga pia nyumba za kijiji ziliopo huko huko maeneo ya mombasa sokoni, na kumalizia jumba moja ambalo liliachwa tokea awamu ya kwanza jumba nama 9 upande wa madema.

Na awamu ya sita ikamalizia pia jumba nambari 10 ambalo lilijengwa kwa nguvu kubwa kutoka kwa vikosi vya SMZ.

Hapa ninahisi kama wananchi wangefaidika vizuri sana kama kila Rais angekua anafanya mambo kama aliofanya Mzee Karume na Dr Salmin lakini naona kila kukicha ni vurugu mechi tu hakuna moja la maana linalofanyika zaidi ya watu kuvunjiwa nyumba zao ambazo wanazijenga kimasikini masikini tena kwa muda wa miaka mingi eti kwa kisingizio cha kua wamejenga maeneo yasioruhusiwa sasa mimi najiuliza kama ni maeneo yasio ruhusiwa hivi Serikali ilikua wapi wakati wananchi wanaanza kujenga katika maeneo haya? lakini hili kwa leo naliacha kwa sababu sio pahali pake kulizungumzia. Soma Zaidi ...

Monday, November 16, 2009

KOFIA ZA KIUA NDANI YA ZANZIBAR

Kuna rafiki yangu mmoja amenitumia hii picha na ameniambia niulize kama je kuna sehemu yoyote ambayo kuna wataamu wa kushona kofia za kiua kuliko Makunduchi Zanzibar?
maana anasema kila mmakunduchi anajua kushona hizi kofia.

sasa mimi sijui kama ni kweli au anajisifu tu kwa hio kama kuna mwenye hoja ataniandikia Soma Zaidi ...

NGUVU YA HoH KISHERIA YAMUOKOA ITAI BBA

Mambo yamezidi kupamba moto ndani ya jumba la Big Brother wiki hii baada ya majina mawili kutajwa kwa ajili ya kufukuwa siku ya jumapili ijayo, majina yaliyotajwa ni Emma pamoja na Itai

Wakati huo huo Itai yeye mwenyewe amechaguliwa kuwa mkuu wa nyumba kwa wiki hii( HoH),kisheria mkuu wa nyumba anakua na fursa ya kumuokoa mtu mmoja ambae yuko juu na ambadilishe na mwengine, kwa hio Itai alipotakiwa kufanya hivo na Big Brother ndipo alipopata nafasi ya kujiokoa yeye mwenye na kujibadilisha na Geradine kwa hio waliokua juu wiki hii ni Emma na Geradine

Kwa hio tunasubiri siku ya jumapili ili kuangalia kama je Emma atanusurika kwa mara nyengine tena? kwa sababu aliwahi kunusurika siku za nyuma. Soma Zaidi ...

HONGERA TZ KWA MAENDELEO MLIOFIKIA KATIKA ELIMU

Hii ni skuli ya msingi Iboma katiaka kijiji cha udinde wilaya ya Chunya Mkoani Mbeyana hawa ni wanafunzi wa darasa la kwanza.
Hongera sana viongozi Soma Zaidi ...

MASIKINI ZANZIBAR HAIKUA HIVI!!!


Picha hizi zinaonesha jinsi tamasha la muziki lijuilikanano kama Fiesta one love lililofanyika ngome kongwe Zanzibar na jinsi watu walivyovaa, kwa kweli nchi imefika pabaya sana.Sikusudii kusema kwamba Zanzibar kulikua hakuna miziki, nisieleweke vibaya. Zanzibar kuna miziki tangu mimi sijazaliwa lakini ilikua ni tofauti na hivi sasa.
Hapo zamani ilikua watu wakienda kwenye Taarab mziki ambao ndio unaopendwa sana Zanzibar, walikua wakivaa kwa heshima na hakukuwa na anaweza kuvaa nusu uchi,wala aneweza kukosa adabu, lakini picha hizi zinaonesha jinsi watu walivobadilika kiasi kikubwa katika mavazi, au hii ndio moja ya maendeleo?, kwa kweli inasikitisha sana kuona hali kama hii na mimi hua najiuliza bila kupata jibu kwamba je hawa watu ni wazanzibari au ni wageni wamekuja kwa sababu ya hilo tamasha? hapo silewi.
Kwa kweli jitihada inahitajika katika kurudisha hadhi na heshima ya Zanzibar, na ninaamini hakuna kinachoshindikana.
Soma Zaidi ...

KEVIN BADO NGANGARI BBA

Kwa mara nyengine tena mnigeria Kevin aendelea kupeta ndani ya jumba la Big Brother, Kevin aliwekwa juu kwa ajili ya kufukuzwa na aliekua mkuu wa nyumba wiki iliopita Edward baada ya kumuokoa Itai na kupata nafasi ya Kevin kuchuana na Leonel kwa kutafuta wingi wa kura, hatimae Leonel akakosa kura za kuweza kumbakisha ndani ya jumba hilo na kuyaaga mashindano hayo, leo joni tutajua ni nani na nani wako juu kwa kufukuzwa jumapili wiki hii

Soma Zaidi ...

Sunday, November 15, 2009

KWANI WAO WAMEWEZA WANA NINI HATA SISI TUSHINDWE TUMEKOSA NINI?

Ni miongoni mwa barabara za wenzetu zikiwa katika mpango ulio bora kabisa, na ukizingatia kwamba wao hawana dhahabu, hawana almasi, hawana tanzanite, hawana shaba wala chuma.Hawana gesi hawana karafuu hawana mafuta ya petroli wala ya taa, wala hawazalishi kitu chochote chenye thamani duniani. Inauma sana Soma Zaidi ...

MAFUNZO YACHUKUA NAFASI YA AZAM TUSKER



Shirikisho la soka nchini TFF limeichagua klabu ya Mafunzo kutoka kisiwani Zanzibar kuziba nafasi iliyoachwa na Azam kwenye michuano ya Tusker itakayoanza kutimua vumbi DesemGazeti moja la kila siku limeandika kuwa, hatua hiyo imekuja baada ya ZFA kuliandikia barua shirikisho hilo kuwa ingekuwa sawa kama nafasi hiyo ya nne ingechaguliwa timu moja kutoka kisiwani humo.

Mkurugenzi kamati ya ufundi, Sunday Kayuni amesema baada ya kugundua kuwa waliteleza kwa kuiteua Azam ndiyo maana nafasi hiyo wakaipeleka Zanzibar.

''Mashindano haya ni makubaliano kati ya wadhamini na TFF kwa hiyo katika uteuzi wa awali iliangaliwa ligi hii inayoendelea sasa na kuchaguliwa timu hizo nne, alisema Kayuni.

Alisema katika mashindano ya mwaka huu Uganda haitakuwa na timu shiriki wakati timu mbili zitatoka nchini Kenya ambazo ni Tusker pamoja na Sofapaka.

Timu zitakazoshiriki michuano hiyo ni pamoja na Yanga, Simba, Mafunzo pamoja na Mtibwa ambao ndiyo bingwa mtetezi.
ba 14 hadi 27. Soma Zaidi ...

Saturday, November 14, 2009

MATOKEO YA MECHI ZA KIRAFIKI PAMOJA NA KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2010

KIRAFIKI
Italy 0-0 Netherland
Brasil 1-0 England
Spain 2-1 Argentina
N/Ireland 0-1 Serbia 0-1
Wales 3-0 Scotland

KOMBE LA DUNIA
Egypt 2-0 Algeria
Sudan 1-2 Benin
Cote d'Ivoire 3-0 Guinea
Burkinafaso 1-0 Malawi
Morocco 0-2 Cameroon
Togo 1-0 Gabon
Rwanda 0-0 Zambia
Kenya 2-3 Nigeria
Mozambique 1-0 Tunisia
Greece 0-0 Ukraine
Rusia 2-1 Slovenia
Ireland 0-1 Frans
Portugal 1-0 Boznia and Herzegovina Soma Zaidi ...

MECHI ZA KIRAFIKI LEO HII

15:00 Wales v Scotland
17:00 Brazil v England
17:30 N/Ireland v Serbia
19:30 Germany v Chile
19:45 Spain v Argentina
19:50 Italy v Netherlands

NB: saa GMT+1
Soma Zaidi ...

ELIZABETH ASEMA WATANZANIA WAMEMUANGUSHA



MSHIRIKI wa Big Brother Revolution, Elizabeth Gupta amewalawahumu Watanzania kwa kushindwa kumpigia kura za kumbakiza ndani ya jumba hilo ambalo mshindi atajinyakulia kitita cha dola 200,000.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Elizabeth alisema kuwa nchi tano zilimpigia kura, lakini Tanzania ilimuangusha kwa vile mashindano hayo wanaangalia zaidi kura zinazopigwa nchini mwako.

“Uganda, Kenya walinipigia, lakini Tanzania kura zilikuwa chache, halafu mashindano ya mwaka huu ni magumu tofauti na miaka mitatu iliyopita, safari hii washiriki ni 25 sheria zimebadilika,” alisema. Elizabeth aliongeza hakuwa na uhusiano na mshiriki mwenzake Kelvin wa Nigeria na kudai kuwa urafiki wao utabaki kuwa wa kawaida na si vinginevyo.

Eliza alisema “Kuishi na watu kazi sana kila mtu ana tabia zake, ukizingatia hakuna mawasiliano mimi sikuwa naigiza ndio tabia yangu ilivyo, lakini wapo ambao wanaigiza ingawa wote lengo letu ni kusaka fedha.

Akizungumzia minong’ono inayodaiwa kuwa yeye ni mjamzito au kabakwa alisema “ni kitu kinachoniuzunisha sana uwa kinaniliza kwa kuwa sikupata muda wa kusikilizwa, ingawa mimi nilisikiliza:

“Kubakwa si siri ila ni kitu kibaya kinahuzunisha, na mimba pia si siri kwani huwezi kuificha kwa sababu itakuja kuonekana, nilitaka niiseme siri inayoniumiza nikiwa BBA nikijua watazamaji watanisikia, lakini sikuweza kusema, kwa sasa bado iache iwe siri ipo siku nikijisikia kusema nitaisema.

Na aliweka wazi kauli yake ya kuwa hajawahi kuwa na mahusiano na mtu ambaye sio halfcast na akadai sio chuki ilopelekea yeye kusema hivyo bali ile ni reality show na alikuwa anaeleza historia ya maisha yake na huo ndo ukweli kuwa hajawahi kuwa na mahusiano na na mwafrika Soma Zaidi ...

KIFICHO AWAOMBA MAHUJAJI KUSAMEHEANA


Spika wa baraza la wawakilishi Zanzibar Alhaj Pandu Ameir Kificho amewataka wananchi wanaojiandaa kwenda kutekeleza ibada ya hija kusameheana kabla ya kwenda kutekeleza ibada hio katika miji mitakatifu ya Makka na Madina.
Alhaj Kificho aliyasemma hayo jana alipokua akizungumza katika semina ya maandalizi ya mahujaji wa mwaka huu 2009 ilioandaliwa na Al-Haramain Hajj Group, wakishirikiana na Jumuia ya Maimam Zanzibar,katika hotuba yake hio kificho alisema kusameheana ndiko kunakojenga umoja nidham na mshikamano.
"Sisi kama binaadam tunafanya makosa, makosa ambayo yanapelekea kutoelewana baina yetu katika jamii, na ni kosa kwa mtu kula kiapo cha kutokusamehe.
Mahujaji wapatao 153 wanatarajiwa kuhudhuria katika semina kwa ajili ya matayarisho ya hija, ambazo zitaishia manamo mwisho wa mwezi huu wa Novemba.Hija ni nguzo moja kati ya nguzo tano za kiislam, ambayo kila muislamu mwenye uwezo anapaswa aitekeleze angalau mara moja katika uhai wake.
Kila mwaka waislamu wapatao milioni mbili wanahudhuria ibada ya hija huko Makka sehemu tukufu kuliko zote katika Uislam.
Soma Zaidi ...

Thursday, November 12, 2009

ELIZABETH APOKELEWA KISHUJAA NYUMBANI

Elizabeth mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Mwalim Julius Nyerere
Elizabeth akiwa na mama yake maara baada ya kutua jana jioni katika uwanja wa Mwalim Julius Nyerere, Elizabeth alipokelewa kama shujaa alieiwakilisha vyema TZ katika jumba la Big Brother.

Soma Zaidi ...

Wednesday, November 11, 2009

ANUSURIKA KUFA BAADA YA KUANGUKA KWEYE NJIA YA TRENI

Mwanamke mmoja nchini marekani ambae alikua amelewa chakari alinusurika kufa baada ya kupepesuka na kuangukia katika njia ya treni, tukio hilo lilitokea katika kituo cha Nort Boston.

Mwanamke huyo alinusurika kufa baada ya watu waliokua wakisubiri treni kituoni hapo kusimamisha treni kwa kuipungia mikono baada ya kumuona mwanamke huyo ameanguka kwenye njia ya treni na kushindwa kuinuka kutokana na kuzidiwa na pombe kichwani, hata hivyo treni hio ilifanikiwa kusimama kabla ya kumponda mwanamke huyo.

Soma Zaidi ...

JE HII NDIO KAZI YA JESHI LA KUJENGA UCHUMI (JKU)?


Nijuavo mimi kazi ya hili jeshi la kujenga uchumi Zanzibar (JKU) kubwa ni kushughulikuia mashamba ya mipunga na mambo na mambo yanayofanana na hayo na sio kushughulikia mambo yanayohusu usalama wa raia, lakini katika picha hii askari wa JKU wanaonekana wakimpiga mikwaju raia huku wenye kazi ya usalama wa raia wakiwa pembeni, jee hapa JKU watakua na jibu gani juu ya hili kama si kufanya yasio wahusu
Soma Zaidi ...

MAFURIKO YAKWAMISHA MAGARI YA MISAADA KENYA

Baada ya ukame wa muda mrefu, mvua kubwa zilipoanza kunyesha katika mkoa wa kaskazini mashariki nchini Kenya zilisababisha mafuriko yaliobomoa barabara.Magari zaidi ya 40 yakiwa yamebeba chakula cha misaada ya wakimbizi wa kisomali yalikwama kutokana na kuwa barabara hazipitiki. Soma Zaidi ...

TUNAFAHAMU NINI KUHUSU MAENDELEO?

Katika kufuatilia kwangu habri katika mambo ya maendeleo ya nchi ya Tanzania nimeona kua imeelezwa sana kwenye vyombo vyahabari Tanzania imepiga hatua kimaendeleo na katika ule mpangilio wa nchi ya kwanza kwa utajiri hadi kufikia nchi masikini kuliko zote duniani nimeona kwamba Tanzania imepiga hatua, ila nimesahahu tu imeshika nambari ya ngapi.

Lakini mimi hua najiuliza kila siku hivi haya maendeleo yaliopatikana hadi kuipandisha chati Tanzania ni kwa kigezo gani? kwa sababu kwa kua mimi sio msomi na wala sio mwana uchumi ninavojua mimi tunaposemna neno maendeleo katika nchi hapa ina maana kwanza nchi ifikie jambo ambalo halikuwepo kabla hususan katika mambo ya kijamii yawe yamepiga hatua kwa mfano katika elimu, afya, maji safi umeme, n.k.

lakini tangu nianze kupata fahamu yangu nasikia Tanzania ina tatizo la umeme, na naweza kusema kwamba tangu mimi sijazaliwa inajuilikana kama tatizo la ukosekanaji wa umeme linasababishwa na kitu gani lakini hadi hivi ninavyoandika habari hizi ni zaidi ya miaka 40 kuna tatizo la umeme au haya ndio maendeleo

Katika suala la elimu hali ndio hio hio, kwa sabau mimi nakumbuka siku hizo nilipokua nasoma tulikua tukipewa vifaa vyote vya kusomea kama vitabu, mabuku, peni , penseli, n.k bure, na hakuna hata mwanafunzi mmoja katika skuli hata moja aliekua akikaa chini, lakini katika nchi hio hio iliopiga hatua katika maendeleo wanafunzi wanakaa chini na hawapewi hata penseli, kila kitu unapaswa ujinunulie mweyewe,hali kadhalika hivo ndivyo ilivo katika kila jambo linalohusu jamii.

Ukiangalia kila siku nchi hii inazungumza huyu kaiba bilioni mia ngapi na huyu kaiba bilioni mia ngapi wanaita ufisadi sasa je hakuna mambo ya kushughulikia zaidi ya huu ufisadi usiokwisha? au hizi ni njama maalum zilizotengezwa ili kuzubaisha watu akili? kwa sababu kama huu ufisadi mbona hakuna hata mmoja aliehukumiwa? mbona viongozi hawafatilii mambo muhimu ya kijamii wameshika tu ufisadi ufisadi ufisadi, au maendeleo yenyewe ndio haya ya kutueleza mambo ya ufisadi kila siku na hizi kelele za kumuenzi Nyere zisizokwisha?

Maendeleo haya yanayozungumzwa yamepatikana katika kitu gani? au ni yale majumba makubwa yanayojengwa katika mji wa Dar-es Salaam? mimi sijui, naomba wataalamu wa mambo ya uchumi wanifahamishe.

Mzanzibari halisi. Soma Zaidi ...

Tuesday, November 10, 2009

AMCHINJA MWENZIWE NA KUMLA

Kijana mmoja anaejuilikana kwa jina la Tadeus Mushi wiki iliopita alimchinja ndugu yake na kumla, tukio hilo lilitokea katika kijiji cha Tindi huko Moshi.

Soma Zaidi ...

Monday, November 9, 2009

ABDI NA SAIDA WAFUNGA NDOA GEMENTE ALMELO

Kutokana na mshika veli kuingia mitini ilibidi wenyewe tufanye kazi hio
Ommykiss, Said, Couchmanu, na Dulla tulipata kumbukumbu baada ya harusi

Nabiel pamoja na visheti kama kawaida
Bwana harusi Abdi na Bibi harusi Saida wakiweka kumbukumbu kabla ya harusi

Licha ya baridi lakini watu walionekana ni wenye furaha
Taswira baada ya harusi
Ali chuchu Mani Dulla pamoja na mpiga picha Said nao pia walipata kumbukumbu muhimu
Majirani marafiki pamoja na wafanyakazi wa Gemente katika picha ya pamoja (mwanamke mwenye shati nyeusi na flana ya pink ndie alieozesha)

Bwana na bibi harusi wakikubaliana kuishi pamoja

Abdi akimwaga wino

Saida nae pia alimwaga wino
Mambo ya ndoa
Soma Zaidi ...

ELIZABETH NJE BIG BROTHER

Hatimae mshiriki pekee kutoka Tanzania ndani ya jumba la Big Borother Elizabeth ameondoka rasmin katika jumba hilo baada ya kukosa kura za kuweza kumbakisha.
Elizabeth ameaga rasmin shindano hilo lenye donge nono la zawadi huku akiwaacha marafiki zake Emma na Kevin wakiwa katika vilio na huzuni.Pia nae Elizabeth alipokua aakihojiwa kwa mara ya mwisho na IK juu ya nini amejifunza ndani ya jumba hilo Elizabeth alisema amejifunza kupata marafiki wazuri katika muda mchache.

Soma Zaidi ...

Sunday, November 8, 2009

HONGERA FARID

Kwa mara nyengine tena Manchester washindwa kutamba Stamford Bridge baada ya kufungwa bao 1-0 na Chelsea Soma Zaidi ...

MECHI ZA UINGEREZA LEO HII

13:30 Hull City vs Stoke City 15:00 West Ham United vs Everton 15:00 Wigan Athletic vs Fulham 16:00 Chelsea vs Manchester United Mechi ya leo kati ya Chelsea na Manchester United imekua kivutio kikubwa kutokana na timu hizo kwaza kila moja inataka kushika nafasi ya kwanza, pili kwa upande wa Chelsea inataka kuendeleza rekodi yake ya kutofungwa na Manchester katika uwanja wake Stamford Bridge, itakumbukwa kwamba ni misimu saba imepita ya ligi kuu, Chelsea hahaijawahi kufungwa nyumbani na Machester United. Nao Manchester United wanataka kuvunja rekodi hio kwani katikamisimu sita ya ligi kuu ni magoli mawili tu ndio waliopata wakiwa Stamford Bridge,wakiwa wameshindwa kuondoka na ushindi Stamford Bridge kwa mechi 13. Sir alex Ferguso ameshinda dhidi ya Carlo Ancelotti mechi moja tu na kufungwa mechi tatu kati ya mechi nne walizokutana.
Soma Zaidi ...

KISA CHA DA'I NA BABA YAKE IMAM

Ndugu zangu wapendwa,
Assalaam Alaikum Wa Rahmatullahi wa Barakatuh
Bila shaka ukisoma kisa hiki utalowa kwa machozi kama vile hisia hizo zilivonipata. Naomba Mwenyezi Mungu Atuongoze katika njia nyoofu na Atuzidishie Imani katika dini yetu hii na kwa jitihada kubwa tumuamini Yeye Allah SWT. Amiin ya Rabbil ‘Alamiin
Kwa yeyote ataesoma, basi aitangaze kwa namna yeyote ili wengine wafaidike.

Fanyeni subra na someni hadi mwisho.

Qur’an 3:104: Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa

Qur’an 16:125 Waite waelekee kwenye Njia ya Mola wako Mlezi kwa hikima na mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora. Hakika Mola wako Mlezi ndiye anaye mjua zaidi aliye ipotea Njia yake, na Yeye ndiye anaye wajua zaidi walio ongoka

Kisa cha Da’i na Baba yake Imam
Kila Ijumaa adhuhuri baada ya salaa na Huduma za Ijumaa katika Msikiti Mkuu, na punde baada ya kipindi cha mafundisho ya “familia” (al Usrah), Imamu na mwanae wa kiume mwenye umri wa miaka kumi na moja, hutoka na kwenda nje mitaani kugawa vitabu vidogo vidogo kuhusu “NJIA YA PEPONI” na vitabu vingine vya mafundisho ya Kiislamu.
Katika adhuhuri yenye kheiri ya Ijumaa moja, wakati ulipofikia Imam na mwanae kwenda kugawa vitabu, hali ya hewa nje ilibadilika na kuwa baridi kali na mvua kubwa.
Mtoto yule alijitayarisha kwa mavazi yake ya kumhifadhi joto na mvua, kasha akasema, “OK baba, mimi ni tayari”
Imam, Baba yake akauliza, “uko tayari kwa ajili gani?” “Baba ni wakati kukusanaya vitu vyetu na kwenda nje” Baba yake akasema, “Mwanangu, nje kuna baridi kali na mvua kubwa” Mtoto yule akamtizama baba yake kwa mshangao. Na akasema, “ baba, watu hawatoingia Motoni kama mvua ina nyesha?”
Baba akajibu, “mwanagu sitoweza kutoka nje na hali ya hewa kama hii!”
Kwa kusononeka, mtoto akamuomba baba yake, “ baba mimi naweza kwenda mwneyewe?” Baba yake alisita kwa muda kisha akasema, “mwanangu unaweza kwena, vitabu hivi hapa. Uwe muangalifu” “Shukran baba.”
Baada ya hapo mtoto yule alitoka nje katika mvua ile. Mtoto huyo wa miaka kumi na moja alipita mitaa ya mji ule akigonga mlango hadi mlango akigawa kitabu kwa kila alie kutana nae.
Baada ya masaa mawili hivi kutemebea katika mvua, alilowa chepe na kupata baridi kali, aligawa hadi nakala ya mwisho aliyo bakia nayo mkononi. Alisimama katika pembe moja na akitizama kama kuna mtu atatokea ili aigawe nakala ile iliyobakia, lakini mitaa ilikuwa kimya kabisa bila wala mtu mmoja.
Aligeuka kuelekea katika nyumba ya mwanzo aliyo iona karibu na kuanza kutembea pembezoni kuelekea katika mlango wa mbele, ailgonga kengere, lakini hakuna alieitikia. Aligonga tena na tena laikini hakuna aliejibu. Alisubiri lakini bila jibu. Mwishowe. Mtoto huyo (Daa’i), aligeuka kutaka kuondoka lakini akahisi kitu na kusubiri. Tena aliugeukia mlango na kugonga kengere na kugonga malango kwa mkono wake kwa sauti kubwa. Alisubiri kidogo, kuna kitu alichohisi kutoka katika ukumbi wa mbele wa nyumba ile. Aligonga tena, mara hii mlango ulifunguliwa taratibu.
Aliesimama mlangoni ni mwanamke mtu mzima alie onekana ni mwenye masikitiko. Aliuliza kwa ulaini, “Nikusaidie nini mwanangu?” Kwa uso mkunjufu na tabasamu, mtoto yule akasema, “Mama samahani kama nimekusumbua, lakini napenda kukuambia kwamba Allah kwa hakika Anakupenda na Anakulinda, na nimekuja tu kukupa kitabu changu cha mwisho ambacho kitakufundisha yote kuhusu Allah na nini lengo la Uumbaji na vipi upate Faraja Zake” Mtoto yule alimpa mama yule kitabu na kugeuka kuanza kuondoka.
Mama yule alimwita (mtoto) wakati anaondoka, “Ahsante mwanangu! Na Mwenyezi Mungu Akubarikie”
Ijumaa iliyofuatia baada ya Salaa ya Ijumaa, katika kipindi kile cha wiki cha “familia”, Imamu alitoa Da’wa kama kawaida yake. Alipomaliza aliuliza, “kuna mtu ana swali lolote au ana kitu che chote anataka kusema?”
Taratibu, kutoka safu ya nyuma ya wanawake, sauti ya mtu mzima ilisikika katika spika. Sauti nzuri , safi na furaha ilio kuwa dhahiri japokuwa haonekani, alisema, “Hakuna katika mkusanyiko huu anae nifahamu wala sijawahi kuonekana humu, hapo qabla. Ijumaa iliyopita sikuwa Muislamu na nilifikiri ningekuwa. Mume wangu alifariki muda umepita. Aliniacha peke yangu katika dunia hii. Ijumaa iliyopita, vile ilivyokuwa siku ya baridi na mvua, basi ilikuwa kushinda hivyo ndani ya moyo wangu, kiasi kwamba nilifikia kikomo cha matumaini ya kuishi.
Hivyo nilichukua kamba na kiti kupanda ngazi hadi kufikia sakafu ya juu ya nyumba yangu. Niliifunga kamba imara katika mwamba wa wa sakafu lile la juu, kisha nikasimama juu ya kiti na kuifunga upande wa pili wa kamba katika shingo yangu. Nilisimama juu ya kiti kwa upweke na niliye vunjika moyo. Nilikuwa karibu kutegua kiti, pale kwa ghafla nilisikia mlio mkubwa wa kengere ya mlangoni kutoka chini ikinikera. Nikafikiri kuwa yeyote ataekuwa atakwenda zake. Nilisubiri na kusubiri lakini sauti ya kengere ilizidi na kukazana, kisha mtu anaegonga kengere alianza kugonga mlango kwa sauti kubwa. Nikajisemea, ‘nani katika dunia hii anaweza kuwa? Hakuna mtu alisha wahi kugonga kengere wala kuja kunitizama’ Niliiregeza kamba shingoni, nikaivua na kushuka chini hadi mlango wa mbele. Wakati wote huo sauti ya kengere ilizidi.
Nilpofungua mlango na kutizama, sikuamini macho yangu kumuona mvulana mzuri mwenye furaha amabe sijawahi kumuona katika maisha yangu. Tabasamu yake. Oh! siwezi kuifafanua. Maneno aliyo nitamkia yaliufanya moyo wangu ulio kuwa umekufa muda mrefu, KUIBUKA KATIKA UHAI, kwa sauti yake ya ajabu, “Mama nataka tu kukuambia kwamba ALLAH KWA HAKIKA ANAKUPENDA NA ANAKULINDA” Kisha alinipa hiki kitabu, “Njiia ya kwenda Peponi” ambacho hivi sasa ninacho mkononi.
Mtoto yule (Malaika) mwema alivotoweka ndani ya baridi na mvua ile, nilifunga mlango na nikasoma kwa uangalifu kila neno ndani ya kitabu hiki. Kisha Nilirudi juu kuchukua kamba yangu na kiti changu. Sikuvihitajia tena.
Mnafahamu? Sasa mimi ni mwenye furaha na mwenye kumuamini Mungu Mmoja. Kwa kuwa anwani ya mkusanyiko huu imeandikwa nyuma ya kitabu hiki, nimekuja hapa mwenyewe kukushukuru kwa Mwenyezi Mungu wa Malaika yule mdogo ambae alikuja katika sekunde za muda wa mwisho na kwa kufanya hivo alisalimisha roho yangu isiingie katika Moto wa milele.
HAKUKUWEPO MACHO MAKAVU TENA HUMO MSIKITINI. Saut za TAKBIIR, ALLAHU AKBAR, zilipaza hewani hata miongoni mwa wanawake pia.
Imam, Baba alishuka kutoka katika mimbari hadi katika safu ya mbele sehemu aliyo kuwa ameketi malaika yule mdogo. Alimchukua mwanae na kulia bila kujizuia.
Bila shaka hakuna jamaa iliyowahi kupata kipindi chenye furaha kama hiki, na bila shaka ulimwengu haujawahi kamwe kuona Baba ambae alijaa na mapenzi na radhi ya mwanae, ila mmoja, huyu mmoja.

Macho yenu yabarikiwe kwa kusoma kisa hiki. Msikifanye kisa hiki kikapotea, someni tena na tean na muwanufaishe wengine. Pepo ni kwa ajili ya Watu wake.
Kumbuka kwamba, Resala ya Mwenyezi Mungu hufanya mabadiliko katika maisha ya mtu alie karibu nawe. Isambaze resala hii kwa wingi uwezavyo.
Sambaza Resala za Mwenyezi Mungu na utaona manufaa kwa kila ufanyacho.

Qur’an:5:3 ……..Leo walio kufuru wamekata tamaa na Dini yenu; basi msiwaogope, bali niogopeni Mimi. Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini. Na mwenye kushurutishwa na njaa, bila ya kupendelea dhambi, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehevu na Mwenye kurehemu

Qur’an:3:110 Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa Watu wa Kitabu nao wameamini ingeli kuwa bora kwao. Wapo miongoni mwao waumini, lakini wengi wao wapotovu

Aya zingine katika Qur’an: 29:46; 4:82; 60:8; 3:111; 39:19

Bibilia
Is 43:11; Ez 1820; Joh 5:30; Act 2:22; Joh 17:3; Jam 2:17; finally, Jer 8:8.

Mwenyezi Mungu Akujaaliyeni muwe wenye kufuzu hapa duniani na huko Akhera, Amiin Soma Zaidi ...

Friday, November 6, 2009

WAZANZIBARI TUNATAKA DOLA YETU, SIO HATI YA MUUNGANO

Umoja wa Wazalendo

“Na shikamaneni kwa Dini ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane…”.

Wazee wetu, Ndugu zetu;

Assalaamu Alaaykum,

UMOJA, UHURU, UADILIFU

KUVAMIWA NA KUMEZWA DOLA HURU YA ZANZIBAR

Kwa Rehma za Mwenyezi Mungu na juhudi za Wazalendo, Zanzibar ilipata Uhuru wake, Disemba kumi, 1963 na kujiunga na Umoja wa Mataifa Disemba kuminasita, 1963; ikiwa ni Dola Huru Kaamili yenye Kiti chake na Bendera yake, na kila lake.

Siku 33 baada ya hivi kupata Uhuru wetu, yaani Januari 11, 1964 jeshi la Nyerere liliivamia Zanzibar na kuleta mauwaji ambayo hayajapata kutokea katika historia ya Zanzibar. Mara tu baada ya mavamizi haya, April 24, hiohio 1964, Nyerere alitufanyia Aprilfool Wazanzibari kwa kuleta zile “Articles of Union, 1964”, hivyo kwa kisingizio cha huu wenyekuitwa muungano wakaimeza Nchi yetu kikamilifu. Kutokana na uovu huu, ndipo Waziri Mkuu wa Tanganyika, Mhishimiwa Pinda kutangaza na kusisitiza kwamba “Zanzibar si Nchi”. Tangu sikumosi ya khiyana kuu hii, Tanganyika ilioifanyia jirani yake Zanzibar; Wazalendo wa Kizanzibari wamekikanya kitendo kiovu hiki na kudai kurejea Dola Huru Kaamili ya Zanzibar.

Mara tu baada ya uovu huu, mengi yameandikwa, na mengi yamesemwa na watu mbalimbali; kukhusu “uhalali wa huu wenyekuitwa muungano” (the legality of the union). Wote hao, hapana hata mmoja aliekuwa na nguvu za hoja kuhalalisha haramu hii, haramu ya kuvamiwa Zanzibar na haramu ya kumezwa Dola ya Zanzibar.

Mjadala umeendelea kukhusu kuwepo khati ya muungano iliosainiwa na Mzee Karume pamoja na yeye Mwalimu Nyerere, wawili ambao ndio waliofanya khiyana hii. Mpaka hivijuzi, sirikali ya Zanzibar na sirikali ya Tanganyika wameendelea kukiri kwamba hakuna khati iliosainiwa na mabwana wawili hawa. Hali yenye kushangaza ni hivi ghafla kuona maneno haya yanasemwa na mkoloni mvamizi, Tanganyika:

“SERIKALI imesema mkutano ujao wa bunge itagawa kwa wabunge pamoja na kuweka katika maktaba mbalimbali pamoja na makumbusho Hati ya Muungano kwa kuwa ni haki ya kila mtu kuufahamu mkataba huo……….”.

Wazanzibari, hatuna mjadala kukhusu khati ya muungano, ipo au haipo; au uhalali wa muungano. Kwa Wazanzibari la asili na la hakika ni kwamba hapakuwa na muungano, bali ni kumezwa Dola Huru ya Zanzibar. Kwahivyobasi, Wazanzibari wanachotaka na wataendelea kukiwania mpaka tukipate, ni kurejea Dola Huru Kaamili ya Zanzibar. Irejee kama ilivyokuwa ilipopata Uhuru wake na kujiunga na Umoja wa Mataifa, Disemba, 1963 ikiwa ni Dola Huru Kaamili, yenye Bendera yake na Kiti chake sawa na Dola nyengine yoyote ile katika Umoja huu wa Mataifa.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu, Subhaanahu wa Taáala atujaalie kila la kheri na atuepushe na kila shari; na atujaalie ufunguzi wa karibu, Aamyn Yaa Rabbi.

Wa Billahi Tawfiiq

Umoja wa Wazalendo

Zanzibar,

Ijumaa Novemba 06, 2009

“…. وأمرهم شورى بينهم ……”.

“….., na mambo yao yakawa ni kwa kushauriana baina yao,…..”. Soma Zaidi ...

SIEF SHARIF AKUTANA NA AMANI KARUME


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Amani Abeid Karume leo amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Chama cha CUF, Maalim Seif Sharif Hamad huko Ikulu, Mjini Zanzibar.Katika mazungumzo hayo, ambayo hayakutarajiwa na wengi wawili hao yaligusia mambo mbali mbali ikiwa ni pamoja na haja ya kudumisha amani na utulivu nchini na maelewano na mashirikiano kati ya wananchi wote.

Viongozi hao wamezingatia haja ya kuzika tofauti zilizopo ambazo zinachangia kuwatenganisha Wazanzibari na kutoa wito kwa viongozi wa vyama vyote vya siasa na wananchi kwa jumla kushirikiana katika kujenga nchi bila ya kujali itikadi zao za kisiasa.

Viongozi hao walifafanua kuwa wananchi wakishirikiana na kujenga nchi kwa pamoja, watapiga hatua kubwa zaidi za maendeleo.Katika mazungumzo hayo, viongozi hao walihusisha umuhimu wa mchakato wa mazungumzo endelevu baina yao na vyama vyao kwa jumla. Soma Zaidi ...

USAFIRI WA WENZEU


Soma Zaidi ...